CDM mwanza bado kwawaka moto | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CDM mwanza bado kwawaka moto

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by WOWOWO, Sep 24, 2012.

 1. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #1
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Katika Kipindi cha Tuongee Magazeti cha Star TV Alfajiri hii kuna habari ya Makada wa CDM katika Wilaya ya Ilemela kutwangana makonde wakati wakiwa kwenye kikao cha kamati ya utendaji ya wilaya hiyo. Katika patashika hilo inasemekana Mbunge wa Ilemela Kiwia alijificha chini ya meza ili kukwepa makonde hayo.

  My Take: Hili fukuto la CDM Mwanza linahitaji tiba ya kudumu. Nadhani kuna tatizo kubwa hapa.

  Note: Source ya habari hii ni Gazeti la Mtanzania la Leo Sept.24,2012
   
 2. KOMBAJR

  KOMBAJR JF-Expert Member

  #2
  Sep 24, 2012
  Joined: Nov 15, 2011
  Messages: 5,848
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 135
  Endelea kupumu is one way of killing strees!:rockon:timesUp!
   
 3. Capt Tamar

  Capt Tamar JF-Expert Member

  #3
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 15, 2011
  Messages: 6,663
  Likes Received: 3,317
  Trophy Points: 280
  Yes watwangane kabisa!!kama sababu ya kutwangana ni maslahi ya taifa,hao wenzao wamechekeana kwa more than 50yrs,na matokeo yake tunayaona!!anayekwamisha maendeleo ni bora apate bakora!safi sana,ila kama mnagombea kugawana mtakutana na nguvu ya umma.
   
 4. R

  Ramso5 Member

  #4
  Sep 24, 2012
  Joined: Dec 13, 2011
  Messages: 63
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Hawakutwangana bali viongozi wa chadema wakiwa na mbunge wa ilemela ktk kikao.ghafla walivamiwa na kundi la vijana wapatao 100 na kuwafanyia fujo kwani viögozi hao wamekiuka amri halali ya mahakama inayomruhusu Henry matata kujishughulisha na masuala ya chama.wiki iliyopita matata alinukuliwa na vyombo mbali mbali akijitapa kuwa wakimwengua kugombea umeya hawatafanikiwa,atawavuruga kwani atawatumia vijana wake wanaofanya kazi kutoka kwenye meli zake ambao ni wengi na hatimaye kweli yaliyotamkwa yametimia rasmi
   
 5. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #5
  Sep 24, 2012
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Wenzetu kenya walitwangana hata kwa viti ndo maana wametupita mbali sana! twanganeni bana tupate maendeleo
   
 6. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #6
  Sep 24, 2012
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  WOWOWO kumbuka wagombanao ndio wapatanao. Ni heri watu wanazungumza hadi kufikia kupigana kuliko wale wanaokubali kila kitu kwa hofu ya kunyamazishwa endapo watafungua mdomo
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 7. Ritz

  Ritz JF-Expert Member

  #7
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 42,252
  Likes Received: 4,674
  Trophy Points: 280
  Kisa cha kupigana ni nini.
   
 8. Daffi

  Daffi JF-Expert Member

  #8
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 25, 2011
  Messages: 3,803
  Likes Received: 178
  Trophy Points: 160
  Gazeti la uhuru nayo unaliamini?!cdhan km kuna ukweli wowote.
   
 9. Mzalendo JR

  Mzalendo JR JF-Expert Member

  #9
  Sep 24, 2012
  Joined: Jun 6, 2012
  Messages: 1,189
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160
  THUMB UP!apo kutakua na kibaraka a.k.a paka mweusi
   
 10. B

  Ba'mdgo JF-Expert Member

  #10
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 17, 2012
  Messages: 230
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  mkuu ukutuambia sababu ni nini aswaa
   
 11. by default

  by default JF-Expert Member

  #11
  Sep 24, 2012
  Joined: Jul 11, 2011
  Messages: 843
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  nguvu ziliwazidia
   
 12. Marire

  Marire JF-Expert Member

  #12
  Sep 24, 2012
  Joined: May 1, 2012
  Messages: 11,420
  Likes Received: 260
  Trophy Points: 180
  sababu ni MATATA ameanza matata yake ,na bado chabulani hajaja na jeshi lake
   
 13. Filipo

  Filipo JF-Expert Member

  #13
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2011
  Messages: 9,329
  Likes Received: 210
  Trophy Points: 160
  I hope unauliza kwa nia njema!
   
 14. Tumaini Makene

  Tumaini Makene Verified User

  #14
  Sep 24, 2012
  Joined: Jan 6, 2012
  Messages: 2,617
  Likes Received: 291
  Trophy Points: 180
  Sina hakika sana na source uliyonukuu. Wengine tumesikia na kusoma habari ya namna hiyo hiyo Gazeti la Habari Leo. Nway taarifa zinafanyiwa kazi mkuu ili kuthibitisha ukweli na uhalisia wake. The ctuation in Mwanza like anywhere else kwa chochote au lolote lile linalohusu maendeleo ya watu hasa kuhusu tumaini lao katika kusaka uhuru na mabadiliko ya kweli, kimfumo na kiutawala, is under very under very serious watch. Ofcourse masuala yote yanafanyiwa kazi kwa mujibu wa katiba, kanuni, miongozo na utaratibu, kama ilivyo kawaida ya CHADEMA. Kwa kuanzia ngazi ya chini husika. Lakini kama ambavyo wameshindwa kila mahali, wenye hila hizo hawatapenya, it is about people's life and destiny. They can't just play with.

