Nimepitia kwa Umakini Katiba ya Chadema tofauti na matarajio ya Chama chochote cha Siasa lazima kuweka msimamo wake hasa mlengwa wa Kiitikadi! Chadema haijaweka wazi kama ni Chama cha Kijamaa au ni Chama Cha Kibepari! Tofauti na CCM ambao wao Wanasema ni Chama cha Kijamaa japokuwa Ujamaa walisha Uweka kando! Vyama vingi duniani huonesha mlengo wake hasa kama ni kuamini Ubepari au Ujamaa! Hata marafiki zao wa Ujerumani na Uingereza wamebainisha mlengo wa Vyama vyao! Wanachama wa Chadema walio wengi hata hapa JF hawajui Itikadi ya Chama Chao(Inasikitisha sana)! Hakuna tofauti kati ya Chadema na Timu ya Simba wala Yanga kwani hawana Itikadi!
My Take: Chadema ijipambanua ina itikadi gani Ujamaa au Ubepari! Wanachadema jiulizeni Itikadi ya Chama chenu ni ipi?
@John Marwa, kwanza kabisa lazima wewe mwenyewe ufahamu maana ya Itikadi hizi na tofauti zake ktk dunia hii ya leo. Ujamaa unaujua wewe sio ujamaa unaotangazwa na vyama vya nchi za magharibi isipokuwa kwa VIAPAUMBELE ambavyo binafsi yangu husema hivi:- Is it the end justifies the Means
or is it the means justifies the end?.
Siasa za Vipaumbele ni itikadi zinazopingana ktk malnego ya ujenzi wa jamii husika kulingana na WATU na MAZINGIRA yao (There so many incarnations) hivyo huwezi kulazimisha vyama ktk mtazamo wa siasa ya Kijamaa na Kibepari bila kuitazama kwanza historia ya nchi husika maanake katika Upinzani wa vyama lazima kuwepo itikadi inayotawala na vyama vingine vikatokana na itikadi inayopingana na iliyopo.
Ujamaa umejikita zaidi ktk kuamini kwamba ndani ya mfumo wa Kibepari lazima kuna oppression ya watu wa chini kutokana na asili ya ushindani ndani ya Ubepari ambapo matajiri wachache ndio hu control vyanzo hivi na kushusha mishahara wa watu wa chini na kati. Hivyo Ujamaa ndani ya Ubepari kazi yake kubwa ni kulinda watu wa chini kwa malengo ya kutokuwa na matabaka yaani wana advocate a completely classless society.
Katika dunia yaleo yenye kupokea soko huria unakuta kwenye Ujamaa kuna ubepari na ktk Ubepari kuna Ujamaa na hapo ndipo upinzani unapopatikana - Zile fikra na siasa za kwamba shughuli zote za kuzalisha na kukuza uchumi ziwe mikononi mwa serikali hazitumiki tena isipokuwa wajamaa wanasisitiza REGULATIONS ambazo main goal is to dispel class distinctions kupata kuwa na harmonious society, free of oppression na financial instability.
Sasa how you gonna do that ndipo Wajamaa husema serikali ina wajibu wa ku control all means of production and distribution of goods. Kwa hilo sidhani kama CCM wapo upande huo wala sidhani kuna chama Tanzania kinaunga mkono serikali kumiliki njia zote za kuzalisha na kukuza uchumi japokuwa vyama vyote vinataka ujenzi wa classless society...
Hapa ndipo ngoma ipo maana sisi sote maskini, asilimia 99 ya Watanzania ni maskini wa hali na mali wasiokuwa na Mtaji isipokuwa wa magenge ya nyanya halafu tunaubeba Ubepari wakati huo huo tukitaka watu wote kuwa jamii isiyokuwa na matabaka!. Kifupi hakuna chama chenye itikadi inayofanana na zile za Ulaya isipokuwa vyama vyote vinabeba mazuri ya huku na kule kupingana na Uongozi ama muundo wa chama. Wasiokubaliana na JK au Nape watakihama chama na wasiokubaliana na Mbowe au Dr.Slaa ndio watakihama chama.