CECAFA Kagame Cup 2014, Rwanda

CECAFA Kagame Cup 2014, Rwanda

inasikitisha inahuzunisha cecafa wanapo andaa kufanyika nchi fulani mashindano viongozi wa chama cha mpira cha husika wanakuwa kama watumwa wanazurura kwenye makampuni kutafuta udhamini.
musonye huja kusaini tu na kutangaza na ndio maana nchi ambazo hazina makampuni hushindwa kuandaa mashinfano hayo kama Zanzibar
 
Tatizo la Azam strikers wao walishindwa kutumia vizuri nafasi walizopata ,hapa TZ tunatatizo la washambuliaji ugonjwa huu sijiu lini utapona
 
CECAFA ikiwa na watu kama Musonye haiwezi kupata wadhamini wa maana. Lazima aondoke ili iendeshwe kisasa zaidi. Yeye anawaza hela za mlangoni mpaka leo.
 
CECAFA ikiwa na watu kama Musonye haiwezi kupata wadhamini wa maana. Lazima aondoke ili iendeshwe kisasa zaidi. Yeye anawaza hela za mlangoni mpaka leo.

Musonye ni mtu mfu hata kama anapumua, RIP Musonye.
 
cecafa ikiwa na watu kama musonye haiwezi kupata wadhamini wa maana. Lazima aondoke ili iendeshwe kisasa zaidi. Yeye anawaza hela za mlangoni mpaka leo.
nani anasema kwamba afrika inajitawala ? Watu kama musoye bado wanatutawala akili zetu , kwani vijana hawana haki kuonyesha vipaji vyao ?both sides are wrong yanga and cecafa ,lakini kuwanyima haki vijana wa yanga ni mbaya zaidi .
 
cecafa ni tasisi ya musonye ya kujipatia lizki ya mkono kinywani.
hebu angalia utaratibu wake ni timu za kuokotaokota kwa mfano somalia sijawasikia kuna ligi au bingwa wa somalia ni vijana wa kutoka swedeni ungereza wanaungana na kutoka kenya wanabadilisha majina tu.
cha ajabu watanzani unasikia eti mashindano makubwa ukanda huu.angalieni utaratibu wa kupata wawakilishi kama BINGWA AFRICA UEFA na nyonginezo fananisha na CECAFA
 
pale kigali mwaka huu yamepoa sana. nimeamini tz mpira unapendwa watu huwa wanajaa, lakini huko kwingine naona viti vitupu vingi sana. labda jana tu wakati APR na ATLETICO wanacheza.
 
IMG_20140810_165241_0.jpg Hawa UKWELI na UHAKIKA ni kweli mashindano haya ni ya nchi TANO tu? Mbona bendera ya Zanzibar haipo hapo?
 
11_1.jpg






AZAM
FC imeanza kwa sare ya bila kufungana na wenyeji Rayon katika mchezo wa ufunguzi Klabu Bingwa AfrikaMashariki na Kati, CECAFA Kagame Uwanja wa Amahoro, Kigali, Rwanda.


Azam ilicheza vizuri na bahati haikuwa yao tu hawakuweza kupata mabao na nafasi ambayo wataikumbuka zaidi niya mapema tu sekunde ya 24, shuti la Himid Mao ‘Ninja' lilipogonga mwamba na kwenda nje.


Pamoja na kwamba walicheza nyumbani, lakini Rayon walifurahia sare na mabingwa hao wa Bara, kwani walikuwakwenye hatari ya kupoteza mchezo.


Kikosi cha Azam FC kilikuwa; Mwadini Ali, Shomary Kapombe, Gardiel Michael, David Mwantika, Aggrey Morris, KipreBalou, Himid Mao/Mudathir Yahya dk89, Salum Abubakar ‘Sure Boy', John Bocco ‘Adebayor', Kipre Tchetche naKhamis Mcha ‘Vialli'/Didier Kavumbangu dk70.
Rayon Sport; Bikorimana Gerard, Ndayisenga Fuad, Nizigiyimana Karim, Sibomana Bakari, Serugendo Arafat,Tubane James, Leon Uwumbazimana/Hategekimana Aparodis dk67, Sibomana Hussein, Ndatimana Roberts, YossaBetrand/Sekle Zico dk88 na Motombo Govin/Kambala Salita dk78.

Kutoka Tovuti ya AzamFC
 
pale kigali mwaka huu yamepoa sana. nimeamini tz mpira unapendwa watu huwa wanajaa, lakini huko kwingine naona viti vitupu vingi sana. labda jana tu wakati APR na ATLETICO wanacheza.
Kuna mwaka mashindano yaliwahi kuchezwa miaka kadhaa mfululizo hapa Darisalama, kwetu kuna hamasa kuliko popote katika kanda huu.
 
Kuna mwaka mashindano yaliwahi kuchezwa miaka kadhaa mfululizo hapa Darisalama, kwetu kuna hamasa kuliko popote katika kanda huu.

Ndugu Rugby Union
Ingekuwa vema kama ungeweka match results hapo juu kabisa, kama update ya post yako ya kwanza. Najua kila siku mechi zinachezwa.
 
Back
Top Bottom