CHADEMA inataka kwenda Ikulu kufanya nini?

CHADEMA inataka kwenda Ikulu kufanya nini?

Wataalika wanajeshi wa china waje na meli za kijeshi kuchukua meno ya tembo,kupandisha mshahara 5% na umeme80% kuongeza nauli za mabasi, kuuza sembe nk
 
Penye nia pana njia ipo siku tu watafika hata kama si viongozi wa sasa.
 
CCM inafanya nini Ikulu kwa sasa ?. Umesahau hili ombwe la uongozi hapa TZ? Je umesahau mambo mengi yanayofanywa na serikali ya CCM? Wewe ni kipofu na kiziwi usione na usiweze kusikia mateso wanayofanyiwa watanzania na vilio kutoka kwa watanzania juu ya mateso wanayoyapata kwenye maisha yao badala ya maisha bora.
Siamini kama watanzania wamesahau juu ya wizi wa EPA, Richmond, Meremeta, utoroshwaji wa Twiga ulofanwa na serikali ya CCM na mpaka leo hakuna hatua zilizochukuliwa. Watanzania mmesahau kweli juu ya kujivua gamba ndani ya Chama kitukufu cha CCM-watu wakasubiri ili kama wako serious basi hakuna atakayebaki CCM baadae wamenyamaza kimya. Ni kweli CCM ni zimwi lakini nachelea kama watanzania watakubali kuendelea kuliwa tu.
Niambie ufisadi ndani ya CDM unaozidi ufisadi unaofanywa na CCM na serikali yake, niambie matumizi mabaya ya fedha za umma unaofanywa na CDM unaozidi matumizi mabaya ya fedha yanayofanywa na CCM na serikali yake. Niambie ushauri ambao CCM inaukubali kutoka kwa wananchi (katiba, serikali3) ukilinganisha na CDM, Niambie chama kilichochafuka katika rushwa katika chaguzi zake kuzidi CCM. CDM itaingia Ikulu na inayo ajenda na wananchi wanaunga mkono ajenda za CDM kuliko CCM ambayo ni dhahiri is dying.
Uliyoandika hapo ni sawa hoja za m/kiti mmoja anaeng'ang'ania madaraka alipobanwa kuhusu tuhuma za yeye kuchukua fedha na kushirikiana na mafisadi akaamua kusema haijalishi pesa anakupa nani Bali unaitumiaje!unamuunga mkono?
 
we ndio mdandiaji hujaangalia wal kusikiliza sera za chama chochote ndio maana unasema chadema wanaenda kufanya nn ikulu..sasa CCM iko inafanya nn ikulu zaid ya kusafirisha unga matumboni na kuendelea kupandisha bei ya kila agusacho mwananchi lakin uliza mshahara wako utapanda lini??
hayo ya unafiki CCM ndio wanaongoza wanajidai wanasimamia sheria uliza walompga na kumtesa dr. ulimboka walikamatwa na alomwekea sumu mwakyembe ni nan na kwann kesi haijafatiliwa??
kutoshaurika CCM ndo kinara hakuna nchi inayotoa rasilimali zake kwa kupata asilimia 10 na znazobak ukampa mwekezaj ushaur huo mmeufanyia kazi??
na kuhusu maslahi tusingekuwa tunahangaika kuhojiana kuhusu mali wanazomilik viongozi au utoroshwaj wa pesa uswisi kama CCM wangekuwa wanasimamia sera zao.
HATUICHAGUI CHADEMA KWA UZURI WA SERA BALI KWA KUSIMAMIA VIZURI SERA ZAKE NA KATIBA KWA UJUMLA
Katiba ipi mkuu,ni hiyo inayogaragazwa na kina mbowe na slaa!kama hata katiba yenu hamuwezi kuifuata Vipi katiba ya nchi?
 
The stupidity network starts like this....you have no right to speak over the party which is not belong to you! Try to publicize your magamba party may be the public will understand you. Try to raise the relevant topics which may put the nation to the next level....finally asses your propaganda with the needs of the Tanzania people. Thats is my few concrete comments to you.
Ungeandika Kiswahili ungeeleweka pia!nakurekebisha hapo "you have no right to speak over the party that does not belong to...."mwisho wa kurekebisha! Pengine ni "....those are my few concrete comments...." Natumaini itasaidia kidogo!
 
TAFAKARI: Kama hapa ndio Makao makuu ya Chama, Je mikoani pakoje? CHADEMA si mnapata ruzuku kwa miaka 10 na kwasasa!!? Kama mmeshindwa kujenga makao makuu yenye hadhi. Je, mtaweza kuijenga Nchi?

NB:
Sijui hali ya Ofisi za CHADEMA Mikoani zikoje tu.

