CHADEMA Haina Itikadi Kama Chama!

CHADEMA Haina Itikadi Kama Chama!

Nimepitia kwa Umakini Katiba ya Chadema tofauti na matarajio ya Chama chochote cha Siasa lazima kuweka msimamo wake hasa mlengwa wa Kiitikadi! Chadema haijaweka wazi kama ni Chama cha Kijamaa au ni Chama Cha Kibepari! Tofauti na CCM ambao wao Wanasema ni Chama cha Kijamaa japokuwa Ujamaa walisha Uweka kando! Vyama vingi duniani huonesha mlengo wake hasa kama ni kuamini Ubepari au Ujamaa! Hata marafiki zao wa Ujerumani na Uingereza wamebainisha mlengo wa Vyama vyao! Wanachama wa Chadema walio wengi hata hapa JF hawajui Itikadi ya Chama Chao(Inasikitisha sana)! Hakuna tofauti kati ya Chadema na Timu ya Simba wala Yanga kwani hawana Itikadi!
My Take: Chadema ijipambanua ina itikadi gani Ujamaa au Ubepari! Wanachadema jiulizeni Itikadi ya Chama chenu ni ipi?

mlengo wa kati kulia,uliza jingine
 
Tunaomba Kiongozi wa Chadema atujuze na kutoa maelezo juu ya Itikadi ya Chadema ni jambo la msingi tuielewe Chadema kama chama ambacho kinataka kupata ridhaa ya Watanzania kuongoza Nchi! Wale vijana mnaotukana hapa JF ebu acheni matusi kwa hii hoja! Slaa,Mbowe,Zitto,Mnyika,Regia,Lema,Ndesamburo,Lema wekeni msimamo wa itkadi ya Chadema hapa jamvini

Naona viroba original bado vinakusumbua,kapate supu hapo lumumba
 
Tundu lissu na jusaa once aliulizwa sikuile jussa alisema wao ni wariberari sio wajamaa aucapitalism lissu alidai kuwa wao wanafuata itikadi ya nguvu ya umma aliboronga sana sikuile
tundu lissu naye. inamaana hajui nchi ikiwa republic maana yake inaongozwa na nguvu ya umma!?
 
3.B. Itikadi ya CHADEMA
3.1.1 CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (center party).


3.1.2 CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wa nchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa, na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.

3.1.3 CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa soko huru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huru na sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katika maeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneo nyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.

3.1.4 CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia za nchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboresha huduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.

3.1.5 CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturi zetu zilizo nzuri.

3.1.6 CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.

3.1.7 CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenye kusimamia zaidi maslahi ya Taifa.

3.1.8 CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja ya taasisi muhimu ya kijamii.

3.1.9 CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katika kujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwa sehemu ya dola.

3.1.10 CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wake unawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.

3.1.11 CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katika kumiliki na kuendesha uchumi.

3.1.12 CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwa wananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili na hali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.

Source:Chama Cha Demokrasia Na Maendeleo – Chadema | Itikadi


Note:


1. Itikadi ya Mrengo wa Kati (Centre) – Huu ni mrengo kati ya Uliberali na Ujamaa wa kidemokrasia. Chadema inatamka hii kama itikadi yake kama chama. Kwa kawaida, Itikadi ya mrengo wa kati (centre) inaamini na kuunga mkono mambo makuu yafuatayo:

· Ongezeko la kodi linaloenda sambamba na ongezeko la vipato vitokanavyo na shughuli za uchumi (progressive taxation); Umiliki binafsi wa mali; Uhuru na haki ya wananchi mbele ya sheria; Uliberali wa kiuchumi na uliberali wa kijamii.
 
Centrism

In politics, centrism or the centre is a political outlook or specific position that involves acceptance or support of a balance of a degree of social equality and a degree of social hierarchy; while opposing political changes which would result in a significant shift of society either strongly to the left or the right.[SUP][1][/SUP] Centre left and centre right politics both involve a general association with centrism combined while leaning somewhat to their respective sides of the spectrum. The term is often used interchangeably with the Third Way, a political position popularized by Bill Clinton and Tony Blair in the 1990s, whereby policies favored a balanced approach and the removal of extreme ideologies.
 
Nafikiri maswali kama haya kwa kutosoma katiba au kupotosha mazuri ya CHADEMA hayatatokea tena.
 
Nafikiri maswali kama haya kwa kutosoma katiba au kupotosha mazuri ya CHADEMA hayatatokea tena.

Nimewaomba Mods waipandishe kwenye main thread ili kuondoa upotoshaji wa makusudi wa watu wa CCM
 
Tunaomba Kiongozi wa Chadema atujuze na kutoa maelezo juu ya Itikadi ya Chadema ni jambo la msingi tuielewe Chadema kama chama ambacho kinataka kupata ridhaa ya Watanzania kuongoza Nchi! Wale vijana mnaotukana hapa JF ebu acheni matusi kwa hii hoja! Slaa,Mbowe,Zitto,Mnyika,Regia,Lema,Ndesamburo,Lema wekeni msimamo wa itkadi ya Chadema hapa jamvini
itikadi yao inafanana na jina lako la bandia unalotumia kwenye JF ila tofauti ni kwenye herufi moja tu. Badala ya "MLENGO" wao wanaita "MRENGO".
 
Chadema hawana dira kwani walianzisha chama kama saccos na baada ya kupata wanachama wengi wakaona kiwe chama cha kisiasa ndo maana unaona na kusikia wakibadilisha katiba yao mara kwa mara. Ilikuwa saccos ya Mtei.
 
Thread ya kale 2011 ila soma katiba cdm vzr 3.1.1 na kuendelea .mrengo wa kati kushoto
 
CHADEMA naifananisha na yule kiongozi wa dini aliyetajwa katika kitabu cha Dini yake kuwa anapo waongoza waamini wake hajui ni wapi wanaelekea
 
Saccos haiwezi kuwa na itikadi .wachaga itikadi yao ni kupiga dili.kama kweli sio watu wa dili wajenge makao mkuu waache kupanga. Kuna tetesi kuwa wamepanga kwenye nyumba ya kiongozi na wanamlipa kodi na kila siku halambe wanazo fanya ni dili za wa kubwa. Kwanini wasifanye halambe ya kujenga makao mkuu? Halambe ya siku moja itajenga makao makuu ya kisasa.
 
Hiyo ni feature ya socialdemocracy systeam ya ZZK chadema wameikana

Chama cha ZZK kinafuata siasa ya ujamaa na kijitegemea ya mwalimu Nyerere na siyo Mixed economy. Na wamejitangaza hivyo na hivyo ndiyo azimio la Arusha lilivyokuwa linataka.
 
Back
Top Bottom