CHADEMA, hapa Lwakatare alikuwa anamaanisha nini?

Status
Not open for further replies.
Mkuu Maranya,
Binafsi nimeichunguza kwa makini sana hiyo video, sina masaka nayo kabisa! Hata hivyo, shaka niliyonayo ni WHY NOW?! Kwamba kwanini wameamua kui-release sasa wakati kuna sakata la Kibanda huku video yenyewe ikionesha ni ya muda mrefu!! Hata hivyo, from UMAFIA POINT OF VIEW, jibu la WHY NOW tunaweza kusema kwamba it's now when it's the right time!!
Ngoja nikuambie kitu kimoja Mwita, Siasa ni moja ya viwanja vya maovu duniani...!! CHADEMA na CCM wote ni waovu tu; danganyeni hao hao!! Na uovu huu ni pamoja na kujengeana twaswira mbaya kwa jamii....the winner always is the one who's smarter!! Niseme tu kwamba, always you've been so smart, lakini leo CCM wamewazidi maujanja!! That's how politics works, huwezi then SIASA si fani muafaka kwako, either rudi kanisani au msikitini kawe mtoa mahubiri!....!!

Mkuu NasDaz nataka nikukumbushe kwamba Mwigulu aliwahi kuibuka na tuhuma za kutumiwa message za vitisho na wabunge wa Chadema.
Lakini tangu Mabere Marando wa Chadema alipokuja na ushahidi wa kwamba ccm wamenunua mtambo wa kutengeneza sms (sms spoofing) ile sinema ilikufa kifo cha kawaida sana.

Pamoja na mtazamo wako kwamba hapa tumenaswa nataka nikuhakikishie kwamba Chadema haijanaswa na watanzania hawawezi kudanganyika na propaganda za kijinga kama hii ya kutengeneza video. Nani asiyejua kwamba ccm ndiyo yenye vyombo vyote vya dola? sasa kama wanazo video za viongozi wa Chadema wakipanga mauaji dhidi ya raia muda wote wamekuwa wakisubiri nini kuwakamata??

Ndugu yangu kanisani ninakwenda na nitaendelea kwenda kwa ajili ya kumuabudu Mungu lakini pia kwenye siasa nitaendelea kuwepo kwahiyo utaendelea kuniona sana hadi siku mwenyezi Mungu atakapoamua vinginevyo.
 
Last edited by a moderator:
kaka mambo mazito sana,nimekula ban nimekuja kivingine,ntarudi kivile mwisho wa mwezi,but chadema is a disaster!
Magamba mtapalangana saana kujinasua lakini ukweli mwisho wa siku utajulikana tuu, kuuwa muuwe nyinyi mnasingizia CHADEMA, watu wenye akili hamuwezi kuwadanganya!!!!
 
CHADEMA bana, issue zikiwakalia upande mnajidai ni kupoteza muda.

Ni mara ngapi CHADEMA wamekuwa wakipost utumbo JF na kushabikiwa humu ndani? Double standards!

The winner never quits! pambana kijana.
Utumbo una grade bwana, huu ni grade ya mwisho na umeoza unamuumbua mwenye nao!.
 
Aisee umekomaa!!!!

Ni page ya 28 naona unapoint moja tu "movement ya lips!!"

Wewe unadhani alietengeneza hii move hakulijua hilo? Tambua kwamba mtengenezaji lazima ajitahidi kuingiza maneno yatakayoendana na 'lips movement!!'

Wakati ukiyakomalia haya(pengine kwa maslai binafsi) jiulize ni kweli CDM ndio walimuua Mwangosi? Je, ni kweli ndio waliomteka Dr. Ulimboka? Je CDM ndio waliomuua kijana wa Moro? Ukimaliza hapo rudi kwenye issue ya Kibanda, usikie Bashe anasemaje!! Alafu rudi hapa uihusishe CDM (Lwakatare) na hii video, u-connect dots, zikioana japo kwa 20% endelea kukomaa hadi Lwakatare akamatwe!!

NAHISI ULIHUSIKA KWA KIASI FLANI KTK UTENGENEZWAJI YA HII STUPIDITY CLIP!! PATHETIC.

Inaonekana mtengenezaji alikomalia hilo la movement ya lips na yey anajua hilo kuw akwenye sauti hawakuzingatia na wameumbuka hasa pale inapoanza kama BONGO MOVIE vile , yani anayeongea anambiwa MIC kuwa atayari action.
 