Hawana lolote hao zaidi ya ufisadi,chadema sio chama cha kukabidhiwa nchi kwa ni dhahiri kuwa Mbowe, Slaa, na vile Vibabu vya Kaskazini lengo lao ni kuendeleza Saccos yao pale watakapo chukua nchi. R.I.P Chacha Wangwe..
 
kiukweli CCM imechoka sana ikitakiwa iwe imeondolewa hata miaka kumi iliyopita tatizi lililopo ni kwamba hakuna chama ambacho kina unafuu vyama vyote ni matawi ya CCM
 
kiukweli CCM imechoka sana ikitakiwa iwe imeondolewa hata miaka kumi iliyopita tatizi lililopo ni kwamba hakuna chama ambacho kina unafuu vyama vyote ni matawi ya CCM
Chama ambacho kati ya nafasi chache za ubunge wa viti maalum m/kiti katua hawala,katibu mkuu wake zake wote wawil,mwansheria kateua mdogo wake hakiwezi Kuwa chama mbadala!walitakiwa waonyeshe mfano hata kwa kidogo walichopata!
 
umesahau NdesaPesa yeye yupo mtoto na mkwe wake
 
Najua maana ya ilani,na mie sio division 5,na natumia kichwa changu kufikiri!mikutano niliyohudhuria ya CDM ilikuwa ni kushambulia tu na sio kueneza sera!ruhusu kichwa Chaka nacho kifikiri na sio kuongozwa kwa Hisia za ukada!

Sasa wewe kenge si utulie tu uone mambo ya wakuwa. Maana tunahesabu miezi kadhaa historia itatokea Tanzani. Na kwanini CCM mnaweweseka sana juu ya CDM? Bila shaka mbinu zenu zote zimefunulia za kuua watu kwenye mikutano ya CDM ili CDM ionekane inavurugu, Kuteka watu na Kusingizia CDM, Kubwa zaidi Zitto mlimtuma kusambalatisha CHADEMA ndiyo hiyo tena yamemtokea puani. Yaani moto mnao siyo masihara katika hili.
 
Ingekuwa bungeni ungeambiwa siyo swali kaa chini!lakini swali lako linajibiwa kwa swali je,hayo maccm yanayo ng'ng'ania ikulu yanaogopa nini kutoka?
 
Wanataka kwenda kualalisha gongo na ushoga, namnukulu babu Slaa alidai hivyo katika mkutano wa Chama Kigoma.
 
Ni malengo ya kila chama cha siasa kutaka kushika dola. Pamoja na Lengo Hilo kuu vyama pia huwa na sera mbalimbali ambazo hasa ndio huwa dira ya malengo makuu ya kushika dola!

Hii huonyesha mipango ya Muda mfupi na mrefu ya kuleta maendeleo kwa wananchi! Mipango hii ndio hasa hutakiwa kutangazwa sana kwa umma ili ujue ni kwa nini Chama hiki kinaitaka dola!

Nachelea kusema Kuwa CDM wamekosa Hoja zenye mashiko kwa upande huu muhimu, wamekuwa ni wazuri sana kwa Hoja za kudandia na siasa za kushambulia bila kutuambia wao watafanya miujiza gani kwani mambo Mengi wanayoikosoa ccm wao pamoja na uchanga wao wanayafanya kwa Kasi Kubwa.

Mambo hayo ni pamoja na ubinafsi, ufisadi, matumizi mabaya ya maharaja, upendeleo, matumizi mabaya ya fedha za umma, kutoshaurika na mengine Mengi tu.

Sasa badala ya Kujibu kwa matusi na kejeli naomba CDM mtuambie mnataka kwenda ikulu kufanya nn? Mtakuwaje tofauti na mlivyo Sasa? Ni kwann watz wasiseme heri "zimwi likujualo halikulli likakwisha"?
Wewe umekaa kimajungu,ukabila,udini hauna lolote.!
 
kwann nguo zako zikichakaa unatupa na kuchoma moto na kisha kununua mpya?
 
TAFAKARI: Kama hapa ndio Makao makuu ya Chama, Je mikoani pakoje? CHADEMA si mnapata ruzuku kwa miaka 10 na kwasasa!!? Kama mmeshindwa kujenga makao makuu yenye hadhi. Je, mtaweza kuijenga Nchi?

NB:
Sijui hali ya Ofisi za CHADEMA Mikoani zikoje tu.

Usiongelee mikoani hiyo hapo hapo makao mkuu hawana hata jengo la chumba kimoja wanadandiadandia itakua huko mikoani
 
Kuwatumikia wananchi manake mmeshindwa nyie kwani hamjui malengo ya chama cha siasa hata hao cck na chausa hata tlp nibkuchukua dola mbona mnaogopa chadema kwenda ikulu kwani hii sio ikulu ya mbinguni ni ya watu bila sisi yaani mimi na wewe hakuna ikulu mbona ccm mnaogopa sana chadema na ole narudia ole wenu chadema wachukue hii nchi mtatafutana manake mlivyo tuibia mtarudisha vyote hivi amuoni aibu wazungu wametutawalahawajachukua hata kenge nyie mnatawala tembo wote kwisha hadi twiga mnaiba halafu muachwe ngojeni dawa yenu..

je unafuatilia kwa karibu matendo yanayoendelea ndani ya chadema au mapenzi na kile chama ndo yanakufanya ulopoke, je umefuatilia mapato na matumizi yao jinsi yanavyokwenda, kweli ccm ni wezi lkn chadema ndo hawafai kabisa, we angalia hata wanavyoongea hao wabunge wao ni jazba na chuki bt hakuna point za mashiko wanazosemaka zaid ya kutiana ubaya tu na fitna
 
Back
Top Bottom