CHADEMA imelinda heshima ya Sosopi

Aug 17, 2016
69
125
Nchi nzima ni zaidi ya majimbo 235 ambayo Sosopi anatakiwa kuyasimamia.

Msigwa kanda ya Nyasa ana simamia majimbo 33
kwa msingi huu Sosopi kwa cheo chake cha makamu mwenyekiti BAVICHA Taifa.

Ni mkubwa zaidi kiutendaji na kimamlaka kiliko msigwa. Msigwa ambae ni Mwenyekiti mpya kanda ya Nyasa ana simamia majimbo 33 katika eneo lake la kimamlaka.

Hivyo Msigwa ni mdogo sana kimamlaka.
Sosopi akiwa na ziara kanda ya Nyasa, Msigwa lazima awepo na kuandaa ziara ya makamu Mwenyekiti BAVICHA taifa.

Sosopi ni kiongozi wa kitaifa na Msigwa ni kiongozi wa kanda. Sasa kuenguliwa kwa Sosopi katika kugombea nafasi ya kanda ni katika kumpa heshma kubwa sana.

Pia chama kimetambua majukumu makubwa na heshma aliyo nayo Sosopi. Sosopi kimajukumu anatakiwa aishi DSM kuwa karibu na ofisi kuu za chama je kanda itakuwa ofisi yaendeshwaje?

Msigwa yuko Iringa na anaishi Iringa hivyo atakuwa mtu sahihi kuwa Mwenyekiti wa kanda kwakua anaishi kanda ya Nyasa muda wake mwingi.

Chama kimefanya busara za kiutendaji kumuengua Sosopi abakie na majukumu yake ya sasa ya BAVICHA.
 
Gamba la Nyoka

JF-Expert Member
May 1, 2007
6,919
2,000
Chadema wanajidanganya halafu wanaanza kuamini uwongo wao kuwa ni kweli.

Mmezingua Demokrasia ndani ya chama halafu mnaanza kujidanganya eti ni sahihi!

Wacha JPM awanyime uhuru wa kufanya siasa, maana hamdiserve kutendewa kidemokrasia wakati chama mnakiendesha kihuni na kidikteta!
 
Endeleaaa

JF-Expert Member
Oct 5, 2007
1,390
2,000
Huwezi kumnyima mtu haki ya uongozi tu kwa vile katokea upande flani wa nchi na vilevile huwezi kumpa mtu nafasi tu kwa vile katokea upande flani wa nchi.
 
SaidSabke

JF-Expert Member
Sep 28, 2006
2,072
1,500
Nchi nzima ni zaidi ya majimbo 235 ambayo Sosopi anatakiwa kuyasimamia.

Msigwa kanda ya Nyasa ana simamia majimbo 33
kwa msingi huu Sosopi kwa cheo chake cha makamu mwenyekiti BAVICHA Taifa.

Ni mkubwa zaidi kiutendaji na kimamlaka kiliko msigwa. Msigwa ambae ni Mwenyekiti mpya kanda ya Nyasa ana simamia majimbo 33 katika eneo lake la kimamlaka.

Hivyo Msigwa ni mdogo sana kimamlaka.
Sosopi akiwa na ziara kanda ya Nyasa, Msigwa lazima awepo na kuandaa ziara ya makamu Mwenyekiti BAVICHA taifa.

Sosopi ni kiongozi wa kitaifa na Msigwa ni kiongozi wa kanda. Sasa kuenguliwa kwa Sosopi katika kugombea nafasi ya kanda ni katika kumpa heshma kubwa sana.

Pia chama kimetambua majukumu makubwa na heshma aliyo nayo Sosopi. Sosopi kimajukumu anatakiwa aishi DSM kuwa karibu na ofisi kuu za chama je kanda itakuwa ofisi yaendeshwaje?

Msigwa yuko Iringa na anaishi Iringa hivyo atakuwa mtu sahihi kuwa Mwenyekiti wa kanda kwakua anaishi kanda ya Nyasa muda wake mwingi.

Chama kimefanya busara za kiutendaji kumuengua Sosopi abakie na majukumu yake ya sasa ya BAVICHA.
Huo ni ulaghai mkubwa siri kubwa iko ndani kwa kuenguliwa sosopi na mbiwe
 
sonaderm

JF-Expert Member
Nov 9, 2015
617
1,000
Nauliza hivi: Makamu mwenyekiti BAVICHA na Mwenyekiti Msigwa ambaye pia ni mbunge nani anapata mtonyo zaidi?
 
Karne

JF-Expert Member
Jun 13, 2016
4,467
2,000
..Ole Sosopi angechaguliwa mashambulizi kwamba cdm inapendelea watu wa "kaskazini" yangepamba moto.

..sikubaliani na siasa za kikabila , lakini ni ukweli usiopingika kwa siasa hizo zipo hapa Tz, na ni mtaji mkubwa kwa CCM.

Cc Gamba la Nyoka
Kwa hiyo CDM inavunja katiba yake ili kukwepa mashambulizi ya CCM?

Na unaona ni sawa tu na kuita busara za mwenyekiti?
 
expedition

JF-Expert Member
Jul 16, 2016
690
1,000
Ndani ya Kanda Msingwa ni kiongozi wa viongozi wote iwe BAVICHA ama BAWACHA na wanachama wote but Sosopi ni kiongozi wa BAVICHA pekee na hana maaumuzi kwa BAWACHA na wanachama wasiokuwa ndani ya BAVICHA.
Ukweli ni kwamba SOSOPI kahujumiwa wazi wazi na amekomeshwa huyo ndiyo Mbowe mmiliki wa kurithi wa CHADEMA.
 
kahupwe

JF-Expert Member
Sep 9, 2016
290
250
Mnatumia nguvu kubwa mno kutaka kuhalalisha upuuzi.

Nini maana ya kuwa na katiba sasa?

Tupeni jalalani katiba chama kiendeshwe kwa busara ya Mwenyekiti.
kama ambavyo mmepuuza katiba ya Jamhuri ya Tanzania? Maana sasa amri moja tu.
 
stigajemwa

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
449
500
Pamoja na maelezo mazuei aliyotoa mnyika napamoja na maelezo mazudi ya mtoa mada lakini lazima mkubali demikrasia imebakwa ndani ya chama kitu kinachowakosesha credibility ya kulaumu wizi na udanganyifu wa kura unaofanywa na ccm ktk kila uchaguzi ngazi ya mtaa hadi taifa.pia mmetuonesha kuwa kamwe demokrasia haiwezi kuchukua mkondo wake ktk nchi za kiafrika bali maslahi binafsi ya mtu,kikundi au chama ndio muhimu
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom