CHADEMA Haina Itikadi Kama Chama!

John Marwa

JF-Expert Member
Joined
May 25, 2011
Posts
275
Reaction score
28
Nimepitia kwa Umakini Katiba ya CHADEMA tofauti na matarajio ya Chama chochote cha Siasa lazima kuweka msimamo wake hasa mlengwa wa Kiitikadi!

CHADEMA haijaweka wazi kama ni Chama cha Kijamaa au ni Chama Cha Kibepari! Tofauti na CCM ambao wao Wanasema ni Chama cha Kijamaa japokuwa Ujamaa walisha Uweka kando!

Vyama vingi duniani huonesha mlengo wake hasa kama ni kuamini Ubepari au Ujamaa! Hata marafiki zao wa Ujerumani na Uingereza wamebainisha mlengo wa Vyama vyao!

Wanachama wa
CHADEMA walio wengi hata hapa JF hawajui Itikadi ya Chama Chao(Inasikitisha sana)! Hakuna tofauti kati ya CHADEMA na Timu ya Simba wala Yanga kwani hawana Itikadi!

My Take:
CHADEMA ijipambanua ina itikadi gani Ujamaa au Ubepari! Wanachadema jiulizeni Itikadi ya Chama chenu ni ipi?

 
Tupe premises mkuu zilizokufanya uende kwenye hiyo conclusion mkuu. Otherwise ts a Crap!
 
Kuna maana gani kuandika uwongo kwenye katiba ya chama kama hao wanamagamba uliowataja?...Umeuona wapi wakitekeleza Ujamaa wanaodai kuufuata?
Kuandika na kutekeleza unaona kipi bora?...Tunawajua nyie kuwa ni mabingwa wa maandishi na kusoma data zisizofanyiwa uchunguzi!
Kuna mkubwa wenu mmoja akianza kusoma miradi ya umeme inayofanyiwa kazi, utajua hakutakuwa na shida nchi hii tena...Lakini njoo kwenye utekelezaji, sihitaji kukupa mifano, maana hapo huenda unatumia jenereta!
 

Gamba likiwa kwenye ubongo huwezi fikiria!
 
Tunaomba Kiongozi wa Chadema atujuze na kutoa maelezo juu ya Itikadi ya Chadema ni jambo la msingi tuielewe Chadema kama chama ambacho kinataka kupata ridhaa ya Watanzania kuongoza Nchi! Wale vijana mnaotukana hapa JF ebu acheni matusi kwa hii hoja! Slaa,Mbowe,Zitto,Mnyika,Regia,Lema,Ndesamburo,Lema wekeni msimamo wa itkadi ya Chadema hapa jamvini
 

"the head is out of control" serious measures to be taken
 
hivi hakuna itikadi nyingine zaidi ya ujamaa na ubepari? ccm itikadi yake ni nini? na je itikadi ya ccm ndo inayoonekana katika mfumowa utawala wa nchi yetu? ujamaa ni nini na ubebari ni nini? hivi hizi si porojo tu za kuwafanya watu wasifikirie mifumo au itikadi zinazowafaa kwa jamiihusika!
 
Tunataka majibu zaidi kutoka CDM
 
Nini hasa maana ya Ubepari kama itikadi? maanake nijuavyo mimi Upebari ni mfumo wa kiuchumi unaosisitiza njia zote za production kuwa private owned, ziendeshwe kwa faida na malipo halali kwa wafanyakazi wake. Privatization haiwezi kuwa itikadi hata siku moja kama sii kuturudisha kule kwenye vita baridi.

Marekani UK na nchi kibao leo hii duniani zinafuata mfumo huu wa kiuchumi tukiwamo hata sisi leo hii, hivyo huwa nashindwa kuelewa mtu anaposema Ubepari kama ITIKADI ya chama wakati CCM ndio wanabinafsisha mashirika bila kufikiri kuliko hata Mabepari wenyewe.

Na ndio maana huuliza hivi Democratic ya kina Obama wanapingana na Ubepari!
 

grrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrrr so unaweza kusema CCM ambao ni chama tawala wana itikadi?
 
Zamani CCM walikiwa 'to the left' sijui sasa practically watasema wako upande gani. CHADEMA ni 'centre -left' Angalia manifesto yao 2010 (chadema manifesto)
 
Mkandara na Mzee wa KIjijini mwacheni kijana kazidiwa baada ya kunywa maji ya bendera yao yamemdhuru kaa E coli .Mpeni pole huyo .
 

 
Tunakubali,CCM itikadi yao ilikuwa ujamaa.Yako wapi hayo mafanikio ya ujamaa?Matokeo yake wamefilisi mashirika ya umma.Sasa ni mabepari wanawanyonya wananchi.wakijilimbikizia mali ya umma wao wenyewe.Tunafikiri na wewe nimmowapa wa hawo wanyonyaji wa CCM ndio maana unaleta hoja isiyokuwa maana kwa wa Tanzania.Wacha ulimbwikene wewe mfisadi.Lete za kuwatetea wananchi.
 

Hata panya na mende pale kabatini waliisoma wakaelewa hata hawakuitafuna katiba ya chama kuwa Chadema ni mrengo wa kati usiofungamana na east/west. You Slave in the new era!
 
soma website ya chadema vyote utavikuta itikadi mrengo na mengine mengi tu, usiwe mvivu wa kutafuta knowledge soma mwenyewe tu ukishindwa ndo uombe msaada na si lazima kiongozi wa chama akujibu vitu viko wazi na unaweza kuvipata usipende kutafuniwa kila kitu utazoea vibaya
 
Zamani CCM walikiwa 'to the left' sijui sasa practically watasema wako upande gani. CHADEMA ni 'centre -left' Angalia manifesto yao 2010 (chadema manifesto)

Safi sana mkuu. Kama mtu ameuliza swali ajibiwe kama ulivyofanya. Hilo ndilo tendo la kiungwana kwa waungwana: Hoja dhidi ya hoja badala ya matusi. Kumbe CHADEMA ina itikadi lakini inaonekana wengine hawaijui ndio maana badala ya kujibu hoja wanaanza kutukana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…