Hata kama si mshabiki wa Chadema sisi tulio nje tunaona mabadiliko makubwa ya nchi yetu. Nchi yetu inabadilika kwa uzuri na hata chama tawala cha CCM kinabadilika!!. Hili ni swala muhimu sana kwamba kwa mara ya kwanza kwenye historia Chama tawala kinaogopa watu!. Kwa mara ya kwanza kihistoria Chama cha CCM kinajikosoa chenyewe hadharani bila kujifungia kwenye chumba. Kwa mara ya kwanza naona kuna kaheshima kidogo kwa wananchi kutoka Chama tawala. Hata kama Chadema isiposhinda lakini ikaendelea hivi ni nzuri kwa nchi kwani hata Chama Tawala kubadilika ni vizuri kwa nchi. Ninawapa pongezi Chadema kwa kubadilisha nchi yetu kwa uzuri. CCM itasema kwamba wanabadilika wenyewe lakini si kweli ni kwasababu ya uoga wa kukosa madaraka na kuamshwa kisiasa hili ni jambo zuri sana kwa nchi. Sasa hivi hakuna siri kwenye chochote serikalini tena na sasa tunaona kama maovu ambayo tulikuwa hatuyajui na ndiyo maana tunaona ufisadi lakini ufisadi umefanyika siku nyingi sana. Vilevile Chadema imesaidia kuwaamsha watanzania wafanyakazi wa serikali ambao hawaogopi kuvujisha data kwa vyombo vya habari kwa manufaa ya nchi. Kuna wengi wa kushukuru lakini Chadema ni wa kwanza na vyombo vya habari ni vya pili.