CECAFA Robo Fainali: Ethiopia Vs Tanzania Bara

Casuist

JF-Expert Member
Jul 23, 2014
1,179
2,940




Leo ni marudio mechi ya makundi kati ya Walias na Kilimanjaro stars tofauti kwa sasa itafanyika kwenye hatua ya robo fainali badala ya makundi. Kilimanjaro stars inaingia robo fainali baada ya kuongoza kundi A wakati Ethiopia ilibidi wasubiri huruma ya 'Best looser' ili kuweza kuvuka.

Ethiopia anaingia mechi ya leo akiwa ameshikilia karata ya uenyeji wa mashindano na waswahili wanasema mtu kwao, akiwa na mashabaki lukuki na umuhimu wa yeye kubaki kuyapa uhai mashindano. Timu zote zimeshawasili uwanjani, tuwe sote kujuzana yatakayojiri uwanjani.

*Mechi saa tisa na nusu mchana na inarushwa kupitia DSTV na channel za SS 5 na SS 9 East
================
00' Refa amepuliza kipenga kuashiria mwanzo wa mechi
01' Kilimanjaro wanapata faulo ya mapema baada ya Kaseke kuangushwa japo haijazaa matunda
07' Ndemla anakosa goli la kuongoza baada ya kupokea pasi nzuri kutoka kwa Bocco
24 :A S soccer:Goaaaal, John Bocco anatia wavuni goli la kwanza kwa mpira wa kichwa baada ya kupiga mpira kutoka kona
32' Mchezaji wa Ethiopia yuko chini baada ya kukimbizana na Himid Mao
34' Ethiopia wanakosa goli la kusawazisha baada ya shuti kali kugonga mwamba wa juu
41' Bocco anakosa goli zuri baada ya kubaki na mlinda mlango, mabeki wa Ethiopia walifikiri ameotea
45+1' Kaseke anakosa goli yeye na lango baada ya kipa kutoka golini
45+2' Mpira ni mapumziko

45' Mpira umerejea baada ya mapumziko
52' Kilimanjaro wanakosa goli baada ya Msuva kupiga shuri na kupanguliwa na golikipa
54' Penati, Yondani anapewa kadi ya njano baada ya kucheza ndivyo sivyo eneo la hatari
56' :A S soccer:Goaaaal, Penati inazaa matunda, Tanzania bara 1-1 Ethiopia
62' Ndemla anakosa goli baada ya kupiga shuti kali sana golini
64' Tanzania wanapata kona pacha japo zote hazijazaa matunda
65' Malimi Busungu anaingia kuchukua nafasi ya Kaseke
68' Faulo kuelea Ethiopia baada ya Bocco kuchezewa mpira usio wa kiungwana, mpira wa faulo ulitoka nje
76' Bocco anakosa goli baada ya kupiga shuti golini ambalo kipa aliliweka mikononi
90' Mpira umeongezewa dakika tatu
90+1 Ethiopia wanafanya mabadiliko ya wachezaji
90+3' Kipenga kimepulizwa kuashiria mwisho wa mchezo, Tanzania 1-1 Ethiopia

MPIRA UNAAMULIWA KWA MATUTA
1 Tanzania wanakosa penati
1 :A S soccer:Ethiopia wanatingisha nyavu
2 :A S soccer:Mao anafunga penati ya kwanza kwa Tanzania
2 :A S soccer:Ethiopia wanaandika penati ya pili Tanzania 1-2 Ethiopia
3 :A S soccer:Bocco anatumbukiza golini
3 :A S soccer:Ethiopia wamekosa, Tanazania 2-2
4 :A S soccer:Goal, Tanzania wanatumbukiza goli
4 :A S soccer:Goal kwa Ethiopia
5 Tanzania wanakosa goli, Ethiopia wanasonga mbele na Tanzania safari inaishia hapa
 
Last edited by a moderator:
Safi sana JB tunawategemea sana vijana wetu huko kwa wahabeshiiiii
 
Hivi tunayo wakosa hawa wahabeshi sijui ila tungekuwa na bao kama nne hivi.
 
Mbona post ya tar 28.nov? Au mm network zimekata kichwani? Bcoz what I know is leo ni tar 30.nov
 
mwishiwe unashangaa kili 1-ethiopia2

halaf tunaanza kulalamika tumewakosa

badala kumaliza gem mapema kama algeria
 
Back
Top Bottom