CHADEMA bado mno Kupambana na CCM

CHADEMA bado mno Kupambana na CCM

chadema ni genge la wahuni wanaotumia kivuli cha chama cha siasa kuwatapeli watanzania wasiojielewa

Nami nimeliona hilo hivi karibuni. Mwanzoni nilikuwa na mawazo kwamba Chadema ni mkombozi wa wanyonge kumbe ni walewale.
 
Source ya nini?, wewe huoni kama wabunge wa chadema na wabunge wa ccm wote wako bungeni kwa manufaa ya matumbo yao?.
Kwa hiyo ulitaka wawepo dodoma kwa ajili ya matumbu yako?
 
Ndio maana mboye aliona akichukua ela kwa nimrod haina shida,
 
Kimsingi CHADEMA haipo kwa ajili ya wananchi, ipo kwa ajili ya kutafuta pesa kupitia mgongo wa siasa!
 
Ndugu wana JF,

Nitakachoandika hapa ni mtizamo wangu, na niko tayari kuelimishwa na kukosolewa maana hiyo ndiyo demokrasia.
Watanzania walio wengi wanapenda mabadiliko mema na ya tija kisiasa hapa Tanzania. Pia wamechoka na ukiritimba, rushwa, wizi wa mali za umma, ufujaji wa pesa za walipa kodi, kupeana vyeo na madaraka bila kujali vigezo husika nk.

Tulikuwa na mfumo wa chama kimoja kwa muda mrefu sana hivyo chama na serikali tawala walikuwa huru kufanya watakavyo bila ya kupingwa.

Ulipokuja mfumo wa vyama vingi vya siasa, wanasiasa wengi walianzisha vyama vya upinzani kwa malengo waliyoyajua wao wenyewe. Vyama vingi kati ya hivyo vilivyoanzishwa vimekufa ama vimezorota tokana na sababu mbalimbali.

Chadema bado kipo na ndicho kinaonekana kama ndiyo mpinzani wa CCM, huku kikiungwa mkono na watanzania wengi waliopigika kimaisha. Watanzania hawa wanaamini kupigika kwao kimaisha ni sababu ya kutawaliwa na CCM kwa muda mrefu. Kila jambo lililobaya ndani ya Tanzania wanailaumu CCM na serikali yake, kwa mfano kuzorota na kushuka kwa elimu, matibabu, wizi wa mali za umma, ufujaji wa pesa za walipa kodi nk.

Chadema ambacho kinaonekana ni matumaini ya wanyonge waliopigika kimaisha kimekuwa kinapiga kelele sana za kuilaumu CCM kwa kuwasababishia maisha magumu Watanzania, na pia kinaomba watanzania wakipe ruhusa ya kutawala Tanzania.

Kwa upande wangu naona CCM na Chadema vyote ni sawa, kwa maana kwamba yanayofanywa na CCM ndiyo yanayofanywa na Chadema.
Kwa kufafanua kidogo ni kwamba nilitegemea kwamba Chadema kama chama cha upinzani, chenye uchungu wa kweli na maisha ya watanzania kingekuja na utaratibu, mipangilio na utendaji tofauti kabisa na ule wa CCM.

Chadema wanasema CCM wanafuja pesa za walipa kodi, lakini Chadema ina wabunge wengi tu ndani ya bunge la Jamhuri. Sisi sote tunajua jinsi gani wabunge wetu wanavyokula pesa za walipa kodi, kuanzia mishahara mikubwa, posho za vikao na marupurupu kibao.

Nilitegemea wabunge wa Chadema wangelikataa kuchukua mishahara mikubwa, posho za vikao na marupurupu ili kuonesha kwamba wanalipinga hilo jambo kivitendo.

Kama walishindwa kuacha kuchukua huo mshahara mkubwa na posho za vikao basi nilitegemea wachukue hizo pesa na wazirudishe kwa watanzania. Wangeweza kutoa sehemu fulani ya mshahara wao kila mwezi na kuchanga pamoja ili kulisaidia jimbo moja la chadema katika ununuzi wa madawati, madawa nk. Kama kuna wabunge wa CDM 10 bungeni, wakachanga 2,000,000 kila moja utaona wazi kwamba wanaweza pata 20,000,000 kwa mwezi kwa ajili ya kusaidia jimbo moja la Chadema. Lakini sioni tofauti kati ya yale wafanyayo CCM na CDM. Wote wanachukua mapesa kujaza matumbo yao, wanachukua ma-VX, posho za vikao nk.

Tutawaamini vipi Chadema kama kweli wanataka kuwaletea watanzania mabadiliko iwapo nao wanatenda yaleyale wanayoyapigia kelele majukwaani?. Kweli tuna upinzani wa kisiasa Tanzania?, kwa mtazamo wangu naona mpinzani wa kweli bado hajazaliwa Tanzania.
Upeo wako mdogo sana. Unayaangalia mambo juu juu mno
 
Umeongea vitu muhimu sana, wenye akili na waelewe... Hawa chadema nao ni majambazi tu, hakuna tofauti waliotuonyesha sisi wananchi, tofauti pekee ambayo mimi nimeona kutoka kwao ni vurugu yani kutokuwa wastaarabu na huku wakiamini wanachofanya wao ndio hasa kinafaa kwa kila Mtanzania. Lakini mambo mengine yote sioni kama wanatofautiana na sisiemu. Tena hapo kwenye posho ndio hatari maana wamefikia mpaka kufukuzana, rejea Zito kufukuzwa kwa kupinga hizo posho japo wao wanasema amewasiliti. Sasa sijui ndio huu usaliti wa kugomea posho ama ni usaliti mwingine.

Namalizia kwa kusema si chadema wala sisiemu ambao wapo kwa ukombozi wa Mtanzania kwa kifupi bado sijaona chama labda na tena labda Jahazi Asilia
 
Ndio maana mboye aliona akichukua ela kwa nimrod haina shida,
Afadhari yako wewe ambaye unapost ujinga lkn unajua utalipwa 7,000/day. kuna wengine siwaelewi ni kwanini wanashinda humu kuposti upuuzi kwa masaa 24
 
Ndugu wana JF,

Nitakachoandika hapa ni mtizamo wangu, na niko tayari kuelimishwa na kukosolewa maana hiyo ndiyo demokrasia.
Watanzania walio wengi wanapenda mabadiliko mema na ya tija kisiasa hapa Tanzania. Pia wamechoka na ukiritimba, rushwa, wizi wa mali za umma, ufujaji wa pesa za walipa kodi, kupeana vyeo na madaraka bila kujali vigezo husika nk.

Tulikuwa na mfumo wa chama kimoja kwa muda mrefu sana hivyo chama na serikali tawala walikuwa huru kufanya watakavyo bila ya kupingwa.

Ulipokuja mfumo wa vyama vingi vya siasa, wanasiasa wengi walianzisha vyama vya upinzani kwa malengo waliyoyajua wao wenyewe. Vyama vingi kati ya hivyo vilivyoanzishwa vimekufa ama vimezorota tokana na sababu mbalimbali.

Chadema bado kipo na ndicho kinaonekana kama ndiyo mpinzani wa CCM, huku kikiungwa mkono na watanzania wengi waliopigika kimaisha. Watanzania hawa wanaamini kupigika kwao kimaisha ni sababu ya kutawaliwa na CCM kwa muda mrefu. Kila jambo lililobaya ndani ya Tanzania wanailaumu CCM na serikali yake, kwa mfano kuzorota na kushuka kwa elimu, matibabu, wizi wa mali za umma, ufujaji wa pesa za walipa kodi nk.

Chadema ambacho kinaonekana ni matumaini ya wanyonge waliopigika kimaisha kimekuwa kinapiga kelele sana za kuilaumu CCM kwa kuwasababishia maisha magumu Watanzania, na pia kinaomba watanzania wakipe ruhusa ya kutawala Tanzania.

Kwa upande wangu naona CCM na Chadema vyote ni sawa, kwa maana kwamba yanayofanywa na CCM ndiyo yanayofanywa na Chadema.
Kwa kufafanua kidogo ni kwamba nilitegemea kwamba Chadema kama chama cha upinzani, chenye uchungu wa kweli na maisha ya watanzania kingekuja na utaratibu, mipangilio na utendaji tofauti kabisa na ule wa CCM.

Chadema wanasema CCM wanafuja pesa za walipa kodi, lakini Chadema ina wabunge wengi tu ndani ya bunge la Jamhuri. Sisi sote tunajua jinsi gani wabunge wetu wanavyokula pesa za walipa kodi, kuanzia mishahara mikubwa, posho za vikao na marupurupu kibao.

