CHADEMA impigie magoti Dr. Slaa!

Source, source please, vinginevyo acheni kutafuta kick kwa kaanzisha thread zisizo balanced.... Kumbuka ya yule kijana wa Arusha?
 
katika watu wanaonishangaza ni wewe unayejiita mzee wa Lumumba. Hivi huku kujipendekeza kutakuisha lini? kipi ambacho unataka kuwaambia watu ili wa kuamini na kukusikiliza? Bora Kubaki kimya kuepusha ujinga kuliko kuonyesha unajua harafu hujui
Kwani kuna ubaya mtu kuishi mtaa wa Lumumba?mimi najua huyu mzee anaishi mtaa wa Lumumba,mzee Tupa tupa nipo sahihi?
 
Dr Slaa amestaafu siasa za vyama ....sasa atakuwa anatoa maoni kama mzalendo huru ...
 
katika watu wanaonishangaza ni wewe unayejiita mzee wa Lumumba. Hivi huku kujipendekeza kutakuisha lini? kipi ambacho unataka kuwaambia watu ili wa kuamini na kukusikiliza? Bora Kubaki kimya kuepusha ujinga kuliko kuonyesha unajua harafu hujui
Mbona sioni kujipendekeza kokote katika bandiko la Kada Mtiifu kindaki ndaki wa CCM,
Alwatan VUTA-NKUVUTE
Au Yeye kuwa Mzee wa Lumumba ni kujipendekeza ??,kawalaumu waliompa huo wadhifa pale Lumumba

Alwatan VUTA-NKUVUTE ni kada wa CCM mwenye kujielewa
 
Ila siyo vibaya kwa sababu Dk. ni mtanzania angekuwa mkenya ningeshangaa.
 
Kwani nyie bado mnamtaka? Si mlimtosa na kumkaribisha fisadi! Mwacheni aishi anavyotaka, yuko huru.
 
Yani wewe unataka mpiga dili awe raisi wa tz then pm awe mzalendo Magu?
 
Naona waziri mkuu kama kapwaya, anaendelea kufunikwa na rais
 
Namshukuru mwenyezi MUNGU muumba mbingu na nchi kwa kunipa afya na uhai na kuniwezesha kuandika haya amabayo Napata kuyaandika sasa, Sifa na utukufu vimwendee yeye mweza yote.

Salamu nyingi zikufikie Mwenyekiti mpendwa wa Chama cha demokrasia na maendeleo, umekuwa kiongozi mahiri kwa kuongoza chama kilichojaa vijana wasomi na wenye kutaka kujua na kujifunza uongozi, hata wakati mwingine walipotaka kwenda kinyume na matakwa yako , ulilitumia rungu lako vizuri kwa kuwapotezea mbali, hata wengine wakafia mbali, namkumbuka marehemu Chacha Wangwe na kiongozi wa ACT wazalendo Mhe Zuberi Zitto Kabwe, ni watu ambao walionja joto yako MHE MBOWE bila kumsahau mwanafalsafa mahiri DR, SLAA,huyu ulimuumiza kisaikologia na kifikra sana, kwani alilolisimamia maishani mwake we ulimgeuka na kulikumbatia lile alihohubiri kwa Watanzania kuwa ndio linalotafuna nchi yetu, yaaani ufisadi, Mhe Mbowe wewe ukawa rafiki mkubwa wa ufisadi ulimkosea sana mwanafalsafa huyu mahiri, na ndio maana kwa misingi ya kifalsafa hakuona kama ni vyema kuendelea na safari hiyo.

Kwa msingi huo DR Slaa anayo haki ya kuombwa msamaha kwani, Mhe Mbowe ulimkosea sana hata kama ni ile ya kinafiki ambayo uliifanya kwa Zitto Zuberi Kabwe ni sawa tu , lakini uoneshe utu na uungwana kwani dhambi ya kumkosea DR inakitafuna chama kwa sasa,kwanini naema inakitafuna chama, mtazame Mashinji hana hoja , anaongea kwa kulalamika, hotuba yake ilijaa malalamishi, sio kujenga hoja, chama kisimame vip, au wajipange vip, Badala yake amewaambukiza na vijana kulalamika, Nadhani ukikaaa na Mashinji faragaha ukimuuliza nini agenda za Chadema kwa miaka hii mitano, atakuwa hana , umempa mtu ukatibu ambae hajui katibu ni nani, na wajibu wa katibu ni nini,hilo ni kosa la pili ambalo umemkosea DR SLAA, mtafute umuombe radhi walau hata awape ushauri mnatakiwa kufanya nini, la sivyo Chadema is dying a natural death.
Asante sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…