CHADEMA inataka kwenda Ikulu kufanya nini?

CHADEMA inataka kwenda Ikulu kufanya nini?

Mawazo yako yanatofautiana sana na Nape.. Nadhani unaweza usilipwe leo. Huwa hampigwi msasa kidogo ili kuendana na mawazo ya wenye CCM?

tofauti na chadema , CCM ni chama huru katika lengo moja, kila mtu yupo huru kutoa mawazo yake yakakubalika, chama ni cha wote hakuna wenyewe kama nyie huko ambako chama kina wenyewe na ukijaribu kupingana mawazo na wenyewe yanakukuta kama yalivyowakuta tunaowaona sasa, karibu katika chama huru...
 
mkuu sijui wewe unaishi pori gani maana kama unaishi Tanzania lazima utaona maendeleo yaliyofanyika tokea enzi za Uhuru na serikali ya CCM, wewe pia mpaka kujitambua ni mojawapo ya matunda ya serikali yetu kutoa elimu bora kwa wananchi wake

Haujajibu swali langu ni ofisi au Jengo gani CCM kama CCM wamejenga?Mimi ni Mtanzania halisi na ninayeishi Tanzania na ninalipa KODI sahihi kwa ajili ya maendeleo ya nchi yangu.CCM bila kodi yangu haifanyi kitu.Sasa unijibu jengo au ofisi ipi ilijengwa na pesa ya CCM?Je wajua hata vile vitega uchumi vilivyoanzishwa na CCM viliisha jifia siku nyingi kwa msemo CHUKUA CHAKA MAPEMA (CCM)
 
Ni malengo ya kila chama cha siasa kutaka kushika dola. Pamoja na Lengo Hilo kuu vyama pia huwa na sera mbalimbali ambazo hasa ndio huwa dira ya malengo makuu ya kushika dola!

Hii huonyesha mipango ya Muda mfupi na mrefu ya kuleta maendeleo kwa wananchi! Mipango hii ndio hasa hutakiwa kutangazwa sana kwa umma ili ujue ni kwa nini Chama hiki kinaitaka dola!

Nachelea kusema Kuwa CDM wamekosa Hoja zenye mashiko kwa upande huu muhimu, wamekuwa ni wazuri sana kwa Hoja za kudandia na siasa za kushambulia bila kutuambia wao watafanya miujiza gani kwani mambo Mengi wanayoikosoa ccm wao pamoja na uchanga wao wanayafanya kwa Kasi Kubwa.

Mambo hayo ni pamoja na ubinafsi, ufisadi, matumizi mabaya ya maharaja, upendeleo, matumizi mabaya ya fedha za umma, kutoshaurika na mengine Mengi tu.

Sasa badala ya Kujibu kwa matusi na kejeli naomba CDM mtuambie mnataka kwenda ikulu kufanya nn? Mtakuwaje tofauti na mlivyo Sasa? Ni kwann watz wasiseme heri "zimwi likujualo halikulli likakwisha"?

jiulize kwa nini ccm wanatumia nguvu nyingi sana kuua au kusambaratisha chadema? Je,wanakatalia madarakani kuna nini? Wanafikia hatua ya kutugawa watz kwa dini au makabila yetu,kuasisi ugaidi na kulipua watu kwenye mikutano ya chadema,je ikulu kuna nini? Ukiweza kujibu haya tutakuambia lengo la chadema ni lipi
 
wanataka kumsaidia mama yako aliyopo kijijini apate ruzuku,umeme,maji na aache kutumia jembe la mkono
 
Wenzako wanajiuliza kwanini c.c.m haipendwi na wananchi lakini hawapati jibu!,nawe unakuja na hadithi uchwara hebu jiulize wewe uko c.c.m unafikiri unaweza kuwa na ushauri gani? Ikiwa majangili hawa watashindwa uchaguzi 2015?.kama unabisha nenda vijijini ujionee jinsi chadema inavyokubalika. Hakika 2015 c.c.m kitakuwa chama cha upinzani.
 
Chadema ni zaidi ya imani tunavyoiamini watanzania wote,hivyo unayepinga wewe mzee wako atakuwa ana nufaika na matunda ya c.c.m ya ujangili,ufisadi,madawa ya kulevya,utesaji wa raia na wandishi,kubambikizia wapinzani kesi za ugaidi na mengine mengi unayoyafahamu.
 
ukijua baba yako aliamua kuoa kwa sababu gani utajua sababu ya chama kutaka kushika dola! sawa boya!
 
kwanza nimelazimika kukudharau kabla ya kukuelekeza kusoma ILANI YA UCHAGUZI YA 2010 ya cdm , majibu ya upuuzi wako huu yamo mle .
 
Chadema ni zaidi ya imani tunavyoiamini watanzania wote,hivyo unayepinga wewe mzee wako atakuwa ana nufaika na matunda ya c.c.m ya ujangili,ufisadi,madawa ya kulevya,utesaji wa raia na wandishi,kubambikizia wapinzani kesi za ugaidi na mengine mengi unayoyafahamu.

wanaounga mkono ccm hivi sasa ni ama viongozi wake au watoto wao , hakuna mwingine !
 
TAFAKARI: Kama hapa ndio Makao makuu ya Chama, Je mikoani pakoje? CHADEMA si mnapata ruzuku kwa miaka 10 na kwasasa!!? Kama mmeshindwa kujenga makao makuu yenye hadhi. Je, mtaweza kuijenga Nchi?

NB:
Sijui hali ya Ofisi za CHADEMA Mikoani zikoje tu.

Kwa hili mkuu nakuunga mkono. Chama kikubwa kama CHADEMA hakipaswi kuwa uswahilini kama hapo. Hata kwa harambee walitakiwa wawe na jengo kubwa at least kama Mawasiliano Towers. Hata TAMWA wanamiliki ofisi nzuri na kubwa kuliko CHADEMA amabayo mapato yake ni makubwa zaidi ya TAMWA.
 
Kimoja ambacho kiko wazi ni kuwa watahalalisha unywaji wa gongo na hivyo kuathiri nguvu kazi ya taifa and eventually, taifa kuporomoka.
 
TAFAKARI: Kama hapa ndio Makao makuu ya Chama, Je mikoani pakoje? CHADEMA si mnapata ruzuku kwa miaka 10 na kwasasa!!? Kama mmeshindwa kujenga makao makuu yenye hadhi. Je, mtaweza kuijenga Nchi?

NB:
Sijui hali ya Ofisi za CHADEMA Mikoani zikoje tu.

Dogo acha ujinga,inaonekana hujasoma historia,leta picha z TANU ilipokuwa imeanzishwa,na ujue ccm ilitumia resources mbalimbali ilipokuwa chama pekee,jitahidi kuwauliza baba yako na mama yako,mana inaonekana ulizaliwa baada ya vyama vingi na hukusoma somo la historia,au umeamua kwa makusudi kuchagua ujinga!
 
kimoja ambacho kiko wazi ni kuwa watahalalisha unywaji wa gongo na hivyo kuathiri nguvu kazi ya taifa and eventually, taifa kuporomoka.

muulize mama yako hakukusomesha kwa gongo? Hoja nyingine vijana mnazikumbatia hazina mantiki!kwakuwa nyinyi mnakunya ma whisky kwa kodi zetu hata gongo mnataka isihalalishwe?
 
Si walishasema wanataka kwenda IKULU kuhalalisha GONGO au mmeishasahau mara hii tu?
 
what a question, ni kama kuuliza hivi unaenda chooni kufanya nini!
 
Si walishasema wanataka kwenda IKULU kuhalalisha GONGO au mmeishasahau mara hii tu?

Tusijitoe ufahamu kiasi hicho! Angalieni manifesto za CHADEMA VS VYAMA VYENU, Being CCM au chochote utajua mwaka 2010 walkuwa wanaplan kufanya nini, then andika thread yako!

Thread ikae kisayansi, sio kimajungu kama ulivyo wasilisha, au ndio kusudio lako?
 
Back
Top Bottom