ntamaholo
JF-Expert Member
- Aug 30, 2011
- 12,956
- 7,005
![]()
Leo ni marudio mechi ya makundi kati ya Walias na Kilimanjaro stars tofauti kwa sasa itafanyika kwenye hatua ya robo fainali badala ya makundi. Kilimanjaro stars inaingia robo fainali baada ya kuongoza kundi A wakati Ethiopia ilibidi wasubiri huruma ya 'Best looser' ili kuweza kuvuka.
Ethiopia anaingia mechi ya leo akiwa ameshikilia karata ya uenyeji wa mashindano na waswahili wanasema mtu kwao, akiwa na mashabaki lukuki na umuhimu wa yeye kubaki kuyapa uhai mashindano. Timu zote zimeshawasili uwanjani, tuwe sote kujuzana yatakayojiri uwanjani.
*Mechi saa tisa na nusu mchana na inarushwa kupitia DSTV na channel za SS 5 na SS 9 East
================
00' Refa amepuliza kipenga kuashiria mwanzo wa mechi
01' Kilimanjaro wanapata faulo ya mapema baada ya Kaseke kuangushwa japo haijazaa matunda
07' Ndemla anakosa goli la kuongoza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Bocco
24 :A S soccer:Goaaaal, John Bocco anatia wavuni goli la kwanza kwa mpira wa kichwa baada ya kupiga mpira kutoka kona
32' Mchezaji wa Ethiopia yuko chini baada ya kukimbizana na Himid Mao
34' Ethiopia wanakosa goli la kusawazisha baada ya shuti kali kugonga mwamba wa juu
41' Bocco anakosa goli zuri baada ya kubaki na mlinda mlango, mabeki wa Ethiopia walifikiri ameotea
45+1' Kaseke anakosa goli yeye na lango baada ya kipa kutoka golini
45+2' Mpira ni mapumziko
45' Mpira umerejea baada ya mapumziko
mkuu, mode wameziunga post. hvyo updates za leo ziwekee heading kubwa, tarehe, uwanja na muda then uanze kutupa updates