CHADEMA, acheni kurandaranda mijini,nendeni kwa wapiga kura vijijini.

mwanakidagu

JF-Expert Member
Jan 24, 2012
208
78
Wananchi wanakiu ,wako tayari kwa mabadiliko lakini wanasiasa na vyama vyao yaelekea hawako tayari kwa. mabadiliko ya kweli,na uongozi tofauti na huu wa ccm uliopo.achilia mbali vyama vingine vya siasa ,ngoja niseme kuhusu CHADEMA,kimebaki kiki randa randa mijini tu huku kiki tambua kura zipo vijijini.

huenda chama hiki hakina nia ya dhati kwa ukombozi wa mtanzania.ukiwatazama kwa undani utadhani wana nia ya dhati ya kupatia wananchi uongozi mpya.

mfano wa mambo haya ni kuwa hawaendi vijijini.huko ndiko kura zilipo lukuki kwa wananchi wa maeneo hayo.

Utasikia doct katikisa jiji la mwanza,mbowe kafunika mbeya ,sumbawanga,iringa ama shinyanga na nk.kamwe mkakati huu wa kwenda vijijini naanza kuona kama vile unachelewa sasa.

sisi wapiga kura tuna jiuliza safari za mwenye kiti wa taifa wa cdm kwenda ikulu na mazungumzo ya siri yalilenga nini?

Mbona hakuna msukumo wa moja kwa moja kwa viongozi hawa toka mioyoni mwao kuhusu kupambana na mkoloni huyu mweusi?,HUKO MIJINI MMEWAELEWA,SASA NENDENI VIJIJINI,WAMEMWACHA ALIFONCE MAWAZO PEKEE ANAKATA MBUGA KWENDA VIJIJINI.

kama chadema kina tudanganya mwisho wa siku kiseme ,tujipange upya kwa 2015.u wapi mkazo na kutembelewa wanakijiji,SASA uchaguzi wa 2014,wa serikali za mitaa umefika.na huo mkuu u puani tu.KAMA CDM HAINA NIA HIYO ISEME MAPEMA ILI SISI TUCHAGUE HATA JIWE,KULIKO KUENDEKEZA UONGOZI WA ccm,na madhambi yao.
 
Nchi nikubwasana ndio mana viongozi makini tofauti na wale wanaoenda kusinzia bungeni kanakwamba hawana pakulala wameona kunaumhimu kuweka mkakati wa majimbo ili kurahisisha utendaji,maendeleo na kukufikia haraka na chama kina taratibuzake labda kama haujafikiwa na M4c subiri usichoke wapo jirani sana!
 
......

These guys prefer to go where they can make money through BAKULI. Unategemea wafanye mikutano vijijini ambapo hawezi kuchangisha fedha?
 
muda haurudi nyuma tusije sema tumechelewa

Tatizo la wanasiasa wetu wanafikiri watashinda kwa propaganda badala ya kuwafikia wananchi na kuwaambia nini watawafanyia. CHADEMA na sera yao ya kukusanya fedha kwenye mikutano ya hadhara sidhani kama wakifika vijijini na sera yao hii watavumiliwa.
 
Hoja yako ni nzuri mkuu! Nakuunga mkono. Tunataka kuona baada ya kila kanda kuzunduliwa tusikie kuwa kila kata na kijiji kimefikiwa na CDM! Ni lazima kutengeneza mtaji wa uhakika wa watakaochagua CDM ktk uchaguzi wa serikali za mitaa mwakani na Uchaguzi mkuu 2015. Hawa wanapatikana vijijini. Moja ya makosa aliyofanya Raila kule Kenya ni kutokutengeneza watu wa uhakika kisayansi sio ki fikra, watakaomchagua siku ya uchaguzi. Kifikra alikuwa anaonekena kukubalika na wakenya wengi lakini kisayansi ilikuwa si hivyo. Kama tukiproject kuwa watakaojiandikisha kupiga kura ni milioni 20 kwa mfano, lazima tuhakikisha kuwa tunao wanachama at least milioni 12 ambao tuna hakika kuwa watachagua CDM. CDM kitumie mwanya huu wa kukubalika mijini kufikia vijiji kwa kuwa mwanya huo hautakuwepo siku zote. Kila Kanda iweke mkakati wa kufikia kila jimbo na kata na kijiji kwa wakati huu. Time is not our ally. Tufanye kisayansi tusije kushtukizwa kama Raila na kushangaa! Oh, too late!
 
hoja yako kaka hujafanyia utafiti kabisa, hebu jaribu kufuatilia habari then after like 2months utajua ukweli upo wapi mukuu...!
in short inatakiwa kabla ya kuweka mada jamvini you have to think big na kuwa na info za kutoshamdau...!
 
Kimsingi kila chama kina utaratibu wake wa kujieneza, ikiwa unaona utaratibu unaoutoa humu jamvini utakisaidia chama basi ukawape ushauri huo na wewe uwe mstari wa mbele kuonyesha mfano kwani kuwa kiongozi si kutumikiwa bali kutumika na kuonyesha njia.
 
Nchi nikubwasana ndio mana viongozi makini tofauti na wale wanaoenda kusinzia bungeni kanakwamba hawana pakulala wameona kunaumhimu kuweka mkakati wa majimbo ili kurahisisha utendaji,maendeleo na kukufikia haraka na chama kina taratibuzake labda kama haujafikiwa na M4c subiri usichoke wapo jirani sana!

.......

Mkuu mbona uko nje kabisa ya mada, sera ya majimbo inazuia kuwafikia watu waliko vijjijini?
 
Kimsingi kila chama kina utaratibu wake wa kujieneza, ikiwa unaona utaratibu unaoutoa humu jamvini utakisaidia chama basi ukawape ushauri huo na wewe uwe mstari wa mbele kuonyesha mfano kwani kuwa kiongozi si kutumikiwa bali kutumika na kuonyesha njia.

Siyo kila anayetoa maoni na awe kiongozi , huu ni umafia ya mawazo, ametoa ushauri na siyo lazima awe mfuasi wa CDM, wasipoufanyia kazi haimhusu basi hawalazimishwi
 
Ungekuwa unafuatilia ungejua kuwa kuna Makamanda kama Alphonsi Mawazo wako visiwani huko ziwa victoria wanatoa elimu hadi watu wanalia. Pia makamanda kama Benson Kigaila wanaingia sana pori kwa pori. Kwa kuwa wewe unapoenda kufuatilia mambo yanayokufurahisha na ambayo yanatangazwa sana umejikuta unafuatilia Mbowe na Doctor.

Pia ukiwa kama mtu unayeelewa demokrasia ya vyama vingi na unataka mabadiliko katika nchi yako, tumia fursa hii kuwaelimisha jamii inayokuzunguka na sio kusubiri hadi Mbowe aje
 
These guys prefer to go where they can make money through BAKULI. Unategemea wafanye mikutano vijijini ambapo hawezi kuchangisha fedha?
ccm imeuza utu wa mtanzania kwa wageni kwa bei ya kutupa!unajua kuna wahindi wanamiliki vijiji na hati wanazo za ekari 4000-20000 kisa kuipa ccm pesa nyakati za uchaguzi?
 
Wana-CCM acheni kurandaranda mijini na kuruka mi-pipa kwenda kutafuna pizza katika nchi za watu Ughaibuni, e nendeni mkaokoe chama chenu kule kwa wananchi vijijini.
 
Nakuunga mkono mkuu,tatizo la chadema maneno na mikakati mingi kuliko matendo, vijijini ndo kuna asilimia kubwa ya wapiga kura,lakini kina freeman wanaishia mjini tu,halafu maneno 2015 tunashika dola, hizi ni ndoto za kulala masikini kuamka tajiri!
 
Unaposema waendevijijini unamaanisha wapi,sio huko alipo kamanda mawazo?au unadhani Cdm ni Freman Mbowe na Silaa tu?unataka viongozi wote waishie huko bila utaratibu? nadhani kaziya ukombozi asiachiwe Mbowe tu nawewe unajukumu lakueneza sera za Cdm ulipo
 
Wewe ni mmoja kati ya wa ajabu sana, unataka na kusubiri sana ukombozi utokee hata kesho.....lakini umeweka kalio tu nyumbani unataka Mbowe/Slaa akufanyie kila kitu.......wameona wawafate mpaka vilabuni kwa kuanzisha kanda.....lakini bado unalaumu......wenye mioyo ya dhati wamejitolea wapo vijijini wanapiga harakati ambazo wewe unasubiri ufanyie

Hapa ni juzi kati huko Mkalama....tena ''kukaaa munumba kabisa''
601427_342961595823500_750167716_n.jpg 528292_342967665822893_850055747_n.jpg
 
Tatizo la wanasiasa wetu wanafikiri watashinda kwa propaganda badala ya kuwafikia wananchi na kuwaambia nini watawafanyia. CHADEMA na sera yao ya kukusanya fedha kwenye mikutano ya hadhara sidhani kama wakifika vijijini na sera yao hii watavumiliwa.

Wanawake wengine bwana badala ya kuongelea maendeleo unakazania kugombea mabwana,Hivi wewe jichola3 umekuwa hauna point zaidi ya kukebehi Chadema,sawa wanachangishana kuonyesha wana uchungu na ukombozi wa nchi yao je Ccm ambao wao ni ufisadi tu hadi kufanya maisha yanakuwa magumu,wanawanyonya wananchi masikini wa Tanzania kwa ikataba kandamizi wanaiba kila kitu nchii hii unaona wivu wapenda maendeleo wakichangishana kwa ajili ya kununua mafuta? Unafikiria kwa kutumia makalio kweli wewe,mbona ya ccm hamuyasemi? Ndio taabu ya kuwa na wanajiita wasomi uchwara wakati shida ni kuganga njaa tu na kushinda kwenye laptop kila siku ajili ya kupewa posho na Mwigulu mwisho atataka mumpe,,,,,,,,,
 
Back
Top Bottom