CHADEMA ime-savaivu, sasa nini?

KalamuTena

JF-Expert Member
Jul 7, 2018
13,189
17,157
Hakuna shaka yeyote, na sidhani kwamba kuna mtu anayeweza kuhoji uwepo wa CHADEMA kama chama cha kisiasa kilicho na ushindani mkubwa hapa nchini licha ya misukosuko mingi iliyoelekezwa kwao ili kuwamaliza kabisa katika miaka mitano na zaidi sasa iliyopita.

Ni sawa kabisa kusema kwamba CHADEMA wamepitia kwenye tanuru la moto mkali, na wamepikika sawasawa kuweza kuendelea na pilkapilka zao za kisiasa na kutafuta njia ya kuliongoza taifa hili.

Sioni mbele yao, kupata hujuma tena, kama walizozipata miaka hii ya karibuni chini ya utawala wa Marehemu Magufuli. Tanzania itakuwa na bahati mbaya sana, kama patatokea hivi karibuni misukosuko iliyolitingisha taifa kama ilivyotokea wakati wa serikali ya Magufuli.

Watu wanaweza kuhoji kwamba kuendelea kuwepo kwa CCM madarakani hiyo ndiyo hatari kubwa kwa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani.

Mimi hilo silioni hivyo kwa sasa, na hata katika CCM ya enzi za Kikwete. Hatari iliongezeka zaidi alipoingia madarakani Magufuli na kutangaza waziwazi kutopenda uwepo wa vyama vya upinzani.

CCM wenyewe kama chama, hila zao zilikuwa ni za kawaida, mradi tu wanapata ushindi, hawakuwa na lengo maalum la kuua upinzani.

CHADEMA wafanye nini (samahani kwa kuwasema CHADEMA, badala ya vyama vya upinzani, kwa sababu vingine ndio hivyo tena vimetekwa).

Huu ni wakati wa CHADEMA kuwa wazi kabisa na sera zao. Wananchi waelewe chama kinasimamia nini.

Kati ya sifa chache, lakini muhimu alizojijengea Magufuli (sio CCM) ni kuonekana kuwa mtetezi wa mali na utajiri wa nchi hii na maendeleo ya wananchi wake.

Amejitambulisha bila shaka yoyote, kwamba yeye alikuwa ni mtetezi mkubwa wa maslahi ya Tanzania na wananchi wake. Amejenga hata ukuta, kulinda Tanzanite yetu iliyokuwa inatoroshwa kwenda nchi za nje na kuwanufaisha hao zaidi ya sisi tulivyokuwa tunanufaika kwayo.

Swala la madini aliliwekea mkazo sana; hata kama ilionekana kama kulikuwa na makosa katika juhudi hizo, lakini wananchi walielewa madhumuni yake. Kuna mifano mingi kuhusu msimamo wake juu ya mali za Tanzania.

Hatujui kuhusu mikataba mbalimbali nchi yetu iliyoiingia na nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa, lakini bado inaelekea wananchi waliamini kwamba mikataba hiyo ilikuwa ni kwa maslahi yao.

Jambo ambalo inawezekana hakulifanya vizuri ni kuhusu mashirikiano yetu na nchi mbalimbali duniani kwa vile alikazia zaidi "ubeberu" na mambo mengine kama masimango yao.

Nimeyaandika haya, ili CHADEMA watambue kwamba kama sera zao hazieleweki kwa wananchi, kazi yao itaendelea kuwa ngumu zaidi kuwashawishi wananchi hao kuwapa madaraka. Ni lazima wajieleze waziwazi kwa wananchi, wao ni nini hasa wanakisimamia kama chama cha siasa, na nchi yetu itafaidika vipi na misimamo yao hiyo kama watapewa ridhaa ya kuongoza serikali.

Kwa hiyo, nadhani ni halali sasa kusema kwamba adui mkubwa aliye mbele ya CHADEMA ni CHADEMA yenyewe. CCM wataendelea na hadaa zao kwa wananchi, hadaa za "Hawa ni Wenzetu" kama ilivyowahi kuwa huko nyuma, na wananchi kama hawaoni mbadala wa kuwapa madaraka, watarudi huko huko kwenye chama kilichooza ndani kwa ndani.

Niseme hapa, sijui kama Samia atakuwa na nguvu za kukibadilisha hiki chama kiwe chama cha wananchi wenyewe kwelikweli. Sijui.
Hatujui
 
CCM itaendelea kutawala kwa muda mrefu Sana.
Hilo linawezekana kama vyama vingine vya siasa vitaruhusu iwe hivyo.

Kuruhusu kunatokana na sababu mbalimbali, kama vyama hivyo kutoweka bidii kuwaondoa CCM.

