CHADEMA haikamatiki Arumeru-RAI

CHADEMA inatakiwa watangaze sera kwa nguvu sana, halafu wahubiri umuhimu wa wananchi kulinda kura zao!
 
Nimefanikiwa kulipata hapa mbezi kweli mwandishi amesema chadema hawakamatiki na mikutano yao imekuwa ikipata watu wengi zaidi ya ccm hasa vijana .

Hata hivyo wametahadharisha kuwa kupata watu wengi siyo tiketi ya kupata ushindi kwani ccm wao wameamua safari hii kutumia kampeni ya nyumba kwa nyumba, mtu kwa mtu ilikuhakikisha wanapata ushindi na mbinu hii waliitumia Igunga.

Zaidi linasema ccm inadeal zaidi na maeneo ya kaskazini na karibu na mlima meru ambapo kuna wapigakura wengi watuwazima wasioyumbishwa tofauti na chadema kukazania watu wa mjini hasa maeneo ya usa, katiti na kadhalika kwenye vijana wengi ambao hajajiandikisha au hawana msimamo.

Na katika kuhakikisha wanapata ushindi huo wemewatuma makada wao katika kata zote 17. kusaka kura nyumba kwa nyumba.

My take. Nakumbuka igunga maneno ya Lison Mukama kuwa "tumeshinda kisayansi" huwenda walitumia mbinu hii ya mtu kwa mtu au nyumba kwa nyumba.

Ni vema chadema wakahakikisha kote walipopita makada wa ccm wanatuma makamanda kwenda kusafisha njia na kuondoa sumu.
Pia hao makada huenda ndiyo wanaopanga njama za kununua shahada au mikakati ya kuiba kura.
 
Mkuu kila mtu imemshangaza.Labda wameona aibu kwa habari yao ya wiki iliyopita
Ni kazi sana kuutetea uongo, kuna member mmoja huwa anasema kuitetea CCM lazima uwe na akili yamaiti. Tukiondoa ushabiki kama hali itaendelea hivi na CDM waka-maintain speed hilo jimbo litakwenda CDM. Kwa nini nasema hivyo,

CCM wamefanya makosa mengi sana ya msingi. Sioi hakufaa kabisa kugombea, uraia wake una utata, hana uzoefu kwenye siasa, mimi nilikuwa namhofia zaidi Sarakikya kuliko Sioi, Sarakikya angewasumbua sana CDM. Kosa lingine nikujaribu kuufanya uchaguzi huu uwe wa kimila zaidi kwa sababu ndani ya jimbo kuna makabila ya aina mbalimbali. Kosa jingine ni hili la kumweka Mkapa kuwampiga kampeni. Wanajua Mkapa ana kashifa nyingi walitegemea ile nguvu ya kiburi ingesaidia kuwanyamazisha wapinzani.

CCM wanategemea nini, kusema ukweli ni miujiza. Wanachotegemea ni mawakala na wasimamizi, kura kubadilishwa kwa tarakimu za matokeo ya kituo. Pili wanategemea labda?? kama kuna vituo hewa vitakavyoongeza kura. Kura zilizofanya CCM washinde Igunga (3,000) ni za kununua kadi ya mpiga kura. Safari hii hiyo mbinu hata kama ipo haitasaidia, hii husaidia tu panapokuwa na difference ndogo lakini kama ni kubwa say ya 10,000 votes, mbinu hii haiwezi fanikiwa.
 
Nimepata tetesi kwamba iwapo Upepo utaendelea hivi Basi CCM itamkafara mgombea wake uhamiaji ili wamwengue Kwa kigezo cha kutokukana uraia wa nchi mojawapo. Hii italeta heshima Kwa Chama Kwamba walishindwa Kwa kutoshiriki of which ni katika harakati za kufuta mtazamo Kwa watanzania kwamba sasa CCM kwishaee Kama wakishiriki Na kushindwa.. Ila mpaka sasa bado timu iliyotumwa Na Chama bado wanatoa majibu yenye utata kwamba CCM inakubalika Na kundi la wazee wengi Na kinabibi ambao Kwa mtazamo wao wanadai ndio waliotunza shahada za kupigia Kura. Wanasema CHADEMA kinaungwa mkono Na Kundi kubwa la vijana ambao wengi hawana Shahada za kupigia Kura Na wale wachache wenye shahada wameshazipoteza.. Ni tetesi jamani sina uhakika zina ukweli kiasi gani

ni kweli,yawezekana hapo kuna neno
 
Gazeti la Rai limeripoti kuwa chama cha CDM kinakipeleka puta chama cha mapinduzi huko Arumeru kutokana na mikutano ya CDM kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika maeneo ya vijijini tofauti na idadi ndogo ya watu wanaohudhuria katika mikutano ya CCM.
Kwa mujibu wa maripota wa RAI hali hii si ishara nzuri hata kidogo kwa chama hicho tawala.
Habari hii iliyotolewa na gazeti hili imewashangaza wengi kwani ni gazeti hilihili liliripoti wiki iliyopita tu kwamba wamefanya utafiti katika kata zote 17 na kugundua kuwa mgombea wa CCM atashinda kwa asilimia 61% huku mgombea wa CDM akiambulia asilimia 38.5%

Mkuu, vipi tena si wewe wiki iliopita ulilishambulia gazeti la Rai kuwa la kinafiki.

Leo limeiandika habari njema kwa Chadema limekuwa Gazeti pendwa.

Chadema bana wanatapata tu kama pweza anaetaka kufa.
 
Mkuu, vipi tena si wewe wiki iliopita ulilishambulia gazeti la Rai kwa la kinafiki.

Leo limeiandika habari njema kwa Chadema limekuwa Gazeti pendwa.

Chadema bana wanatapata tu kama pweza anaetaka kufa.

Mkuu wangu nimelisifia wapi gazeti la Rai? Nilichofanya ni kuripoti walichoandika tu.
 
Mkuu, vipi tena si wewe wiki iliopita ulilishambulia gazeti la Rai kuwa la kinafiki.

Leo limeiandika habari njema kwa Chadema limekuwa Gazeti pendwa.

Chadema bana wanatapata tu kama pweza anaetaka kufa.
Tofautisha kati ya maoni na utafiti, kilichokuwa kinashambuliwa ni procedures za utafiti kama walivyouita hatukuwa tunashambulia gazeti bila sababu. Haya ya leo ni maoni si utafiti kama wangeita utafiti tungehoji vile vile.
 
Kuna mantiki gani kumnadi mgombea ambaye si raia wa Tanzania?. Wana CCM wote waliopo ndani ya Arumeru wameonekana hawafai isipokuwa SIOI ambaye ni raia wa Kenya?. Hapa CCM tumechemsha kiasi kikubwa sana, ningekuwa ni mwenyeji wa Arumeru Mashariki nisingeshiriki kwenye kampeni za CCM kwani siko tayari kumpigia kura ama kumchagua Mkenya ili awe mbunge wetu, huyu inabidi akawe mbunge wa Kericho kama si Kakamega.
 
Mkuu, vipi tena si wewe wiki iliopita ulilishambulia gazeti la Rai kuwa la kinafiki.

Leo limeiandika habari njema kwa Chadema limekuwa Gazeti pendwa.

Chadema bana wanatapata tu kama pweza anaetaka kufa.

Mwana wa mwenye Pihechidi za bure nyiiiiiiiiingi bana
 
Gazeti la Rai limeripoti kuwa chama cha CDM kinakipeleka puta chama cha mapinduzi huko Arumeru kutokana na mikutano ya CDM kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika maeneo ya vijijini tofauti na idadi ndogo ya watu wanaohudhuria katika mikutano ya CCM.
Kwa mujibu wa maripota wa RAI hali hii si ishara nzuri hata kidogo kwa chama hicho tawala.
Habari hii iliyotolewa na gazeti hili imewashangaza wengi kwani ni gazeti hilihili liliripoti wiki iliyopita tu kwamba wamefanya utafiti katika kata zote 17 na kugundua kuwa mgombea wa CCM atashinda kwa asilimia 61% huku mgombea wa CDM akiambulia asilimia 38.5%

Ni baada ya kuona kuwa mauzo yanazidi kushuka, hatimae limeona ni bora kurudi KUNDINI! Hongera RAI. Mtafuteni Kubenea awape somo vizuri!

Hadi gazeti la Rai likaja na utafiti mwingine ulio na mtazamo tofauti na walioutoa wiki moja iliyopita utambue kwamba wameelekezwa na ccm ama gamba kuu rost tamu kubadilisha aina na mbinu za propaganda. Makamanda mkijisahau tu kidogo na ku relax ccm watatumia nafasi hiyo vizuri, hawawezi kufanya kosa kuacha kutumia upenyo wa ninyi kurelax. Kilichopo hapo ni Nassari kuendelea na kampeni ya mtaa kwa mtaa na kwa baadhi ya watu/wazee mashuhuri kama alivyofanya kwa kuitembelea familia ya shujaa wa Tanganyika na Meru, Marehemu Japhet Kirilo.

Ni kweli kwamba mikutano ya chadema inakusanya watu wengi sana kuliko ccm lakini hilo litoshe kuwapa ujumbe makamanda walioko mstari wa mbele kwamba ccm lazima watakuwa na plan B, plan c na hata ikiwezekana plan D. Na kwa sehemu kubwa hii mechi ya arumeru mashariki wataicheza nje ya uwanja, kwahiyo ni lazima wapiganaji wa chadema huko mstari wa mbele wajipange kukabiliana na hujuma za ccm nje na ndani ya uwanja.

Kwakweli sitarajii kabisa this time around nisikie habari ya kwamba ccm wamechakachua, kwakuwa naamini sasa mbinu zao zote zinafahamika na uwezo wa kuzikabili na kuzishinda uko ndani ya chama.

you have spoken my mind!
 
Chadema kuweni makini sana hawa magamba hawasomeki,wekeni mawakala wanaoaminika siku ya kupiga kura na waambieni wapiga kura kulinda kura zao,hakuna kulala mpaka kisomeke.Machalii msije kutuangusha awamu hii.
 
Wanasema CHADEMA kinaungwa mkono Na Kundi kubwa la vijana ambao wengi hawana Shahada za kupigia Kura Na wale wachache wenye shahada wameshazipoteza.. Ni tetesi jamani sina uhakika zina ukweli kiasi gani

sio kweli kwamba vijana wa kimeru hawatunzi vitambulisho vya kupigia kura kwa sababu vitambulisho hivi vina matumizi mengi katuka shughuli zao kama vile kusajili line za simu,matumizi ya kibenki n.k

KWA HISANI YA MTU WA TANZANIA
 
NAPENDA KUWAASA MAKAMANDA WAJIPANGE KWELIKWELI MAANA HUU NI UCHAGUZI WA MIKAKATI NA PROPAGANDA!!! NI UCHAGUZI KATI YA MAFISADI NA NGUVU YA UMMA!!!
Naomba niwapashe wadau wangu juu ya mambo yanayofanywa na CCM kama propaganda yao muhimu kuchakachua mambo kabla ya uchaguzi wenyewe.

1. TBC ni television ya taifa lakini kwa asilimia 99.9 Inaleta habari za Kampeni arumeru zinazohusu CCM tu!!! Ndio maana nasema baada ya kumuacha Tido Mhando TBC= TVT now days!
2. nasikitika kusema kuwa hata ITV imechakachuliwa na CCM, Hii sio ITV niliyokuwa naifaham!! Ukiangalia habari zao za Arumeru zipo Biased! Yaani Wakimuonyesha mgombea wa CCM wanaonyesha na Umati wote wa watu waliohudhuria!!! Kibaya ni kwamba kwa upande mwingine wakionesha Mgombea wa CHADEMA wanamuonyesha yeye tu bila kuonesha wanaomsikiliza, au wakionyesha wanaonesha watu waliopo ukingoni ukingoni ili kutuposha tufikiri waliohudhuria mkutano wa CHADEMA walikuwa wachache!! Hii ni AIBU !!!!! ITV badilikeni maana mzee Mengi tuliyemuamini kwa kulaani ufisadi tunaweza kufikiri na yeye ni fisadi kwa sababu ya jambo hili tu!!! Pili hata magazeti mengi yanafanya hivyo hivyo. yaani yamenunuliwa na mafisadi!!! Kweli nilikuwa naipenda ITV lakini naona nakaribia kuacha kuiangalia!!!
2. Nas
 
Gazeti la Rai limeripoti kuwa chama cha CDM kinakipeleka puta chama cha mapinduzi huko Arumeru kutokana na mikutano ya CDM kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika maeneo ya vijijini tofauti na idadi ndogo ya watu wanaohudhuria katika mikutano ya CCM.
Kwa mujibu wa maripota wa RAI hali hii si ishara nzuri hata kidogo kwa chama hicho tawala.
Habari hii iliyotolewa na gazeti hili imewashangaza wengi kwani ni gazeti hilihili liliripoti wiki iliyopita tu kwamba wamefanya utafiti katika kata zote 17 na kugundua kuwa mgombea wa CCM atashinda kwa asilimia 61% huku mgombea wa CDM akiambulia asilimia 38.5%

gazeti limejikomba tu hilo
ukweli ni kwamba sioo rahisi kwa CDM yetu hii kushinda ARUMERU hata YESU ashuke. mbowe amedhoihiorisha ni jinosi gani ana ubaguzi wa wazi wazi ndani ya chama yaani yeye amehamia arumeru na kukataa kusaidia kata yoyote tanzania kati ya kata ozte nane zinaozgombewa?.
 
na pia inabidi tukubali kuwa ushindi hautokani na mauzulio ya mikutano ya kampeni cz kuna watu wanaattend kampeni while wameshauza shahada zao na fomu no 16 lubuva kakataa kuitumia la msingi hapo ni kukomaa na kampeni ya nyumba kwa nyumba na elimu ya uraia itolewe kwa nguvu zote makamanda coz kwenye hii game yupo taikuni mwenye nywele nyeupe anainterst zaidi ya kimtandao na amesharejea na anasema yupo tayari kwa mapambano ya aina yoyoyte so lets be carefull makamanda
 
hawa jamaa zetu wa chadema huwa na matamnio ya mvuta bangi.wakishashindwa wanadai ura zilichakachuliwa
 
1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom