CHADEMA haikamatiki Arumeru-RAI

Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,534
13,225
Gazeti la Rai limeripoti kuwa chama cha CDM kinakipeleka puta chama cha mapinduzi huko Arumeru kutokana na mikutano ya CDM kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika maeneo ya vijijini tofauti na idadi ndogo ya watu wanaohudhuria katika mikutano ya CCM.
Kwa mujibu wa maripota wa RAI hali hii si ishara nzuri hata kidogo kwa chama hicho tawala.
Habari hii iliyotolewa na gazeti hili imewashangaza wengi kwani ni gazeti hilihili liliripoti wiki iliyopita tu kwamba wamefanya utafiti katika kata zote 17 na kugundua kuwa mgombea wa CCM atashinda kwa asilimia 61% huku mgombea wa CDM akiambulia asilimia 38.5%
 
Cdm ni wakati wa kulinda kura kwa gharama yoyote,
magamba ndicho wanachopanga sasa
 
kwani hili gazeti lilishaachana na siasa uchwara...au lilijivua gamba.!!
 
Nimeona kichwa cha habari kwa mbali kwa wauza magazeti sikupata nafasi ya kununua.
Sikuamini kama hilo ni gazeti la Rai ninalolijua.
 
Umesema eti ni gazeti gani hilo ambalo limetoa taarifa hiyo hapo chini vile? Kama gazeti lenyewe ni RAI basi habari hiyo itakua imekosewa hivyo kamrudishie Bashe akaipitie upya na kuifanyia uhariri 'usiofungamana' na ukombozi nchini.

Gazeti la Rai limeripoti kuwa chama cha CDM kinakipeleka puta chama cha mapinduzi huko Arumeru kutokana na mikutano ya CDM kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika maeneo ya vijijini tofauti na idadi ndogo ya watu wanaohudhuria katika mikutano ya CCM.

Kwa mujibu wa maripota wa RAI hali hii si ishara nzuri hata kidogo kwa chama hicho tawala.
Habari hii iliyotolewa na gazeti hili imewashangaza wengi kwani ni gazeti hilihili liliripoti wiki iliyopita tu kwamba wamefanya utafiti katika kata zote 17 na kugundua kuwa mgombea wa CCM atashinda kwa asilimia 61% huku mgombea wa CDM akiambulia asilimia 38.5%
 
Gazeti la Rai limeripoti kuwa chama cha CDM kinakipeleka puta chama cha mapinduzi huko Arumeru kutokana na mikutano ya CDM kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika maeneo ya vijijini tofauti na idadi ndogo ya watu wanaohudhuria katika mikutano ya CCM.
Kwa mujibu wa maripota wa RAI hali hii si ishara nzuri hata kidogo kwa chama hicho tawala.
Habari hii iliyotolewa na gazeti hili imewashangaza wengi kwani ni gazeti hilihili liliripoti wiki iliyopita tu kwamba wamefanya utafiti katika kata zote 17 na kugundua kuwa mgombea wa CCM atashinda kwa asilimia 61% huku mgombea wa CDM akiambulia asilimia 38.5%

Hadi gazeti la Rai likaja na utafiti mwingine ulio na mtazamo tofauti na walioutoa wiki moja iliyopita utambue kwamba wameelekezwa na ccm ama gamba kuu rost tamu kubadilisha aina na mbinu za propaganda. Makamanda mkijisahau tu kidogo na ku relax ccm watatumia nafasi hiyo vizuri, hawawezi kufanya kosa kuacha kutumia upenyo wa ninyi kurelax. Kilichopo hapo ni Nassari kuendelea na kampeni ya mtaa kwa mtaa na kwa baadhi ya watu/wazee mashuhuri kama alivyofanya kwa kuitembelea familia ya shujaa wa Tanganyika na Meru, Marehemu Japhet Kirilo.

Ni kweli kwamba mikutano ya chadema inakusanya watu wengi sana kuliko ccm lakini hilo litoshe kuwapa ujumbe makamanda walioko mstari wa mbele kwamba ccm lazima watakuwa na plan B, plan c na hata ikiwezekana plan D. Na kwa sehemu kubwa hii mechi ya arumeru mashariki wataicheza nje ya uwanja, kwahiyo ni lazima wapiganaji wa chadema huko mstari wa mbele wajipange kukabiliana na hujuma za ccm nje na ndani ya uwanja.

Kwakweli sitarajii kabisa this time around nisikie habari ya kwamba ccm wamechakachua, kwakuwa naamini sasa mbinu zao zote zinafahamika na uwezo wa kuzikabili na kuzishinda uko ndani ya chama.
 
Nimeona kichwa cha habari kwa mbali kwa wauza magazeti sikupata nafasi ya kununua.
Sikuamini kama hilo ni gazeti la Rai ninalolijua.

Mkuu kila mtu imemshangaza.Labda wameona aibu kwa habari yao ya wiki iliyopita
 
Hadi gazeti la Rai likaja na utafiti mwingine ulio na mtazamo tofauti na walioutoa wiki moja iliyopita utambue kwamba wameelekezwa na ccm ama gamba kuu rost tamu kubadilisha aina na mbinu za propaganda. Makamanda mkijisahau tu kidogo na ku relax ccm watatumia nafasi hiyo vizuri, hawawezi kufanya kosa kuacha kutumia upenyo wa ninyi kurelax. Kilichopo hapo ni Nassari kuendelea na kampeni ya mtaa kwa mtaa na kwa baadhi ya watu/wazee mashuhuri kama alivyofanya kwa kuitembelea familia ya shujaa wa Tanganyika na Meru, Marehemu Japhet Kirilo.

Ni kweli kwamba mikutano ya chadema inakusanya watu wengi sana kuliko ccm lakini hilo litoshe kuwapa ujumbe makamanda walioko mstari wa mbele kwamba ccm lazima watakuwa na plan B, plan c na hata ikiwezekana plan D. Na kwa sehemu kubwa hii mechi ya arumeru mashariki wataicheza nje ya uwanja, kwahiyo ni lazima wapiganaji wa chadema huko mstari wa mbele wajipange kukabiliana na hujuma za ccm nje na ndani ya uwanja.

Kwakweli sitarajii kabisa this time around nisikie habari ya kwamba ccm wamechakachua, kwakuwa naamini sasa mbinu zao zote zinafahamika na uwezo wa kuzikabili na kuzishinda uko ndani ya chama.

Salute mkuu wangu!
 
Umesema eti ni gazeti gani hilo ambalo limetoa taarifa hiyo hapo chini vile? Kama gazeti lenyewe ni RAI basi habari hiyo itakua imekosewa hivyo kamrudishie Bashe akaipitie upya na kuifanyia uhariri 'usiofungamana' na ukombozi nchini.

Mkuu usinichekeshe.
 
Nadhani gamba rostam wana BIFU TAKATIFU na mamvi now day,nlidhani unasema Raia mwema
 
Tatizo la Tanzania ni kwamba kura haziamui mgombea.... CCM ni wezi, na huwa wanaibiana hadi wenyewe kwa wenyewe
 
Rai ina mambo labda kuna mtu mwingine tena wanaanza kumtafuta baada ya Salim
 
............huko Arumeru kutokana na mikutano ya CDM kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika maeneo ya vijijini tofauti na idadi ndogo ya watu wanaohudhuria katika mikutano ya CCM..........[/QUOTE]

hii ni sawa na kutamba "timu yetu safi sana - inacheza kwa ball possession ya 70% dhidi ya 30% ya mpinzani", while magoli ndiyo yanayo-count at the end of the day!

ccm wao wanajua wazi kuwa arumeru kwa fair play hawawezi kushinda huo uchaguzi, so wanawaachia chadema wajisahau na ball possession yao ili wawasurubu kwenye counter-attack (kwenye injury time) kwa kutumia goal poachers wao (uwt)!

so kwenye injury time, nawashauri chadema wa-resort kwenye formation ya 10-0-0!!!

kama unajua football, utajua ninachokisema....
 
hapa hakuna kuchakachua, makamanda tupo huku na kila kura italindwa, mpaka kitaeleweka, tumechoka na hizi siasa za kurithishana utadhani ni nchi ya kifalme, lazima nassari ampoteze sioi kwa mbali sana,
 
Nimepata tetesi kwamba iwapo Upepo utaendelea hivi Basi CCM itamkafara mgombea wake uhamiaji ili wamwengue Kwa kigezo cha kutokukana uraia wa nchi mojawapo. Hii italeta heshima Kwa Chama Kwamba walishindwa Kwa kutoshiriki of which ni katika harakati za kufuta mtazamo Kwa watanzania kwamba sasa CCM kwishaee Kama wakishiriki Na kushindwa.. Ila mpaka sasa bado timu iliyotumwa Na Chama bado wanatoa majibu yenye utata kwamba CCM inakubalika Na kundi la wazee wengi Na kinabibi ambao Kwa mtazamo wao wanadai ndio waliotunza shahada za kupigia Kura. Wanasema CHADEMA kinaungwa mkono Na Kundi kubwa la vijana ambao wengi hawana Shahada za kupigia Kura Na wale wachache wenye shahada wameshazipoteza.. Ni tetesi jamani sina uhakika zina ukweli kiasi gani
 
Back
Top Bottom