Allen Kilewella
JF-Expert Member
- Sep 30, 2011
- 18,305
- 33,924
Ninaposema CHADEMA, hapa namaanisha viongozi wenye dhamana ya kuzungumza kwa niaba ya wanachama wenzao, kwa maana nyingine wao ndiyo chama na wanaposema wao chama huwa kinakuwa kimesema. CHADEMA kila mara hujiweka kwenye kujihami badala ya kushambulia.
Kwa mfano mpaka sasa wapinzani wa CHADEMA wamefanikiwa kuwaaminsha watu kwamba CHADEMA ni chama kinachodhibitiwa na Wakristu na watu Kaskazini. Lakini wakati inashutumiwa hivyo, CCM inashutumiwa asilimia zaidi ya 60 Makatibu wa CCM walikuwa ni waislamu lakini CCM haikuitwa ni chama cha Waislamu!
Wakati huu ambapo CHADEMA inaitwa ya "kikanda" Mwenyekiti wa CCM na Rais wa Jamhuri ya Muungano ameteua watu wengi toka Kanda ya Ziwa na mikoa ya Jirani lakini CCM haiitwi ya Kikanda wala Magufuli hasemwi kuwa anateu watu wa "kwao" kama ambavyo inasemwa kwa Mbowe kuhusu CHADEMA na Uchaga.
Tatizo la CHADEMA ni kwamba wao huchukulia vitu vinavyoharibu chama kama ni vitu "vitu vidogo" kwa hivyo hawajishughulishi navyo. Leo mtu akiwa ni mchaga anataka kugombea nafasi ya uongozi wa chama huko mtwara anashindwa kugombea kwa kuwa itaonekana kwamba wachaga wanapandikiza watu wao kila sehemu ya nchi. Viongozi wanafanyaje kuondoa hizi propaganda kwamba bila kuwa mchaga au mtu wa kaskazini huwezi kuwa kiongozi ndani ya CHADEMA?
Wakati watu wa Kaskazini waliopo CCM wanaweza kuwa viongozi mahala popote ndani ya Tanzania, CHADEMA mtu ukiwa wa Kaskazini na ukiwa kiongozi nje ya mikoa ya kaskazini inajengwa picha na CCM kwamba CHADEMA ni ya watu wa Kaskazini na viongozi wa CHADEMA wanabaki wameduwaa hawana la kufanya! Ni lini CHADEMA itatoka na kuwaambia watu kwamba nchi hii mtu anaweza kuwa kiongozi wa chama cha siasa mahala popote bila ya kujali asili wala dini yake?
Ukiangalia suala la Ben Saanane, Mikutano ya hadhara, kufukuzwa Bungeni, CHADEMA siku zote huamini kwamba wananchi "wataelewa tu" kwamba CCM ni chama kibaya bila ya kufanya juhudi za kuonesha kwamba CCM ni chama kibaya na mabaya ya watanzania chanzo chake ni CCM!