CHADEMA haikamatiki Arumeru-RAI

Gazeti la Rai limeripoti kuwa chama cha CDM kinakipeleka puta chama cha mapinduzi huko Arumeru kutokana na mikutano ya CDM kuhudhuriwa na umati mkubwa wa watu katika maeneo ya vijijini tofauti na idadi ndogo ya watu wanaohudhuria katika mikutano ya CCM.
Kwa mujibu wa maripota wa RAI hali hii si ishara nzuri hata kidogo kwa chama hicho tawala.
Habari hii iliyotolewa na gazeti hili imewashangaza wengi kwani ni gazeti hilihili liliripoti wiki iliyopita tu kwamba wamefanya utafiti katika kata zote 17 na kugundua kuwa mgombea wa CCM atashinda kwa asilimia 61% huku mgombea wa CDM akiambulia asilimia 38.5%

Hizi habari toka kwenye magazeti New Habari Coop si huwa mnaziponda kila siku kuwa hazihaminiki, leo imekuwaje au kisa imesifia CDM!?
 
Back
Top Bottom