Mwanajamii
JF-Expert Member
- Mar 5, 2008
- 7,063
- 71
Kuna kila dalili kwamba CHADEMA hakitamsimamisha DR. SLAA kugombea Urais kupitia Chama hicho mwaka 2015 na kwamba mbadala wake anaandaliwa kutoka ndani ya CCM. Habari zilizopatikana toka ndani ya CHADEMA zinasema, uongozi wa Chama hicho hauridhishwi na utendaji kazi wa Katibu Mkuu huyo kwa kile kinachosemekana kwamba anaingilia shughuli za Chama ngazi za chini kwa mfano MKOA WA KILIMANJARO, uongozi ngazi ya Wilaya na Mkoa hususani BAZIL LEMA, PHILEMON NDESAMBURO, na LUCY OWENYA wanamlalamikia Dr.SLAA kuendesha uchaguzi katika Kata ya NJORO bila kuwashirikisha , ambapo JOHN JOMBA NKOY alichaguliwa kuwa Mwenyekiti wa CHADEMA Kata ya NJORO na ABDULRAHMAN YUSUF SHARIFF kuwa Katibu. Aidha Dr. SLAA alijaribu kulipa deni la CHADEMA linalokadiriwa kuwa Tsh. Mil.94 kwa TRA, kitendo ambacho Uongozi wa Chama uliona kama huko ni kujipendekeza kwani kuna madeni mengi tena makubwa ya kulipa hasa yale ambayo anayedai ni Mwenyekiti au swahiba zake. Swali ni, je huwenda ukawa mwisho wa Dr. SLAA ndani ya CHADEMA?MAONI YANGU: Watakuwa hawajamtendea haki Dr SLAA kwa vile ni yeye aliyengarisha nyota za watu wa aina mbalimbali na hata Chama kikapata idadi kubwa ya wabunge na kufakiwa kuunda kambi ya upinzani bungeni. Toa maoni yako.