Uchaguzi 2020 CHADEMA hawaaminiki, tuwapime kwa ishu ya Korona tu tutapata picha

Amani Msumari

JF-Expert Member
Aug 21, 2016
1,830
976
Wanabodi,

Sina lengo la kuishambulia CHADEMA ila Kuna mambo yananitatiza kuhusu kuaminika kwao.

Sote tunajua timbwili walilolianzisha bungeni kuhusu korona mpaka kufikia kijikarantini kibabe. Wakati wenyewe wanajikaranti, wapiga kura wao walikuwa wanapambana uraiani kutafuta mkate wao wa kila siku.

Ila nikawaza, hivi kweli hawa wanauchungu na wapiga kura wao? Hivi hawa wanajua wapiga kura wao wanatafutaje riziki zao? Jibu nikalipata kuwa hawana uchungu na wapiga kura wao. Mgombea wao akiwa huko ughaibuni aliwasapoti kwa 💯%.

Wakati wabunge wa CHADEMA wakijikarantini, wenzao wa CCM walisimama kidete bila kuogopa kufa kuwapigania wapiga kura wao na watanzania kwa ujumla. Mbaya zaidi, CHADEMA iliwafukuza wabunge waliokataa mpango huo dhalimu. Ninashangaa wakijiita chama cha demokrasia, hamna kitu hapo.

Kama hayo hayatoshi, nilidhani CHADEMA watapiga kelele kuzitaka mamlaka zihairishe uchaguzi kwani kuna gonjwa la hatari la korona. Aah wapi, mwenyekiti aliyekuwa anavaa Kama ninja au Batman pamoja na sauti ya Lissu kutoka Tena sijui mji gani huko ubelgiji sasa wanakusanya watu, no social distance no facial masks. Wakihojiwa wanasema korona ipo, sasa watu hawa Kama wanaamini hivyo, si watakuwa wauwaji hawa?

Anyway, nimegundua nini ujue? Jamaa wanamkubali sana jembe JPM kwa vitendo ila wanamkataa kwa maneno. Matendo yao yanamkubali sana bwana mkubwa na ndio maana nikaandika uzi huu:

Uchaguzi 2020 - Zikiwa zimebaki siku 20, wapinzani wanashindana huku akili na mioyo yao ikiamini mshindi ni Magufuli

Tuwakatae wapinzani kwani wamejidhihirisha kuwa sio waaminifu.

Tarehe 28 kura zote kwa John Magufuli, mbunge na diwani wa CCM.

Tanga.
 
Joni alikimbilia chato
Asubutu! Mtu asiende kwao?
Akili ya kuambiwa changanya na yako, usiwe mwepesi Kiasi hicho. Kwani Chato ikikuwa free covid-19 zone hata useme alikimbilia huko?

Mwigulu Nchemba aliapishiwa Chato. Kama haitoshi, Magufuli aliutangazia umma kuwa mwanae aliigua korona

Mjiongeze wajameni
 
Nafurahi issue ya corona haikua na imapct kubwa sana kwetu. Ila kama ingevamia basi tungepukutika kama kuku wa mdondo.

Mnamuoma anko mshindi lakini mimi namuona ni mtu mwenye roho mbaya asiyejari maisha ya wengine
 
Joni alikimbilia chato Amani, huwezi kupinga hilo
 
Kwani wao ndo walikuwa wanasimamia wizara ya afya hadi wapimwe kwa corona. Mbona mgombea wenu alikimbia Ikulu zaidi ya miezi mitatu amefichama kijijini kama alikuwa haogopi sasa alikwenda kufichama nini.
 
Issue ya Korona imemharibia sana Mbowe huko Hai. Haeleweki kabisa huko.
Hiyo corona Mzee alikimbilia Chato miezi kadha.

Watanzania wanahitaji maisha bora (fedha mfukoni) nyie mnakuja na ma flyover,sgr,stiglers,na majengo.Nani aliwatuma?
Lissu msemakweli mlimshindwa kwa marisasi,sasa anawakomesha uwanjani kweupee.Huyo shetani mnayemtumikia siku zake zimeisha.
 
Nafurahi issue ya corona haikua na imapct kubwa sana kwetu. Ila kama ingevamia basi tungepukutika kama kuku wa mdondo.

Mnamuoma anko mshindi lakini mimi namuona ni mtu mwenye roho mbaya asiyejari maisha ya wengine
Hana ushindi wowote hawa sisimu mbumbu tu.
Msumbiji, zimbabwe, angola, zambia nk mbona hakuna corona kama tanzania?

Nchi nyingi za Africa azikuadhirika sana na corona.
Sisimu wamekazana oooh kwasababu ya magufuli, ooooh ameibuka shujaa wa corona.

Upumbavu nao ni sifa, kuna siku atawaitia chumbani mtaenda kwa zamu.
 
Issue ya Korona imemharibia sana Mbowe huko Hai. Haeleweki kabisa huko.

Ukiangalia ile video vizuri akiwa anagombana na polisi kuna jamaa nyuma alikua amevaa barakoa! haha sasa sjajua anafanya nn kwenye umati, anyway kwa kuongezea, hawa jamaa ni wafinyaji sana wa uhuru wa maoni, ukianza na youtube channel yao ile official sasahv kila video wakitoa wanafunga uwanja wa comment, ukienda twitter kwenye page ya binti kidomo wao ukimpa makavu anakublock
 
Nafurahi issue ya corona haikua na imapct kubwa sana kwetu. Ila kama ingevamia basi tungepukutika kama kuku wa mdondo.

Mnamuoma anko mshindi lakini mimi namuona ni mtu mwenye roho mbaya asiyejari maisha ya wengine
Kaka hiyo unayoongelea wewe n "labda" yaani hiyo imeisha na Magu ameibuka kidedea
 
Nafurahi issue ya corona haikua na imapct kubwa sana kwetu. Ila kama ingevamia basi tungepukutika kama kuku wa mdondo.

Mnamuoma anko mshindi lakini mimi namuona ni mtu mwenye roho mbaya asiyejari maisha ya wengine
Vyuo na shule zilifungwa kuwanusuru wanafunzi, serikali ikahimiza tahadhari zote kama social distancing, kusimamisha mijumuiko kama kwenye matamasha mbalimbali, kutumia sanitizers na barakoa hadi hali ya maambukizi ilipoonekana kupungua sana. Ni hatua gani angechukua zaidi aonekane anawajali wengine?!
 
Sasa mbona mnawabeza CHADEMA kwa kufuata hatua za tahadhari?
 
Back
Top Bottom