Mungi
JF Gold Member
- Sep 23, 2010
- 16,980
- 9,560
Heri ya Krismas wadau,
Nimefuatilia kwa kina comments za wadau wa jukwaa hili kufuatia mwanajeshi aliyepiga picha na Lema kwenye mkutano wake pale Mererani.
Katika mazingira ya kawaida tunaweza kusema kumbe hata jeshi limeguswa na ugumu wa maisha, ama kumbe ndani ya jeshi kuna baadhi ya maafande nao wanachukizwa na utawala mbovu wa serikali ya chama cha mapinduzi.
Lakini katika sakata hili la mwanajeshi wa JWTZ kuonyesha mapenzi take kwa chadema, na kudhiriki hata kutamka wazi kuwa yupo tayari hata kufukuzwa kazi ya jeshi kwa ajili ya chadema iangaliwe kwa macho mawili kumtambua vizuri kama ni kweli ana mapenzi ya dhati na chadema, na siyo kwamba anatumiwa kwa ajili ya kuihujumu chadema.
Inawezekana kabisa kuwa labda ni kweli ameguswa na ugumu wa maisha, ama amechukizwa na utawala mbovu wa Jk ambao umesababisha ugumu wa maisha kwa wananchi wakiwamo familia ya mwanajeshi.
Ikumbukwe kuwa Makamba alishawahi kutamka wakati wa kampeni.za uchaguzi 2010 kuwa CCM wana mbinu zaidi ya 100 kuitawala Tanzania.
Pia ikumbukwe kuwa ni majuzi tu tuliweza kusoma tuhuma mbalimbali kupitia mtandao huu juu ya tuhuma zinazowahusu viongozi na wanachama wa chadema kuihujumu chadema.
Ni ukweli usiopingika kuwa hata mkuu wa nchi ankubali kuwa chadema ni tumaini la watanzania. Sasa katika muktadha huo mwanya unaweza kutumika kuwahadaa wananchi, inawezekana amekuja kufanya kazi maalum.
Kauli ya mwanajeshi huyu kusema kuwa yupo tayari kufukuzwa kazi kwa ajili ya kuishabikia chadema inanipa mashaka, mwanajeshi wa jwtz. Inanifanya niamini kuwa yupo kwa kazi maalum kumdadisi au kufiatilia nyendo na kauli za Lema na viongozi wa chadema, pia ili afanikiwe kazi yake maalumu ni lazima atafukuzwa kazi, ambapo chadema na Lema wanaweza kuwekeza imani kwa mwanajeshi huyo. Maana yake ikigundulika kuwa ni kweli ni mwanajeshi wa Jwtz kwa mujibu wa sheria za jeshi adhabu atakayopewa ni kufukuzwa kazi.
Lakini kwakuwa ni kazi maalum, kitakachofanyika itakuwa ni kufukuzwa kazi kama kiini macho, huku akiendelea kupokea mshahara wake kama kawaida, huku akiendelea kukusanya habari na kuripoti kwa waliomtuma.
Kitendo cha Lema kurudi mjengoni kimewaumiza sana serikali ya CCM.
Mfano leo nilikuwa mahali wadau fulani wa taasisi nyeti walikuwa wanazungumza kwamba Lema lazima aundiwe zengwe kwa namna yoyote ile, niliposikia vile nikaanza ku-refer na mjeshi nikaona kuna mchezo.
All in all chadema inaaminika kwa sera za wazi bila kificho, hivyo hata wangeletwa FBI bado ingekuwa shida kwakuwa chadema kimejiwekeza kwenye mioyo ya watanzania, na kubwa zaidi chadema ina mkono wa Mungu.