Sababu ya kufukuzwa=Ameenda kinyume na ILANI, SERA pamoja na Maazimio ya CDM..kama mtu akienda kinyume na ilani ya chama chake mojakwamoja kwenye kampeni zilizopita ulikuwa unadanganya wapiga kura wako..mfano kipindi cha kampeni, Shibuda angesimama na KUSEMA "NATAKA POSHO ZIONGEZWE KWA WABUNGE" je wewe Ben Ungempa kura yako?Hebu tuendeleze mjadala kama wachangiaji huru.ni kwa nini Shibuda afukuzwe? mtindo gani utumike kumfukuza? Je kuna madhara yoyote politically kwa wananchi na chama chake?Na je,asipofukuzwa kuna madhara yoyote kwa chama na wafuasi wake?Je,njia ya kumfukuza kupitia matamshi ya viongozi au kamati kuu tu inatosha kuonyesha dhamira ya dhati ya uwajibikaji kwa wapiga kura na matumizi mazima ya Demokrasia huru kupitia mfumo wa vyama vingi na mawazo huru?
Hii point usingeitoa wewe ningeigongea ka-like. Hujawahi kuwa na mapenzi mema na chadema hata siku mojaZitto amepotoka kidogo kwenye hili, hamuwezi mkajenga chama chenye watu wenye mawazo sawa, utakapokuwa na chama cha upinzani na viongozi wake wakawa wanakubaliana kila wakati, fahamu kuwa chama hicho bado hakina wigo mkubwa wa kiuongozi,na kadri kitakavyoendelea kuwa hivyo ndivyo kinavyozidi kufunga milango kwa watu wengine kujiunga na chama hicho na hivyo kujifungia milango ya kuuonyesha umma mtandao mkubwa wa kiuongozi uliotayari kuchukua nchi...Hii sio issue yenye hadhi ya kujadili kwenye kikao kikubwa kama cha kamati kuu, unless kama hawana vitu vya maana vya kuongelea so wameamua wauze chai tu...; ingetosha tu kupotezea kwa kusema msimamo wa chama ni kufutwa kwa posho zotejapo mbunge mmoja mmoja anaweza akawa na mawazo yake binafsi, unless kama kuna hoja nyingine kubwa kuliko hii na hili la posho linatumika tu kama kisingizio cha kumfukuza...
Sio point ya kukubalika na wapiga kura wake, zitto amesema Chedema kinaendeshwa kwa taratibu, kanuni na katiba so kama hawezi aondoke CDM sasa ni chama kikubwa kisipo kisipotenda kulingana na standards na wanacho kiamini kitapoteza sifa na muelekeo wake sasa hivi.Makao makuu CDM mnamiliki maamuzi ya kumfukuza au kutokumfukuza, ama Shibuda ana miliki wapiga kura ambao kwao yeye ndiye jembe lao la ukweli wako tayari kufa nae hata ahame chama chenu. Shibuda ataenda kwa Cheyo na bado atakuwa na vote kubwa sana.
Sababu ya kufukuzwa=Ameenda kinyume na ILANI, SERA pamoja na Maazimio ya CDM..kama mtu akienda kinyume na ilani ya chama chake mojakwamoja kwenye kampeni zilizopita ulikuwa unadanganya wapiga kura wako..mfano kipindi cha kampeni, Shibuda angesimama na KUSEMA "NATAKA POSHO ZIONGEZWE KWA WABUNGE" je wewe Ben Ungempa kura yako?
Asipofukuzwa kuna madhara mengi sana mfano mimi mpaka sasa sina imani na shibuda hata kidogo.
Mtindo wa kumfukuza=Apewe barua inayosema yeye sio mwaminifu kwa chama chake then barua imtake arudishe kadi ya chama halafu ndio mwisho wa mchezo huo.
Mkuu siku nyingine usitumie hiyo analysisBy the way zitto is not trusted!!! anaonekana kuanzisha makundi ndani ya cdm just kwa kutumia ushawishi kidogo alio nao...Lakini sishangai just see the following analysis of kigoma politicians in cdm
Dr Aman Walid Kaburu------from kigoma....was in CDM kwa unafiki akarudi CCM
David Kafulila....From kigoma.....Was in CDM umbea na kutoa siri za chama caused him to go to NCCR MAGEUZI
Zitto Kabwe...From kigoma.....In CDM now but not Trusted.......to no one knows but i dought magamba part
from above analysis i don't tust zitto
zitto alitofautiana na watu sio chamaNimesoma mwananchi uk wa 4 nashangaa zitto anasema shibuda afukuzwe kwa kutofautiana na chama. mimi naona tofauti za mawazo ni kawaida. kama basi ni kosa la kufukuzwa zitto awe wa kwanza maana alizungumza na waandishi kupinga msimamo wa chama wakati shibuda alizungumza bungeni anakolindwa na sheria. zitto anataka chadema ianguke nimwonavyo
Ni kweli kabisa mtu kama julius malema (President - ANC Youth league) kwa siasa za Tanzania angekuwa ameshafukuzwa zamani, ni mtu ambae ana ushawishi mkubwa sana ndani na nje ya ANC, na mara nyingi amekua akitoa mawazo yake nje ya vikao vya ANC ambayo mara nyingi yanapishana na sera za ANC, mfano mzuri ni ile sera ya nationalisation of mines, hii sio sera ya ANC lkn Malema siku zote anaisimamia, na mara nyingi sana amekuwa mstari wa mbele kupinga na kukosoa sera za ANC hadharani ambazo hazileti haki na usawa kwa kwa weusiNadhani Colin Powel angekuwa mwanachama wa chama cha siasa Tanzania angekuwa ameshafukuzwa,pia Julius Malema mwenyekiti wa vijana wa chama cha ANC angekuwa mwanachama wa chama cha siasa Tanzania angekuwa ameshafukuzwa.