Nilitegemea wabunge wa Chadema wangelikataa kuchukua mishahara mikubwa, posho za vikao na marupurupu ili kuonesha kwamba wanalipinga hilo jambo kivitendo.

Kama walishindwa kuacha kuchukua huo mshahara mkubwa na posho za vikao basi nilitegemea wachukue hizo pesa na wazirudishe kwa watanzania. Wangeweza kutoa sehemu fulani ya mshahara wao kila mwezi na kuchanga pamoja ili kulisaidia jimbo moja la chadema katika ununuzi wa madawati, madawa nk. Kama kuna wabunge wa CDM 10 bungeni, wakachanga 2,000,000 kila moja utaona wazi kwamba wanaweza pata 20,000,000 kwa mwezi kwa ajili ya kusaidia jimbo moja la Chadema. Lakini sioni tofauti kati ya yale wafanyayo CCM na CDM. Wote wanachukua mapesa kujaza matumbo yao, wanachukua ma-VX, posho za vikao nk.

Tutawaamini vipi Chadema kama kweli wanataka kuwaletea watanzania mabadiliko iwapo nao wanatenda yaleyale wanayoyapigia kelele majukwaani?. Kweli tuna upinzani wa kisiasa Tanzania?, kwa mtazamo wangu naona mpinzani wa kweli bado hajazaliwa Tanzania.

Inakatisha tamaa

Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha
 
kusema watanzania waliopigika zaidi ndiyo wanaoipenda CDM ni kutowatendea haki wananchi, lakini kusema mpinzani wa CCM bado hajazaliwa ni tusi kubwa sana kwa watanzania na hasa sisi ambao tumepigika na hatuna vyama, sasa tufanye nini wanaJF, mimi nashauri tusimkashifu huyu jamaa, ila tumuelimishe. sasa ndugu yangu kama wewe unapenda kupata kura nyingi zaidi kwenye uchaguzi, njia nzuri ni kutushawishi sisi tusio na vyama na wale walio vyama vingine ili wakupigie kura sio kutoa maneno ya matusi kwa watanzania wengi, kwa kufanya hivyo huwasaidii CCM badala yake unawaweka pabaya zaidi si ndiyo ndugu yangu, lakini pia unajenga chuki ya watanzania zidi ya CCM jambo ambalo kwa maoni yangu naona halijakaa vizuri.
 
Ka vipi 2015 usipige kura kama huoni chama cha kukipa kura yako. Tuachie sisi tulikwisha fanya maamuzi.
 
Inakatisha tamaa sana, japo sitaki
Kuamini sana maneno yote uliyoandika kwamtazamo wako, ila
Kuna ka Ukweli kananyemelea, naanza kuona
Ukombozi umeanza
Kufikia , ila
Bado naamini kidogo kwa sasa kuwa chadema wakijipanga wanaweza

Tukubaliane kutokukubaliana inatoooosha

Nimekupata vyema mkuu. Nami naomba tukubaliane kutokukubaliana katika hili suala.

Ila angalia na soma tena nilichoandika. CCM na CHADEMA wote ni sawa.
 
kusema watanzania waliopigika zaidi ndiyo wanaoipenda CDM ni kutowatendea haki wananchi, lakini kusema mpinzani wa CCM bado hajazaliwa ni tusi kubwa sana kwa watanzania na hasa sisi ambao tumepigika na hatuna vyama, sasa tufanye nini wanaJF, mimi nashauri tusimkashifu huyu jamaa, ila tumuelimishe. sasa ndugu yangu kama wewe unapenda kupata kura nyingi zaidi kwenye uchaguzi, njia nzuri ni kutushawishi sisi tusio na vyama na wale walio vyama vingine ili wakupigie kura sio kutoa maneno ya matusi kwa watanzania wengi, kwa kufanya hivyo huwasaidii CCM badala yake unawaweka pabaya zaidi si ndiyo ndugu yangu, lakini pia unajenga chuki ya watanzania zidi ya CCM jambo ambalo kwa maoni yangu naona halijakaa vizuri.

Mimi ni mtanzania na sina chama cha siasa ninachokipenda kwa sasa.
Kama kusema ukweli ninajenga chuki ya watanzania zidi ya CCM basi ni bora nijenge hiyo chuki lakini ukweli nitausema. Sitaki na wala siupendi unafiki.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom