Hata nilipo taka kufikiria ili nijiunge na chama kimoja wapo cha upinzani nilipata jibu la haraka sana kama vyama vya upinzani vya tz havina viongozi makini na wenye nia ya upinzani wa dhati zidi ya chama tawala ccm.
Nilijiuliza wako wapi hawa..JIDAWI, MAPALALA, LAMWAI, NGAWAIYA, MREMA, MARANDU, WALID AMAN KABARU,TAMBWE HIZA.HAMAD RASHID, SAID ARFI NA LEO DR SLAA.
Hawa ni watu waliojiaminisha kwa wtz kama wao ni viongozi shupavu wanao taka mabadiliko.
Na wtz wakawaamini wakawafuata na wako watz walifungwa waliopata vilema walipoteza wapendwa wao kwa ajili yao lakini leo jiulizeni waliko watu hawa na misimamo yao ya kisiasa.
Ndio maana mm nimeamua kutomuamini kiongozi yeyote yule wa vyama vya upinzani tz.
Waswahili wanamsemo wao.. Jini ukisha lilijua jina lake nirahisi kuliita na kulipandisha.
Sitoshangaa siku nikimuona mbowe au mbatia wakibadilika na wakiwa kama dr slaa na wengine niliotangulia kuwataja.
Nitabaki ccm na nitakuwa wa mwisho kuondoka.