Kumekuwa Na mijadala mbalimbali hivi sasa baada ya ujio wa Act-wazalendo Na itikadi Yao ujamaa wa kidemokrasia almaaruf Kama mrengo wa kati kushoto,lakini natatizwa Na jambo moja wakati Fulani kulikuwa Na mdahalo kuhusu itikadi uliokuwa ukiongozwa Na dada Rose Mwakitwange Ccm ikiwakilishwa Na Nape Nnauye,Cdm Na Mabere Marando Na Cuf ikiwakilishwa Na Ismail Jussa,
nakumbuka Kama sikosei Cdm kupitia Marando walisema itakadi Yao mrengo wa kati kushoto ambao ndio mrengo wa Act-wazalendo,naomba kuuliza kwa wana Chadema itikadi yenu Ni ipi maana hatujasikia hata mara moja kutoka viongozi wakuu wakiizungumzia itikadi ya Chama.
jenga tabia ya kusoma katiba za vyama
3.B. Itikadi ya CHADEMA
3.1.1 CHADEMA ni chama cha itikadi ya MRENGO WA KATI (centerparty).
3.1.2 CHADEMA ni chama kinachoamini kukuza na kuimarisha uchumi wanchi kwa kutumia raslimali za nchi yetu bila kuathiri uhuru wa Taifa,na kuhakikisha kuwa umma kwa ujumla unanufaika na raslimali zao.
3.1.3CHADEMA inaamini katika kujenga na kuimarisha uchumi wa sokohuru, utakaoheshimu na kulinda haki na mali za watu, biashara huruna sekta ya watu binafsi bila kupoka mamlaka ya umma katikamaeneo nyeti hususani pale penye hitilafu ya soko au penye maeneonyeti ya kiuchumi. Tunaamini katika soko huru sio soko holela.
3.1.4 CHADEMA inaamini kuhakikisha matumizi bora ya raslimali asilia zanchi ili zichangie kikamilifu katika pato la taifa na hasa kuboreshahuduma za kiuchumi zinazotumiwa na wananchi wote.
3.1.5CHADEMA inaamini katika uzalendo na kuthamini mila na desturizetu zilizo nzuri.
3.1.6 CHADEMA inaamini katika uhuru chini ya sheria zilizo za haki.
3.1.7 CHADEMA inaamini katika siasa ambazo ziko juu ya vyama zenyekusimamia zaidi maslahi ya Taifa.
3.1.8 CHADEMA inaweka umuhimu wa pekee katika familia kama moja yataasisi muhimu ya kijamii.
3.1.9 CHADEMA inaamini katika umuhimu wa uhuru wa kuamini katikakujenga maadili ya mwanajamii mmoja mmoja bila kuifanya dini kuwasehemu ya dola.
3.1.10 CHADEMA inaamini taifa linaundwa na watu, hivyo uhai wakeunawategemea watu, na mabadiliko yake yanatokana na watu.
3.1.11 CHADEMA inaamini katika kujenga uwezo wa wazawa katikakumiliki na kuendesha uchumi.
3.1.12 CHADEMA inaamini kumiliki raslimali na mali miongoni mwawananchi kunawapa uhuru zaidi hivyo tunataka kujenga chama na baadaye taifa lenye kutoa fursa, ambapo kila mtu bila kujali asili nahali yake anaweza kutimiza na kufanikiwa kadiri ya vipaji vyake.
http://www.chadema.or.tz/cdmdownloads/katibayachadema.pdf