CHADEMA imelinda heshima ya Sosopi

..YES.

..kama hali halisi inalazimisha hivyo ili kukiwezesha chama kuongeza ushawishi ktk kanda ya Nyasa.
Hali halisi ipi? Acheni unafki wenu....sisi ni Chadema damu tena ni viongozi lkn huu unafki wa viongozi wa juu wa chama hiki itakifikisha chama hiki kubaya...
 
Ndani ya Kanda Msingwa ni kiongozi wa viongozi wote iwe BAVICHA ama BAWACHA na wanachama wote but Sosopi ni kiongozi wa BAVICHA pekee na hana maaumuzi kwa BAWACHA na wanachama wasiokuwa ndani ya BAVICHA.
Ukweli ni kwamba SOSOPI kahujumiwa wazi wazi na amekomeshwa huyo ndiyo Mbowe mmiliki wa kurithi wa CHADEMA.
Sahihi kabisa chief
 
Kwani Sosopi anatoka Kanda ya kaskazini? Ninyi ndo walewale

..nafahamu kwamba Ole Sosopi amezaliwa na kukulia Iringa.

..ndani ya chama anaweza asiwe na matatizo yoyote yale.

..tatizo liko nje ya chama. Je jamii inayomzunguka inamchukuliaje? Je Ole Sosopi na cdm wataweza kuhimili kampeni chafu za kikabila dhidi yake?

..Ole Sosopi angekuwa anagombea eneo kama Dsm ambako wakazi wake ni more diverse ningekuwa na mtizamo mwingine.
 
Acheni sifa za fanganya toto amekatwa kimjini mjini yameisha. Msigwa hamuandalii kiongozi wa Bavicha akiwa ziara wana babicha ambao wako chini kiuongozi kanda hiyo ndio wataandaa.
 
..nafahamu kwamba Ole Sosopi amezaliwa na kukulia Iringa.

..ndani ya chama anaweza asiwe na matatizo yoyote yale.

..tatizo liko nje ya chama. Je jamii inayomzunguka inamchuliaje? Je Ole Sosopi na cdm wataweza kuhimili kampeni chafu za kikabila dhidi yake?

..Ole Sosopi angekuwa anagombea eneo kama Dsm ambako wakazi wake ni more diverse ningekuwa na mtizamo mwingine.
Mkuu emb yape majawabu Haya maswali maana unaonekana ni team maamuzi on Sosopi's matter;

1. Nini maana ya demokrasia kwa muktadha wa CDM?

2. Kwanini hamkumuondoa sosopi mapema wkati wa mchakato wa awali kabisa/wakati wa kampeni au kabla badala yake mumemuacha mpk dakika Za mwisho mkamuondoa bila kumpa nafasi na Haki yake ya kuchaguliwa?

3. Kwanini mnahofia Mambo ya ukabila na ukanda ikiwa mna Uhakika hayo hayamo ndani ya Chadema?

4. Utakubaliana na Mimi kuwa hayo maamuzi ya Mbowe yamekua ni desturi kufanya maamuzi binafsi hata wakati wa kumpata Dr. Mashinji Katibu Mkuu badala ya kupiga Kura kwa wote walioomba?

5. Mnapata wapi mandate ya kudai Haki na demokrasia hapa nchini wakati ndani mnabaka demokrasia na Haki ya wengine kuchaguliwa?

6. Mchakato wa kupata viongozi ni kwa mujibu wa Katiba au ni kwa matakwa na mahaba ya Mwenyekiti?

7. CDM ni Mali ya nani, ya Mbowe au ya wanachama?
 
Kwani mpaka anachukua fomu ya kugombea hawakulijua hilo kuwa anamajukumu mengne? Je msigwa yeye ana nafas ngapi ndani ya chama? Na kama ana nafasi zaidi ya moja inamaanisha chama hakina watu wengine wenye sifa za uongozi?
 
Nali,

..maswali yako mengi ni magumu na siwezi kuyajibu.

..tena inaelekea tayari una majibu yako mfukoni kwa hiyo haitakuwa na maana mimi kuyajibu maswali hayo.

..uchaguzi umekwisha na mwenyekiti wa kanda ya nyasa ni Mh.Msigwa.

..sasa ni wakati wa kumuunga mkono Mh.Msigwa ili kukijenga chama.

..Ole Sosopi ni makamu mwenyekiti wa bavicha. Bado anayo nafasi ya kutoa mchango wake ktk chama.
 
Interpretation ( nali maswali yako magumu na sina jibu).
 
Chadema wanajidanganya halafu wanaanza kuamini uwongo wao kuwa ni kweli.

Mmezingua Demokrasia ndani ya chama halafu mnaanza kujidanganya eti ni sahihi!

Wacha JPM awanyime uhuru wa kufanya siasa, maana hamdiserve kutendewa kidemokrasia wakati chama mnakiendesha kihuni na kidikteta!
hoja bin hoja mkuu naona wee huna hija
 
Interpretation ( nali maswali yako magumu na sina jibu).

..huyo ndugu yangu tayari ana majibu ya maswali yake.

..ni mtu mwenye msimamo mkali na asiyependa ku compromise.

..kutokana na msimamo wake anaamini kuwa katiba za vyama vya siasa ni sawa na katiba ya nchi.
 
Nchi nzima ni zaidi ya majimbo 235 ambayo Sosopi anatakiwa kuyasimamia.

Msigwa kanda ya Nyasa ana simamia majimbo 33
kwa msingi huu Sosopi kwa cheo chake cha makamu mwenyekiti BAVICHA Taifa.

Ni mkubwa zaidi kiutendaji na kimamlaka kiliko msigwa. Msigwa ambae ni Mwenyekiti mpya kanda ya Nyasa ana simamia majimbo 33 katika eneo lake la kimamlaka.

Hivyo Msigwa ni mdogo sana kimamlaka.
Sosopi akiwa na ziara kanda ya Nyasa, Msigwa lazima awepo na kuandaa ziara ya makamu Mwenyekiti BAVICHA taifa.

Sosopi ni kiongozi wa kitaifa na Msigwa ni kiongozi wa kanda. Sasa kuenguliwa kwa Sosopi katika kugombea nafasi ya kanda ni katika kumpa heshma kubwa sana.

Pia chama kimetambua majukumu makubwa na heshma aliyo nayo Sosopi. Sosopi kimajukumu anatakiwa aishi DSM kuwa karibu na ofisi kuu za chama je kanda itakuwa ofisi yaendeshwaje?

Msigwa yuko Iringa na anaishi Iringa hivyo atakuwa mtu sahihi kuwa Mwenyekiti wa kanda kwakua anaishi kanda ya Nyasa muda wake mwingi.

Chama kimefanya busara za kiutendaji kumuengua Sosopi abakie na majukumu yake ya sasa ya BAVICHA.
Tatizo hapo lilikuwa ni kuacha Democracy ifanye kazi, vinginevyo mlitakiwa kumuomba hasigombee, na sio kumkata
 
Huwezi kumnyima mtu haki ya uongozi tu kwa vile katokea upande flani wa nchi na vilevile huwezi kumpa mtu nafasi tu kwa vile katokea upande flani wa nchi.
Kaka sosoppi ni hazina ya taifa hatutakiwi kulimiti eneo lake la utendaji
 
Nali,

..maswali yako mengi ni magumu na siwezi kuyajibu.

..tena inaelekea tayari una majibu yako mfukoni kwa hiyo haitakuwa na maana mimi kuyajibu maswali hayo.

..uchaguzi umekwisha na mwenyekiti wa kanda ya nyasa ni Mh.Msigwa.

..sasa ni wakati wa kumuunga mkono Mh.Msigwa ili kukijenga chama.

..Ole Sosopi ni makamu mwenyekiti wa bavicha. Bado anayo nafasi ya kutoa mchango wake ktk chama.
Kumbe! Kajipange tena....
 
Hayo mkazungumzie huko kwenu maamuzi yaliyofanywa yamezingatia mambo Mengi sana kwa akili yako ndogo huwezi kujua
Uko sahihi watanzania wengi tunaakili ndogo Sana kujua mantiki ya maamuzi haya. Kwa kuwa tunaakili ndogo na hatujui mengi, ndio maana tunasema mbadala wa CCM Bado.
 
Back
Top Bottom