Makachero kutoka Makao Makuu ya Polisi wamevamia Makao Makuu ya Chadema iliyopo Kinondoni, kwa kile kinachoaminika ni Clip iliyowekwa kwenye Jukwaa hili hapo jana iliyomrikodi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Wilifred Lwakatare, mpaka sasa wapo ndani ya Ofisi ya Makao Makuu wakiendelea na mchakato wao kwenye ofisi ya Katibu Mkuu aidha tuta update kinajiri kwa kadiri ya kitakachoendelea.


Duh! Tutegemee kukamtw akk na MENO ya TEMBO ummo ofisini kwnai hawa ni wazee wa Kubambikiza.
yani unatgemea KATIBU MKUU awe an siri aiweke ofisini,
Ingekuwepo yule secretary wa juzi si angekuwa kasha ondoka nayo au kuisema.
 
Watanzania msiwe wepesi wa kukubali kila jambo. Hiyo video imetengenezwa na wala si ya kweli. Kumbukeni kwenye ulimwengu wa IT kila kinawezekana. Msidanganyike CCM wameshikwa pabaya. Hizo ni propaganda za Nape na Mwigulu!
 
Kwa mambo kama haya, ni dhahiri kuwa CCM imefika mwisho. Mungu nipe uhai niendelee kuyaona haya kabla 2015
 
Nyie chadema kumbe hovyo sana. Mko tayari kutetea ujinga kwasababu tu unahusu chadema.

Je hiyo sauti sio ya Lwakatare? Je picha sio yake?

Kama hii picha imetengenezwa basi Lwakatare na chadema nendeni polisi na mahakamani mara moja.

Hiyo picha imepigwa kwa simu au pen ambayo ilikuwa most likely kwenye mfuko wa shati.

Mipango mingi ya ujambazi hufanywa kwenye public areas. Ni rahisi hata njama zikigundulika kuruka kuliko ukifanyia nyumbani au ofisini.

Huyu Lwakatare afadhali sana alikosa ubunge. Ni mtu hatari kabisa.
 
tatizo wewe ni katika wale wanopenda kuona kile wanachoamini na si kuamini kile wanachokiona,wenye macho wanaiona hiyo video,you cant cover up kitu kilichowazi kwenye mitandao and every thing,chadema has to come clear kwenye hili,mambo ya kuisingizia serikali kwa uovu wa wenu yamefikia mwisho,mungu ana mambo yake ona mnavyodharirika sasa,kumbe hata chacha wangwe yalimkuta yatokanayo na vikao kama hivi vya mikakati ya lwakatare!shame on you guys
Na waliomlipua Mwangosi mchana kweupe ni CHADEMA, waopiga watu marisasi ARUSHA ni CHADEMA, waiomteka Dr Ulimboka hadi akawataja ni CHADEMA, WEWE NI VIPI unafanya kazi kitengo gani???? Mbona unakuja na vitu vya ajabu ajabu hapa maana yake ni nini????

 
tatizo wewe ni katika wale wanopenda kuona kile wanachoamini na si kuamini kile wanachokiona,wenye macho wanaiona hiyo video,you cant cover up kitu kilichowazi kwenye mitandao and every thing,chadema has to come clear kwenye hili,mambo ya kuisingizia serikali kwa uovu wa wenu yamefikia mwisho,mungu ana mambo yake ona mnavyodharirika sasa,kumbe hata chacha wangwe yalimkuta yatokanayo na vikao kama hivi vya mikakati ya lwakatare!shame on you guys
Hiyo ndiyo VIDEO ya Mwigulu kwamba CHADEMA inapanga mauwaji ya wakubwa?????Hamna hata aibu kuleta vitu vya ajabu hapa????Peleka mkanda wako Polisi kama ushahidi waliohusika woote wakamatwe kama wauwaji washitakiwe!!!!!

 
Makachero kutoka Makao Makuu ya Polisi wamevamia Makao Makuu ya Chadema iliyopo Kinondoni, kwa kile kinachoaminika ni Clip iliyowekwa kwenye Jukwaa hili hapo jana iliyomrikodi Mkurugenzi wa Ulinzi na Usalama Wilifred Lwakatare, mpaka sasa wapo ndani ya Ofisi ya Makao Makuu wakiendelea na mchakato wao kwenye ofisi ya Katibu Mkuu aidha tuta update kinajiri kwa kadiri ya kitakachoendelea.

Niliandika kuhusu maelekezo ya Zoka kwa Kova na sasa ndio yanaendelea haya , ........
 
How to Detect a Doctored Photo

http://www.channels.com/episodes/16338290?page=7
Mkuu naona Clip hiyo wameishaichomoa, haipo, na nimekutana na maelezo haya....no download available. Nitafurahi kama nitaweza kupata source nyingine



dctrd11.jpg
 
Kama ilivyo kwa binadamu, kuna wengine baada ya kuiangalia hii video, hawataiamini hata kidogo kilichomo, wengine wataiamini lakini watasema Lwakatare amehongwa na wengine wataachwa tu maswali mengi, huku wengine wataiamini kabisa.

Tatizo lililo mbele ya CHADEMA litategemea na kiwango cha idara ya mahusiano ya jamii kufanya kazi makini kuliaminisha kundi ambalo limeamini/litaamini na lile ambalo bado linajiuliza kama hizi ndiyo nyendo za CHADEMA.

Kitengo cha mahusiano ya jamii CHADEMA kinakabiliwa na utoaji majibu mbadala kwa watu wanaodhani, kama CHADEMA kinaweza kupanga mbinu chafu za kumdhuru Mwananchi kwa manufaa ya kisiasa wakati hata bado hakijapewa na wananchi vitengo vya usalama wa raia (polisi, TISS ) itakuwaje kama wakipewa hizo taasisi.

Kama kiongozi mkuu wa maswala ya ulinzi wa chama ana fikra mbaya kama hizi, itakuwaje kama akikabidhiwa moja ya taasisi za ulinzi wa raia, kama inavyoeleweka, kila serikali mpya huleta watu wake inaowaamini wa ulinzi (TISS) na kama ilivyo tradition kwa maswala ya ulinzi, kuna uwezekano mkubwa kama CHADEMA ikishinda, Lwakatare anaweza akapewa moja ya taasisi hizi nyeti za nchi.

CHADEMA ina kazi mikononi mwake.
 
kulikuwa na post hapa jana kuwa CCM wametumia fedha takriban 80 million kutengeneza huu upuuzi wenu INDIA. kumbe kilichosemwa jana ilikuwa ni kweli ee. sasa yametimia magamba kung'oka madarakani kwa nguvu ya umma.
 
Hivi kuna mtu kajiuliza kwanini tukio la Kibanda lilipotokea tuu Ridhiwani Kikwete na Nnape Waliandika kwenye facebook wall zao kuwa .....semeni huyu naye katekwa na Rama wa Ikulu?

Walikuwa wanaandaa umma kuanza kujiuliza ili wakija na singo hii iweze kuaminika?

Imechukua muda gani tangu Mwigulu aliposema kuwa ana mkanda wa mipango ya mauaji na kuwa ameupeleka polisi kwa ajili ya uchunguzi nini kimefanywa na vyombo vya dola?

Kuna maelekezo yameshatolewa na Zoka kwenda kwa Kova kuwa amuite Lwakatare na amhoji kisha azungumze na vyombo vya habari kuwa wanamshikilia kiongozi mmoja wa Cdm kuhusiana na tukio lakutekwa na kupigwa kwa Kibanda , jambo wasilolijua ni kuwa tayari kuna CD zinazoonyesha tukio zima la tangu kutekwa na waliompiga kwani kwenye geti alilokuwa anaingia kibanda kuna camera ndogo za CCTV na tukio zima lilinaswa.....nasubiria kuona nini kinafuata..............

Aidha, kuna haja ya Membe kujitokeza kuwa ni kwanini ziara yake ya Morocco alienda na Zoka na kukaa kwenye hoteli yake kwa siku tatu bila kutoka walikuwa wanapanga nini na Zoka aliporejea alianza kutoa maelekezo gani juu ya jambo hili?

Mbona hatujamsikia rais akitaka tukio hili lichunguzwe na kuomba msaada nje kama lile la Padiri kuuliwa kule Znz?

Tuendelee kutafakari pamoja , inakuwaje Lwakatare ajirekodi kwa camera kubwa ya zaidi ya 8 mega pixels na 34 mm , hii ni kwa mujbu wa ukubwa wa picha ya Lwakatare, na hii ni camera ambayo ilitegeshwa wala sio simu kwani hii inaonekana kuwa haiyumbi hata kidogo , na kama ingekuwa simu basi walau picha zingecheza........nawatakia tafakuri njema sana ......tuendelee kuutafuta ukweli ili tuujue ......


Haya niliandika asubuhi .....sasa yametimia kwani makachero wa Polisi wameingia makao makuu ya CDM wakifuatilia, polisi waoga walishakuwa na hii clip from January but wameamua kufanya propaganda leo..........wataumbuka .......they have to be smart .....
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom