CHADEMA inatumia koti la UKAWA kujikongoja kisiasa

CHADEMA inatumia koti la UKAWA kujikongoja kisiasa

Acha hizo....hakuna kitu kama hicho...cuf wako vizur..na tunaunga mkono mabadiliko na mwaka huu ukawa ndan ya nyumba
 
HAPANA, UKAWA ni mkakati kamambe wa kuiuwa CCM

RIP CCM
 
ndugu wana jf tumeshuhudia muungano wa vyama vya upinzani kama chadema,cuf na vingine vinavyounda UKAWA.lakini kwa kadri muda unavyoenda tunaona baadhi ya vyama ndani ya ukawa kama CUF vikizidi kupoteza umaarufu na mvuto tofauti ilivyokuwa zamani.Tunaona hata wanachama wapya wanaojiunga UKAWA wote wanachukua kadi za CHADEMA,hatuoni wakielekezwa kuchukua kadi za vyama vingine ndani UKAWA.Nilitegemea ujio wa Lowasa ndani ya UKAWA pamoja na team zake Kama 4u mvt na friends of Lowasa kila chama kingegawana wanachama ili kuleta uwiano.Ndani ya UKAWA CHADEMA imejinufaisha kwakujipatia umaarufu na wanachama.vyama vingne vimesahaulika kama CUF chama chenye nguvu kabsa Zanzibar. nimalize kwakuuliza swali.
JE KUUNDWA KWA UKAWA NI MKAKATI WA SIRI WA CHADEMA KUIUA CUF NA VYAMA VINGINE VYA UPINZANI?

Kumbuka CUF imekua imara muda wote, hasa Zanzibar. Na kipindi hiki baada ya October 25, kitakua chama tawala Zanzibar, na cha kishiriki katika Serikali kuu ya Jamhuri wa Mungano (UKAWA). Sasa hapo ni chama kipi kimenufaika zaidi km si CUF. THINK BIG!!!!
 
Nadhani wakati naandika mada mbalimbali humu kuwa CUF na NCCR mnatumiwa na CHADEMA kama karai la zege mlinibeza sana sasa imekula kwenu. MBOWE, MAALIM SEIF NA JUMA DUNIA HAIJI kawapiga bao la kisigino. CUF na NCCR byebye.
 
Bro, tumieni huu wakati vizuri kwa kumjenga MAGUFULI wenu!!! UKAWA iacheni sasa!
 
ELIMU YA MBOWE NI ZAIDI YA PHD

Mbowe ni form six failure lakini ni mjanja kuliko watu wenye Phd zao Ukawa. Ona sasa alivoiua NCCR na CUF ndani ya mwaka mmoja. Peter Msigwa aliwahi sema mtu yoyote atakayempigia kura Lowasa akapimwe akili na mimi sidhan kama Mbowe,Mnyika na Lissu wana vichaa kiasi hicho cha kumpigia kura katuni.

Watu wanataka ruzuku alafu mapimbi wamekalia "Lowasa mabadiliko, mabidiliko Lowassa" Poleni sana msiojitambua, hamumjui Mbowe.
 
[h=2]MAGUFULI ATINGA MKOANI GEITA[/h]
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji mdogo wa Katoro kwenye mkutano wa kampeni uliofanyika viwanja vya Mnadani, mkoani Geita.
​
Mgombea wa Urais kupitia CCM Dk. John Pombe Magufuliakiwapungia mkono maelfu ya wakazi wa mji mdogo wa Katoro kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia wananchi hao kuwa anataka kuijenga Tanzania mpya ya Viwanda, pia katika serikali yake itaongeza maeneo ya wachimbaji wadogo na kuwawezesha ili waweze kuchimba vizuri.
​
Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Geita Ndugu Joseph Msukuma akihutubia wakazi wa Katoro kwenye mkutano wa kampeni za CCM za kumnadi mgombea wa Urais wa CCM Dk. John Pombe Magufuli.
​
Umati wa wakazi wa Katoro ukifuatilia mkutano wa Dk. John Pombe Magufuli.​
 
Mbowe ni genius! Kinachoendelea kwenye siasa za Tanzania, kinasaidia sana kumwonyesha Mbowe katika ubora wake, siyo ukabila lakini kuna wakati Wachaga wapewe sifa wanazo stahili. Mbowe anafahamu hesabu na anachanga karata zake na kuzicheza vizuri sana!

Sijui kwa wengine lakini, kusema kweli mimi naona urafiki wa Mbowe na EL siyo wa kudumu. Baada ya October 25, litajengwa 'tofali' jipya katika ujenzi wa democrasia ya vyama vingi Tanzania bila kujali itashinda UKAWA au CCM! Muungano wa UKAWA na EL, una nia moja tu kupunguza absolute power ya CCM na kama siyo CCM kufa basi iwekwe kwenye viwango sawa na vyama vingine.

Anyway u-genius wa Mbowe upo wapi? Ni kwenye 'usajili!' EL, 2015 kama Slaa mwaka 2010, ni 'mchezaji' mkali ambaye unaweza kumtumia sasa kubeba ubingwa wakati ukiendelea kukuza vipaji! Kuna fursa Mbowe ameiona, ambayo hata Slaa hakujua 2010 kwamba alikua 'usajili' wa msimu ule! Mbowe ni 'mtaalamu' hata ukimwita jina gani, au useme ameuza chama, kwa kazi ya mwenyekiti wa chama ni nini?! Uza chama, I mean, uza chama!! Wakati kuna watu vyama vinawadodea na kuwafia mikononi, Mbowe anauza chama.............chema chajiuza!

Hongera Mbowe, wacha EL akusogeze, kama siyo kukamata nchi mwaka huu, lakini mwendo huu, lazima utakua karibu! Mbowe amecheza, ni bonge la kocha, na Lazima tumpe pongezi zake!
 
Mabadiriko ni wewe mwenyewe unajua chadema wamejificha ktk kichaka cha ukawa lakini mgongo unaonekana!! Ukawa ni umoja wa majizi ya kasikazini na majambazi ya ndani na nje ya nchi yanayotaka kupora mali zetu.
 
Mleta mada nenda kashikishwe ukuta tu hiyo ndy kazi yako...pumba...v
 
Ni Kweli unayosema (MABADIRIKO ni wewe Mwenyewe) Ila sisi UKAWA tunataka MABADILIKO
 
Wewe ulikuwa unatushauti chichi tuchague chama gani. Chichi chichiemu hatutaki
 
Dhambi iliyofanywa na UKAWA ya kuwatupa nje wagombea urais wa ukweli, kama jinsi mfumo ulivyokuwa umetengenezwa.

Kwamba Dr. Slaa angebeba mikoba ya ukawa itaendelea kuitafuna ukawa miaka nenda rudi.

Kama tumeshindwa kuisimamia mifumo yetu wenyewe tena midogo tu ya ndani, tutawezaje kusimamia mifumo ya nchi. Ni uendawazimu tuu.

Acheni kudanganya wananchi.

Watu wote waliopo nyuma ya mifumo ya kifisadi iliyopokelewa kutoka CCM wako midomo wazi wanasubiri Lowasa kama akiingia ikulu waanze kupiga hela. Wakiongozwa na DJ wetu Mbowe. Ni hatari sana kwa nchi.

Ndio maana salama yetu itakuwa baada ya uchaguzi tutaifumua yote na kuunda upya. Hapo ndipo anguko la CHADEMA Mafisadi litakapotokea ma kuibuka CHADEMA asilia chini ya uongozi makini
 
Back
Top Bottom