CHADEMA ikishinda vita ya propaganda itachukua nchi 2015

-Badala ya kujenga hoja unajiropokea tu.Unadhihirisha ulivyo narrow minded kwa kutaja majina ya watu.Huu ndio ufuasi kipofu(blind follower) tunaousema hapa.Grow up.I think i should ignore you hadi pale utakapojenga hoja ambazo ni credible

....Sijawahi kuwa mfuasi wa mtu yeyote, ila wewe endelea kuwa mfuasi wa kupigania "watu" badala ya "fikra" kwa nguvu zako zote kama unavyofanya sasa kama hapa ndipo unapoishia kufikiri au ndiyo option pekee ya kuendelea kuwepo kwenye siasa, hapa ndipo ilipo tofauti ya "wavulana" na "wanaume" katika siasa...

....Wenye fikra za kifuasi wapo wazi,na wanaonekana kwa maneno na matendo yao, wapo tayari ata kurusha ngumi ilmuradi wamtetee "mtu" badala ya "fikra", na upo katikati ya kundi hilo sasa, ukishakuwa ana "akili ndogo hizi" hauwezi kusimama kwa miguu yako, tegemea mbebaji tu...
 
....Umaarufu wa Chadema ukiyeyuka, wanasiasa wengi waliopo Chadema leo ndio utakuwa mwisho wa fani yao ya siasa kwa sababu hawajajipambanua kwa wananchi kama wanaweza kusimama wenyewe, ata akina Masumbuko Lamwai wanalijua hili...

...LAKINI ata ANC ikifa leo-Kijana Malema atabaki, ata Kibaki alipomgeukia ndani ya NARC-Raila Odinga alibaki, ata ODM ilipomgeukia-Ruto alibaki, na ata changamoto ya ICC ilipokuja-Uhuru Muigai alibaki, ata Chadema ikifa leo-Zitto atabaki, kwanini? hawategemei upepo wa "mtu" wala "matukio", wanaweza kusimama kwa miguu yao...

-Badala ya kujenga hoja unajiropokea tu.Unadhihirisha ulivyo narrow minded kwa kutaja majina ya watu.Huu ndio ufuasi kipofu(blind follower) tunaousema hapa.Badala ya kujenga taasisi unataka watu wajijenge.Grow up.I think i should ignore you hadi pale utakapojenga hoja ambazo ni credible
 
Nikiwa kama mwanachadema hai nimeanza kupata wasiwasi juu ya sisi CHADEMA kuingia Ikulu 2015.

Mimi ninafikiri mbali na jitihada kubwa za ukombozi na vuguvugu la mabadiliko MOVEMENT FOR CHANGE M4C ni lazima tutambue mbinu CHAFU na DHAIFU wanazotumia MAGAMBA kusambaratisha UMOJA WETU na jitihada zetu za kuingia IKULU 2015. Yani magamba wao usiku na mchana wanatafuta cha kufanya ili tu UMOJA UNAOASHIRIA UKOMBOZI 2015 UVUNJIKE.

Maandiko matakatifu yanasema ukimpiga mchungaji kondoo watatawanyika, hilo nalielewa na ninyi mnafahamu.

Baada ya magamba kuona jinsi shujaa wetu Dr Wilbroad Slaa alivyongara kuelekea 2015 wameanza kutafuta kasoro zake tena mbaya zaidi ili kutufanya sisi Chadema tutawanyike.. Nape anasema Dr slaa ana kadi ya CCM ili hali kadi aliyonayo ni ile ya TANU ya enzi za chama kimoja. Sasa nashangaa inakuwaje wana chadema mnashindwa kuelewa mbinu hizi chafu za MAGAMBA?

Vijana chadema mweanza mnasema eti ajiuzulu! Hivi ninyi bado hamtambua DIVIDE AND RULE POLICY wanayotumia huju gamba NAPE ili kufifisha nguvu ya UMMA? Mara masuala ya Kuzuia ndoa yake mahakamani ni mbinu zao pia. Ikumbuke hivi majuzi waziri wa ushirikiano wa Afrika mashariki mh 6 alisema dr Slaa ni tishio la CCM 2015.Wanachadema wenzangu nasema kweli tutapoteza resources nyingi katika harakati ila tusipofahamu mbinu za ADUI Tunayempiga hata tuchangishe mabilioni Kuichukua nchi itabaki kuwa ndoto milele.

Wasomi Vijana wenzangu huko mwanza mbinu za magamba chafu zinawafanya mkigawe CHAMA? na hao MAGAMBA wamekumbatia MAFISADI hawataki hata kuwashtaki mnadanganywa mnakaa kusema Slaa Ajiuzulu? Poleni sana kuingizwa mkenge na MAGAMBA baada ya kuona CHADEMA TUNANGARA KUELEKEA 2015.

Nawasilisha kwa Uchungu sana!
 
Makamanda yameingiwa na hofu kubwa yanatapatapa ovyo.
unacheki eh, mpaka yanatumia policcm wao kutuliza makamanda.(but hapo kwenye kijani piga magwanda kwani ndo rangi yao)
 
Mkuu, naona wewe una wasiwasi wa jambo lisilokuwepo, yaani unaogopa kivuli cha upuuzi.

*Hakuna mwanaCHADEMA anayeweza kutikisika kwa propaganda za kipuuzi kama hizi za Nape.

*Hao vijana wanaojiita wa BAVICHA mkoa wa Mwanza wanafahamika kwa malengo yao, wanajua wanachokifanya na ni sehemu ya Mkakati wa Nape katika sakata hili.
*
 
Umebakia muda mchache tu kabla ya CHADEMA kutangaza ushindi 2015.

Kwa sasa CCM imeamua kuanzisha vita ya kipropaganda kupitia mitandao ya kijamii na magazeti. Nina hakika hii ni silaha ya mwisho kwa CCM na pale tutakapoweza kuishinda basi njia ya CHADEMA kushika nchi 2015 itakuwa nyeupe.

CCM imeshakataliwa mjini na vijijni, pia imekataliwa na waislamu kwa wakristo,wazee kwa vijana, tunahitaji busara za hali ya juu kupambana na propaganda.

Tumeanza na mungu tutamaliza na mungu.
Aimeen...!
 
CDM haiwezi kutingishwa na maneno ya kwenye kanga.
Hizi propaganda zitapita na cdm itabaki kuwa imara daima na kutakeover 2015. RIP CCM
 
Makamanda yameingiwa na hofu kubwa yanatapatapa ovyo.

Hakuna aliyeingiwa na hofu ww gamba, ccm inajiandaa kuwa chama cha upinzani 2015 ndo maana wanaangaika na vipropaganda za kipuuzi zinazongozwa na nape kushambulia chama tawala 2015 CDM.
Mbinu ya divide and rule ilifanikiwa kipindi cha ukoloni tu, sasa hivi mtagonga mwamba jombaa,, mkileta vipandikizi venu tunavitimua kama kawa hatutaki mamluki pande hiziiii.
 
...Taratibu unaelekea kwenye "akili ndogo" kisiasa, geuka kabla haujazama, Siasa za Ufuasi hazidumu lakini siasa za fikra huru zitadumu ata pale wabebaji watakapogota, hii ndio tofauti ya vijana makini wanaoweza kusimama kwa miguu yao wenyewe na vijana hohehahe wanaosubiri tu kubebwa kwenye mbeleko...

Unamaanisha kupinga uasi ndani ya chama ni akili ndogo kisiasa ? Au Nape kuendelea kuwaponza vijana na kuwaharibia future yao ndiyo akili kubwa kisiasa ? Hebu fafanua , labda unaweza kuwa na points .
 
KIUKWELI DR Slaa ni Jembe.Yule mzee ananyota kali mno kwasasa, Mtanzania amchukiae anapoteza muda. mzee Anatisha mwacheni as alivo .tusiongee tu coz tunaipenda Ccm bana.
 
...Taratibu unaelekea kwenye "akili ndogo" kisiasa, geuka kabla haujazama, Siasa za Ufuasi hazidumu lakini siasa za fikra huru zitadumu ata pale wabebaji watakapogota, hii ndio tofauti ya vijana makini wanaoweza kusimama kwa miguu yao wenyewe na vijana hohehahe wanaosubiri tu kubebwa kwenye mbeleko...

