Celtel = Zain Why???

Ndugu,hawa watu ukianza kushindana nao hutafika mahali!Wanaandika tuu yale wanayoyafikiria na kusikia huko mitaani ila waambie waseme wanayoyajua ama kutoa data!Watapotea hata hutajua walipopotelea![/QUOTE]


...Inawezekana, mkuu! But how about labda wanafanya hivyo kuepuka arguing with a fool because people might just not notice the difference??? teh teh.
 
Nimekuwa nikijiuliza nini maana ya kubadili badili majina ya makampuni makubwa kama vile, SHERATON iligeuka kuwa ROYAL PALM na sasa MOVENPICK. Pia makampuni ya simu kama Mobitel ikageuka kuwa tiGO. Lakini hili la sasa la kampuni ya simu celtel kuwa ZAIN limenifumbua macho. Nimejiuliza huku na kule mwisho nikapata jibu kwamba, kila kampuni hupewa kitu kinaitwa "Tax Holiday" ambapo mkataba huwa miaka mitano mitano ambapo kampuni husika huwa haipaswi kulipa kodi yoyote. Kwa hiyo hzinduzi wa makampuni haya kwa kubadilisha majina nimeona ni mzigo kwa jamii, kuna ufisadi mkubwa unafanywa, wananchi tumechoka, hatutaki.


japo sina uhakika na kinachoendelea zain, hili la kubadilisha majina kwa ajili ya kukwepa kodi ni ufisadi unaotumika. hali hii nimeiona hata botswana.
 
Hayo ni mawazo ya nyinyi msiojua biashara za kisasa.ni mambo ya kawaida watu kuuza na kununua makampuni makubwa hivyo kupelekea kubadili majina.
 
Ila binafsi hili jina la "Zain" linanibore sana...halijakaa kibiashara...wangemalizia tu kama ni Zainab tujue. Halafu hiyo mirangi yao Black, sijui light blue, dark pink...haiendi haiendi...please....
sijui kama ni kweli lakini nasikia kibosile mwenye mali ana binti anaitwa zainab akaona bora amuenzi,mambo ya fedha hayo.na sisi tuanzishe mobile kampuni yetu tuiite 'kalumanzilatel'!
 
sijui kama ni kweli lakini nasikia kibosile mwenye mali ana binti anaitwa zainab akaona bora amuenzi,mambo ya fedha hayo.na sisi tuanzishe mobile kampuni yetu tuiite 'kalumanzilatel'!
Haya ni maneno ya mitaani kabisa aisee.Fungua mtandao usome Zain ni nini .Hii ni kampuni ya simu iko Kuwait kwa miaka mingi sana.
 
Kwa mianya tunayowapa wawekezaji, Tanzania imekuwa kama kichwa cha mwendawazimu - kila kinyozi mmh. Ona sasa hata JF inatumiwa kama PR ya Zain. Waarabu wanaujua utajiri wa Tanzania na wanajua ulafi (ujinga?) wetu - wanachotanguliza ni kuingiza mguu tu kwanza halafu shingo na kumalizia mwili mzima mwishowe twajikuta nje nje. Tax holiday tunayotoa ni ya pekee na inatosha kabisa kuwafanya wabadilishe jina.

Kibiashara kubadilisha jina holela si busara na ndiyo maana kwa wenzetu majina yalioyoanzishwa karne zilizopita bado zinashamiri hata kampuni ikiuzwa. Hapa Tz majina hubadilishwa kama mashati - ndio utamaduni wetu. Na kama kwa kufanya hivi kuna unafuu km. tax holiday, why not ?

Get my point mkuu....
22 countries na ukilinganisha customer base utakuta Celtel Tz wana base ndogo kulinganisha na nchi zingine. I doubt if they changed their name bcoz of tax holiday from Tanzania.
Celtel was quite a strong brand in averyway so we need to know why!!! was it for Tanzania or for the zainab world???
 
Back
Top Bottom