Wananchi hawawezi kukabidhi nchi kwa chama chochote kisichokuwa tayari kulinda maslahi mapana ya nchi yao.

Kumbuka, ni wananchi wenyewe ndio wenye mamlaka ya mwisho, sio mtu mmoja tena au kikundi cha watu wachache walio na mabunduki na mabomu ya kutoa machozi.

Tanzania hatutegemei kurudi tena kiongozi wa aina hiyo hivi karibuni.
 
Kazi kubwa iliyo mbele yao (CHADEMA), ni kuwaendea wananchi walipo,huko mitaani. Wasitegemee sana hizi siasa za majukwaani.
CCM imetumia udhaifu wao huo kwa vile wao CCM wako kila sehemu mitaani.

CHADEMA inabidi warekebishe muundo wao wa chama ili ngazi za mashina ziwe na sehemu muhimu zaidi ndani ya chama hicho.
 
Sidhani kama wanaweka mkazo kwenye kuhakikisha wana sera mbadala zinazoeleweka kwa wananchi
Wasipoliwekea mkazo stahiki hili, wataendelea kuwa chama cha upinzani miaka yote.

Ni kazi kubwa sana inayowakabili, lakini ni kazi inayowezekana kama wakiweka dhamira ya kweli katika kazi hiyo.

Inahitaji viongozi wenye 'commitment', sio wachumia tumbo wanaotegemea tunda liwadondokee kichwani.
 
Kalamu1
nimeshiliki kwa ukamilifu uchaguzi wa 2021

Nimeshiriki vyema mchakato mzima wa kampeni mwanzo mwisho itoshe kusema, wanachokosa CHADEMA ni jeshi la kulinda kura zao na vyombo vya kutangaza huo ushindi wao!

hiki chama kipo zaidi ya 80% maeneo ya nchi hii!

Sera zao mbona zinaeleweka vizuri tu!

elimu bure(jpm) akaikwapua 2015, serikali za majimbo ili kupunguza centralization ya uchumi na upendeleo katika maendeleo ya nchi, katiba mpya na ushirikishwaji wa wananchi katika maamuzi ya nchi kidemokrasia!

Cha kuwashauri CHADEMA ni kupunguza tu zile siasa za kihanarakati zisizo na tija yoyote.

Ule uporaji wa kura wa mwaka jana ndyo taswira ya uimara wa CHADEMA!
 
Ule uporaji wa kura wa mwaka jana ndyo taswira ya uimara wa CHADEMA!
Mwaka jana hapakuwepo na uchaguzi mkuu 'guwe_la_manga', huo ulikuwa ni uchafuzi.

Lakini swali ambalo bado ninajiuliza ni hili, labda nawe utasaidia kulijibu:
Hivi kweli CHADEMA waliingia kwenye uchaguzi huo wakitegemea kwamba utakuwa huru na wa haki? Zingatia hapa kilichofanyika na ule uchaguzi wa serikali za mitaa uliokuwa umetangulia!

Ni nini hasa kilichowaaminisha CHADEMA kwamba wangeweza kushiriki na kupata ushindi katika hali iliyokuwa bayana kabla ya kupiga kura!

Siwezi kamwe kukubishia juu ya utayari wa ushindi walioutegemea kutoka kwa wananchi kama ulivyoeleza kuwa hali uliyoishuhudia wewe mwenyewe. Sasa jiulize, wananchi wakawapigia kura CHADEMA, CCM wakazipora, na kukwa kimya kana kwamba hakuna kilichotokea! Huoni hitilafu katika hali hiyo?

Maoni yangu ni kwamba, hata kama CHADEMA walipewa kura nyingi na wananchi, wananchi hao hawakuwa na msisimuko wa kuiunga mkono CHADEMA. Hata kama waliwapa kura zao, hiyo ilikuwa ni kwa sababu hapakuwa na mwingine wa kumpa; zilipoporwa, wananchi hawakuwa na mori wa kukataa uharamia huo.

Kazi waliyokuwa waifanye CHADEMA kabla ya kura kupigwa, ni kuwaandaa wananchi wasikubali kunyang'anywa haki yao ya msingi, haki ya kuwachagua viongozi wanaowataka.

Mwisho, kutokana na niliyoandika hapo juu, sina hakika sana kwamba wananchi hata kama waliwapa kura zao nyingi CHADEMA, sababu ya kufanya hivyo ilikuwa ni kwa sababu walielewa na kuzikubali sera, kama zile ulizozitaja wewe.

Kunawezekana sana kama waliwapigia CHADEMA kura, sababu inaweza kuwa ni kwa sababu ya kuwakataa CCM, na hasa kutokana na aliyokuwa ameyafanya mwenyekiti wa chama hicho kama rais.

Sitapenda unielewe kwamba wananchi hawazipendi sera za CHADEMA, lakini ningependa kupata ushahidi unaojitegemea zaidi.
 
Kalamu1
miaka mitano ya Magufuli ilififisha confidence ya watu ya Nguvu ya Umma!
Zile kashkash za jpm ziliwatisha wengi!
Kumbuka mwamuko wa watu katika chaguzi za 2010 kwenda juu na ule wa 2015!

Wananchi kabla ya jpm waliandamana na kulinda kura zao,we pia ni shahidi wa hili!

Ila siyo muumini wa siasa za kashkash na maandamano!

Cha msingi Serikali iweke usawa katika siasa,ipeleke mswada bungeni wa mabadiliko ya katiba,ili jasho linalomwagika katika operesheni za kuiba kura lielekezwe pengine kwenye tija!
 
Chadema inatakiwa kuwa na viongoz shupavu ngazi za juu I'll wananchi wawaamin siyo makajanja, labda chakaufanya ni kuungangana kwa upinzan hapo wanaweza itikisa serikal aliyoiacha jiwe ,wao wenyewe chadema Bado Sana, Wanachama wa chadema wengi wako mjin na humu jf wakati Wanachama wa ccm wako vijijin na ndio wapiga kura.
 
Kuunganika kwa upinzani sasa ni ngumu sana, baada ya kutoaminiana kati ya vyama vya upinzani.

Ni vigumu, kwa mfano sasa CHADEMA kuungana na ACT-Wazalendo, au CUF ya Lipumba au NCCR ya Mbatia.

Kutatokea kitu gani kinachoweza kuvifanya hivvi vyama viungane, sio rahisi.

Uimara wa viongozi wa ngazi za juu ndani ya CHADEMA, nadhani sasa unajulikana. Wasingekuwa imara, hasa katika miaka mitano hii waliyopata kila aina ya dhoruba, leo hii CHADEMA isingekuwa tofauti sana na NCCR Mageuzi.

Ndiyo maana CHADEMA 'IMESAVAIVU', vinginevyo lengo la Mwenyekiti wa CCM lingekuwa limetimia.

Wewe unadhani watu kama akina Halima Mdee, Ester wawili kurubuniwa ilikuwa kazi rahisi? Ujue, hata akina Mbowe wameihimiri mikiki mikiki mingi, lakini wakabaki imara.
 
Umesema sawa kabisa. Tatizo, inaelekea CHADEMA wenyewe wanachoamini ni kwamba wanafeli kwa sababu tu ya kuibiwa kura na hujuma zingine zinazofanywa na CCM. Sidhani kama wanaweka mkazo kwenye kuhakikisha wana sera mbadala zinazoeleweka kwa wananchi.
Wewe siyo mtu MAKINI. Kama ungefuatilia aliyotenda Magufuli 2016-20 alikuwa anatembea kwenye Ilani ya CDM. Walichotofautiana CDM na Magufuli ni kukandamiza DEMOKRASIA, Utawala bora, kukanyaga Katiba, kukandamiza uhuru wa kujieleza na UDIKTETA. Lete kingine au funga mdomo
 
Wewe siyo mtu MAKINI. Kama ungefuatilia aliyotenda Magufuli 2016-20 alikuwa anatembea kwenye Ilani ya CDM. Walicjotofautiana CDM na Magufuli ni kukandamiza DEMOKRASIA, Utawala bora, kukanyaga Katiba, kukandamiza uhuru wa kujieleza na UDIKTETA. Lete kingine au funga mdomo
Mkuu 'Stuxnet'

Yatunze vyema sana maneno ya mistari hii miwili hii.

Mimi ningependa niyakumbuke mara kwa mara nitakapokuwa nawasuta CHADEMA kwa kushindwa kuyaeleza kwa wananchi, na badala yake mazuri wanayoyasimamia yanaporwa na mtu anayewakandamiza, na wala wananchi wasiwe na uelewa wa kitu gani kinatokea.

Mimi nauona huo kuwa udhaifu kwa upande wa CHADEMA (granted, iliwezekana hivyo kwa sababu walikandamizwa); lakini kama wataendelea na hali hiyo toka sasa kwenda mbele, basi lawama itakuwa ni yao.
 
Hakuna shaka yeyote, na sidhani kwamba kuna mtu anayeweza kuhoji uwepo wa CHADEMA kama chama cha kisiasa kilicho na ushindani mkubwa hapa nchini licha ya misukosuko mingi iliyoelekezwa kwao ili kuwamaliza kabisa katika miaka mitano na zaidi sasa iliyopita.

Ni sawa kabisa kusema kwamba CHADEMA wamepitia kwenye tanuru la moto mkali, na wamepikika sawasawa kuweza kuendelea na pilkapilka zao za kisiasa na kutafuta njia ya kuliongoza taifa hili.

Sioni mbele yao, kupata hujuma tena, kama walizozipata miaka hii ya karibuni chini ya utawala wa Marehemu Magufuli. Tanzania itakuwa na bahati mbaya sana, kama patatokea hivi karibuni misukosuko iliyolitingisha taifa kama ilivyotokea wakati wa serikali ya Magufuli.

Watu wanaweza kuhoji kwamba kuendelea kuwepo kwa CCM madarakani hiyo ndiyo hatari kubwa kwa CHADEMA na vyama vingine vya upinzani.

Mimi hilo silioni hivyo kwa sasa, na hata katika CCM ya enzi za Kikwete. Hatari iliongezeka zaidi alipoingia madarakani Magufuli na kutangaza waziwazi kutopenda uwepo wa vyama vya upinzani.

CCM wenyewe kama chama, hila zao zilikuwa ni za kawaida, mradi tu wanapata ushindi, hawakuwa na lengo maalum la kuua upinzani.

CHADEMA wafanye nini (samahani kwa kuwasema CHADEMA, badala ya vyama vya upinzani, kwa sababu vingine ndio hivyo tena vimetekwa).

Huu ni wakati wa CHADEMA kuwa wazi kabisa na sera zao. Wananchi waelewe chama kinasimamia nini.

Kati ya sifa chache, lakini muhimu alizojijengea Magufuli (sio CCM) ni kuonekana kuwa mtetezi wa mali na utajiri wa nchi hii na maendeleo ya wananchi wake.

Amejitambulisha bila shaka yoyote, kwamba yeye alikuwa ni mtetezi mkubwa wa maslahi ya Tanzania na wananchi wake. Amejenga hata ukuta, kulinda Tanzanite yetu iliyokuwa inatoroshwa kwenda nchi za nje na kuwanufaisha hao zaidi ya sisi tulivyokuwa tunanufaika kwayo.

Swala la madini aliliwekea mkazo sana; hata kama ilionekana kama kulikuwa na makosa katika juhudi hizo, lakini wananchi walielewa madhumuni yake. Kuna mifano mingi kuhusu msimamo wake juu ya mali za Tanzania.

Hatujui kuhusu mikataba mbalimbali nchi yetu iliyoiingia na nchi na mashirika mbalimbali ya kimataifa, lakini bado inaelekea wananchi waliamini kwamba mikataba hiyo ilikuwa ni kwa maslahi yao.

Jambo ambalo inawezekana hakulifanya vizuri ni kuhusu mashirikiano yetu na nchi mbalimbali duniani kwa vile alikazia zaidi "ubeberu" na mambo mengine kama masimango yao.

Nimeyaandika haya, ili CHADEMA watambue kwamba kama sera zao hazieleweki kwa wananchi, kazi yao itaendelea kuwa ngumu zaidi kuwashawishi wananchi hao kuwapa madaraka. Ni lazima wajieleze waziwazi kwa wananchi, wao ni nini hasa wanakisimamia kama chama cha siasa, na nchi yetu itafaidika vipi na misimamo yao hiyo kama watapewa ridhaa ya kuongoza serikali.

Kwa hiyo, nadhani ni halali sasa kusema kwamba adui mkubwa aliye mbele ya CHADEMA ni CHADEMA yenyewe. CCM wataendelea na hadaa zao kwa wananchi, hadaa za "Hawa ni Wenzetu" kama ilivyowahi kuwa huko nyuma, na wananchi kama hawaoni mbadala wa kuwapa madaraka, watarudi huko huko kwenye chama kilichooza ndani kwa ndani.

Niseme hapa, sijui kama Samia atakuwa na nguvu za kukibadilisha hiki chama kiwe chama cha wananchi wenyewe kwelikweli. Sijui.
Hatujui

Kimeozaje mkuu. Kujidanganya kwako ndo kosa kubwa sana. Unaongea as if CHadema imejaaa kila kitu safi na haki. Hapo ndo unaonekana mjinga. Kuwa mkweli hata kama inauma ndo dawa ya kweli. Kosa kubwa sana. MlifanyA kwa Dr slaa. Kama mbunge alifanya kazi kubwa jimboni kwake. Hivyo watu walimwamini. Sio maneno maneno ambayo ukiuliza kafanya Nini ohhhh anajua kutukana.
 
Back
Top Bottom