HAKUNA CHA ufuasi mkuu zaid ya ukweli unaosimamiwa, nyie na siasa zenu za uasi hamtafika popote kunguru wakubwa
 
Huwa nasema kilasiku tatizo la magamba wanapigana kuisambaratisha CDM tatizo sio cdm tatizo ni wananchi wanataka mabadiliko duniani kama ilivyo kwenye nyanja nyingine kiuchumi,kisiasa,kijamii hata kitamaduni sasa Tanzania ni kipande cha ardhi ya dunia chenye watu Wanaoongozwa na chama cha magamba cha muda mrefu nusu karne sasa hivyo hakuna namna kinaweza kukwepa mabadiliko haya na mbadala wake ni CDM,wananchi wameona mwanga huko CDM sasa wanataka kulikimbia giza CCM kwenda kwenye mwanga CDM,hivyo CCM wanapingana na wenye nchi,vita hiyo hawatakaa washinde hata siku moja ni ndoto.
 
KIUKWELI DR Slaa ni Jembe.Yule mzee ananyota kali mno kwasasa, Mtanzania amchukiae anapoteza muda. mzee Anatisha mwacheni as alivo .tusiongee tu coz tunaipenda Ccm bana.
yafaa Dr slaa apewe heshima zake za kuratibu ukombozi wa pili wa mtanzania
 
naona ule mpango wa kuivuruga chadema kwa kutumia masalia umekwama!
 
Hakuna mpenda maendeleo ambae atakosa kuilaumu serikali ya ccm kwa kudumaza maendeleo hapa nchini kwetu. tumejaaliwa rasilimali nyingi za asili. madini, bahari, mbuga za wanyama na ardhi nzuri ni baadhi ya neema tulizo ruzukiwa na Mungu. kama serikali yetu ingesimamia ipasavyo na kwa uadilifu kuvuna au kutumia rasilimali zetu, watanzania tungekua na maisha mazuri sana!

wengi wetu tunataka mabadiliko. mabadiliko lazima yawe ya kisiasa. tumekua na mfumo wa vyama vingi kwa miaka 20 sasa.tuna vyama vingi vya kisiasa lkn vyama vya upinzani vinavyong'ara ni chdm, cuf na nccr. chdm kimeonesha kung'ara zaidi kuliko cuf na nccr.

kuna propaganda ambayo imeenezwa na ccm kwa kushirikiana na vyombo vya habari. ni propaganda ya kuwalisha watanzania imani potofu kuhusu cuf na chdm. imani hiyo ni kwamba vyama hivi vina mrengo wa udini, ukanda na ukabila.

vyombo vyetu vya habari haviendeshwi kiueledi! vimeshabikia propaganda hii, ama kwa makusudi au kwa ujinga, na kuifanya ijikite katika ubongo wa watanzania! imekua ni kawaida kwenye magazeti yetu kuwekwa picha za mbowe, slaa na viongozi wengine wa chdm wakiwa na viongozi wa dini upande wa wakristu. imezoeleka hivyo kuwaona wakiwa na mapadri au maaskofu. picha za viongozi wa chdm wakiwa na viongozi wa dini za kiislamu huwa hazipewi front page appearence. naamini zikiwekwa picha kama hizo watu watashangaa sana! kwa nini washangae? ni kwa sababu hawajazoeshwa kuwaona viongozi wa chdm wakiwa na viongozi wa dini ya kiislamu. hali hii imewafanya waislamu waamini kuwa lisemwalo kuhusu ufungamano wa chdm na wakristu ni kweli.

09_10_kct1h5.jpg

Ni nadra sana kuona magazetini picha kama hii hapo juu

LAIZER.JPG

Ni aghlabu sana kuona picha kama hii magazetini

100_0330.JPG

Ni aghlabu sana kuona picha kama hii magazetini. Waislamu huendelea kuamini kuwa ukaribu wa chdm na ukristo ni mkubwa

kwa upande mwengine, vyombo vya habari havijawahi weka picha ya lipumba akiwa na viongozi wa kikristu. sidhani kama lipumba hajawahi kutana na viongozi wa kikiristu. kwenye mikutano ya kisiasa ya cuf imezoeleka kuona kwenye magazeti zimewekwa picha za wafuasi wa cuf wenye baraghashia, shungi, kanzu na ndevu. wafuasi wa cuf ambao hawana muonekano huu huwa hawaoneshwi. hali hii imewafanya wakristu waamini kuwa lisemwalo kuhusu ufungamano wa cuf na waislamu ni kweli. jitihada zangu za kupata picha ya lipumba na kiongozi yeyote wa dini ya kikristo zimegonga mwamba! nimecheki hadi kwenye tovuti ya cuf sijaiona!

kinacho nishangaza ni kwamba gazeti la tanzania daima lenye ukaribu na chdm halijawahi weka mfululizo picha za viongozi wa chdm wakiwa na viongozi wa waislamu. vilevile gazeti la fahamu lenye ukaribu na cuf halijawahi weka picha za viongozi wa cuf wakiwa na viongozi wa wakristo. magazeti haya yanayo hodhiwa na vyama hivi kwa nini hayavalii njuga kupambana na propaganda ya ccm!? uzembe na kutojali kwa vyama vya chdm na cuf kupambana na propaganda hii kunanishangaza sana!

watanzania tuna hulka ya kuamini kitu haraka. vilevile tuna hulka ya kung'ang'ania kitu tukisha kiamini. uzembe unaofanywa na chdm na cuf kupambana na propaganda hii umeshawagharimu sana cuf na kwa sasa naona umeanza kuwagharimu chdm. watanzania wameshaanza kuamini propaganda hii ya ccm. wakristu wameanza kukiona chama cha cuf kama chama kisichowahusu. ni cha waislamu wakiongozwa na wapemba. waislamu nao wameanza kukiona chama cha chdm kama chama kisichowahusu. ni cha wakristo wakiongozwa na wachagga. imani hizi zinazidi kujengeka vichwani mwa watanzania kutokana na udhaifu wa chdm na cuf katika kuipiga vita imani hii potofu.

piga, ua, garagaza, imani hii haiwezi kufutika. wakristu wengi wataendelea kuamini kuwa cuf ni chama cha waislamu na waislamu wengi wataendelea kuamini kuwa chdm ni chama cha wakristu. mtanzania akisha lishwa imani fulani, kumbadilisha ni kazi ngumu! huo ndiyo ukweli. anaekataa ukweli huu ana lake! mtanzania akiamini simba au yanga kumtoa huko ni kazi ngumu.

ukiangalia nchi zilizo tuzunguka, utabaini kuwa vyama vingi vikongwe vya siasa vimeangushwa. kanu na unip ni mfano. vilabu vingi vya mpira vilivyokua juu miaka ya nyuma havisikiki sana siku hizi. mifano ni kcc, villa, express. gormahia, afc leopards, bata bullets nk...... klabu hizi hazisikiki kwa kishindo hivi sasa. kwa hapa kwetu timu ni simba na yanga kila mwaka japo azam wanawasumbua kiasi fulani. hii ni dalili ya uhafidhina wa watanzania. ni wazito kubadilika!

Tanbihi:
chdm na cuf wajue kuwa bila ya kura za watanzania wote hakuna ushindi. chama chochote kikitegemea kura za waislamu tu au wakristu pekee, kimekwenda na maji. kitaendelea kuisindikiza ccm.

siyo kwamba nakukatisheni tamaa wana mageuzi, watanzania wenzangu. tuendelee kuunga mkono mageuzi lkn kwa hapa kwetu kazi ipo.

Nini kifanyike?

lifanyike moja wapo kati ya haya mawili;
1- ama vyama vijitahidi kufuta itikati hii ya ukanda na udini iliyojengeka katika vichwa vya watu. ikumbukwe kuwa kitu kikirudiwarudiwa sana masikioni mwa watu, huonekana kama ukweli!
2- au watanzania wajiunge na ccm ili kufanya mabadiliko humohumo. kinacho tukera ni jina ccm au ni matendo ya serikali ya ccm? "if you cant defeat them, join them". kauli hii haimaanishi kuwa mimi ni mwana ccm, la hasha! natoa changamoto ili tujaadili nini la kufanya.

nimeandika kwa nia njema nikisukumwa na uzalendo
nawasilisha!!!!!!!!!!!!
 
Back
Top Bottom