Bahati mbaya ya walio wengi wanajadili siasa bila kuwa na ufahamu wa siasa, na hivyo kubaki wakikubali matokeo ya mambo ya kisiasa na kujaribu kupinga yale mambo yaletayo matokezeo hayo; nitajaribu kuandika kwa ufupi sana ili niweze kueleweka;
1; migongano ya mawazo na mikwaruzano katika chama chochote cha siasa ndio kujizatiti kwake, kwani siasa siku zote haitaki wala haihusudu sera ama falsafa ya "dogmatism" kuwa mmoja akisema basi neno lake halibadilishwi wala halipingwi.,kutohoji mambo katika chama hakuwapi watu nafasi ya kujisikia kuwa wao wanamiliki chama kama wanachama na kujaribu kuendesha chama cha siasa kama kanisa kuwa msemaji ni "padri" pekee na wengine hawana ruhusa ya kuhoji basi ni "kukiua" chama hiko. Upevuko wa kisiasa na kuimarika ni kukubali kuishi katika malumbano ya hoja ambayo hayaharibu lengo la chama cha siasa husika-fahamu kuwa lengo la chama cha siasa ni kushika dola na kutawala.,hivyo mifarakano na majibizano katika kufikia lengo hili ni kitu kisichozuilika kulingana na experience, uwezo wa kutafakari, elimu na mazingira na wakati wa kutumia wazo fulani. Nasema haya kwa kuwa hivi sasa kuna mtazamo katika chama changu kuwa mtu yeyota ambae anamawazo tofauti ama fikra yeyote inayopingana na mwenyekiti ama "wenye chama'' KAULI ama wazo hilo si la sawasawa na hivyo litapingwa wazo hilo lakini mbaya zaidi kupingwa mtuo wazo hilo.,nasema haya kwa kuwa yaminifika binafsi, na pia bado mifano hallsi na ya wazi ipo kwa watu ambao ni prominent katika chama lakini wanafanyiwa fitna na majungu kwa kuwa wanamawazo tofauti juu ya uendeshaji na usimamiaji wa shughuli za kichama.
2; Historia ya vyama vya siasa duniani na hata hapa nchini kwetu imeprove notion kuwa malumbano na mitazamo tofauti inakuza na kuimarisha chama, nitakumbuka John Adams alivyotofautiana na wanachama wenzake kuhusu mamlaka ya bunge na hata baadae kuhusu quasi-war na hata mwanawe John Quincy Adams akiwa kama ex-president aliwahi kusimama mahakamani kama mwanasheria akitetea kuachwa huru kwa watumwa na kufutwa kwa biashara hiyo hali ya kuwa chama chake na Rais wa wakati huo Andrew Jackson..,ukiachana na historia katika siasa za kimataifa, bado hapa nchini kwetu watu walitofautiana ndani ya vyama tangu wakati tanu haiko madarakani "akina sykes na kitwana" lakini hata baada ya kupata dola bado mifarakano ilikuwepo baina ya nyerere na wadau wengine kwenye chama watu wakawekwa vizuizini wengine in partition bado hata akina kawawa waliwahi kurushiana ngumi baada ya mgongano na akina oscar ndani ya mikutano ya chama na hili halikuwafanya kutomiliki na kutawala dola sawasawa.
3; Leo zipo hisia na mitazamo kuwa malumbano ya hoja na mivutano ndani ya chama ni kitu hatari kwa maendeleo ya chama na kushika hatamu, tupo tunaozuiliwa kusema kwa kuwa tuliwahi kusema kitu tofauti na mawazo ya wangine hapo nyuma, wapo tunaokaribia kutolewa ndani ya chama kwa kupinga baadhi ya mambo ambayo tunaamini kuwa hayapo sawa ndani ya CHADEMA na tulithibitisha na kutoa hoja za msingi juu ya misimamo na kupinga kwetu. Lakini nasema kuwa hili haliwezi kutufikisha katika malengo yetu makuu bali litatuvuruga.,haikuwahi kutokea mtu kuendesha kundi lolote la watu kwa mawazo yake tu " hata ikiwa kundi hilo ni familia yake ya yeye, mkewe na mtoto wao" vipi kwa chama cha siasa.??? Sisemi kuwa mimi binafsi nahitaji kubaki mwanachama na kiongozi wa chama lakini pia nakiri na naweza kuthibitisha kuwa TUNAWAHITAJI PIA MHESHIMIWA ZITTO NA SHIBUDA hata wakiwa na mitazamo inayopingana na msimamo fulani wa chama.
4; Kama migongano na mivutano ya kimawazo katika chama ingelikuwa ni hatari kwa chama, yanayoendelea ccm yalitosha kukiondolea nguvu ya moja kwa moja ya chama hiko lakini tumeshuhudia kuwa bado hayajakishusha chama hiko kisiasa,.tumeshuhudia matokea ya ubunge hivi karibuni na matokea ya chaguzi ndogo za madiwani jinsi ccm ilivyoweza kujishindia viti vingi.,ni kuonyesha kuwa mifarakano ndani ya chama hakiharibu lengo kuu la kushika dola.. TUSOMA, TUJIFUNZE NA TUKOMAE KISIASA.,HAKIKA TU WACHANGA SANA KATIKA HILI.