  Unajua mambo mengine ni ya ajabu sana na wanaoyafanya wanachekesha kweli...kama watu wanajua kuwa kuwa mwanachama wa CHADEMA kwa sasa ni heshima kubwa katika jamii ya watu waelewa, sasa kwa nini wanapopata dhamana za uongozi hawataki kutumikia watu badala yake wanatumikia matumbo yao. Kama watu wanafikiri kupata umeya wa Mwanza kupata CHADEMA kuna maana kubwa, kwa nini wameshindwa kuonesha uadilifu hadi wanakiri kula rushwa hadharani.
   
 15. nyabhingi

  nyabhingi JF-Expert Member

  #15
  Sep 24, 2012
  Joined: Oct 12, 2010
  Messages: 10,898
  Likes Received: 5,360
  Trophy Points: 280
  mkuu nccr kabla ya kuwa ccm c walianza kutwangana makonde hivihivi kule tanga,.wadhibitini wahuni ndani ya chama
   
 16. n

  nyangasese Senior Member

  #16
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 21, 2011
  Messages: 129
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 33
  Acha uzushi cdm mwanza iko imara na inakubalika kupita maelezo hata ccm hilo wanalijua na wanachokifanya ccm ni kuihujumu cdm na kuichafua kupitia mamluki waliowaandaa.Habari ya unachosema cdm wavurugana nimeisikia asubuhi ya leo kupitia metro fm ambapo diwani Adamu chagulani alikuwa akihojiwa na kusema kuwa kulikuwa na vikao vya uteuzi kwa wagombea wa umeya cdm kwa nyamagana na ilemela,kwao nyamagana uteuzi ulienda vizuri kwa kuwa yeye hagombei.lakini kwa ilemela,Chagulani amesema kuwa matata ana amri ya mahakama inayomruhusu kugombea umeya na amewalaumu viongozi kukaidi amri ya mahakama.hapa cha kujiuliza ni kuwa amri ya mahakama inahusiana vipi na mtu kuenguliwa kugombea umeya na vikao halali vya chama.na kwa nini matata anaung'ang'ania sana umeya.kwa nini asiridhike na maamuzi ya viongozi wake waliomuengua kugombea umeya
   
 17. sosoliso

  sosoliso JF-Expert Member

  #17
  Sep 24, 2012
  Joined: May 6, 2009
  Messages: 7,519
  Likes Received: 1,857
  Trophy Points: 280
  Ajabu hii.. Jamaa anautaka umeya kwa gharama zote..:nono:
   
 18. t

  thatha JF-Expert Member

  #18
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Chadema wachapana makonde Mwanza
  Jumatatu, Septemba 24, 2012 05:47 Na John Maduhu, Mwanza

  *Vurugu kubwa zaibuka, mkutano wavunjika
  *Mbunge Kiwia ajificha chini ya meza kujinusuru
  KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ilemela jana kilivunjika, baada ya kutokea vurugu kubwa, zilizosababisha wajumbe kutwangana makonde.

  Kikao hicho kilikuwa kikifanyika katika Hoteli ya Ladson iliyopo Bwiru, kwa ajili ya kupitisha majina ya wagombea wa nafasi ya meya na naibu meya wa Manispaa ya Ilemela,

  Hata hivyo askari polisi walifanikiwa kuwasili mapema hotelini hapo na kuwatawanya wajumbe wa kamati ya utendaji pamoja na vijana wa chama hicho, waliokuwa wamevamia kikao hicho.

  Vurugu hizo zilizodumu kwa saa moja na kusababisha kizaazaa hicho, zilizuka baada ya uongozi wa Kamati ya Utendaji wa chama hicho Wilaya ya Ilemela, kukaidi amri ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Mwanza.

  Mahakama hiyo ilikuwa imezuia kufukuzwa uanachama wa aliyekuwa Diwani wa Kata ya Kitangiri, Henry Matata, hadi pale kesi ya msingi itakapomalizika.

  Mahakama hiyo pia iliamuru diwani huyo aendelee kuwania nafasi ya umeya wa Ilemela, ambapo kamati hiyo ilizuia jina la Matata lisiwemo katika majina ya watu wanaogombea nafasi ya umeya.

  Dalili za kuvurugika kwa hali ya amani ilionekana tangu mapema, baada ya Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Ilemela (OCD), Debora Magiligimba, kuwasili katika hoteli hiyo akiwa katika gari lililokuwa limebeba askari polisi.

  Hata hivyo Mwenyekiti wa Kamati hiyo, Yunusu Chilongozi, alisema kikao hicho hakitambui amri hiyo ya mahakama, hivyo hakukuwa na haja ya kumruhusu Matata kuwa miongoni mwa wagombea.

  Pamoja na juhudi za polisi kuwataka viongozi hao kuheshimu amri ya mahakama, viongozi hao walizidi kukaidi, ndipo OCD na askari wake walipoamua kuondoka katika eneo hilo na kuwaacha wanachama pamoja na viongozi wakiendelea kuvutana.

  Muda mfupi baada ya askari kuondoka, kundi kubwa la vijana wa Chadema lilivamia katika ukumbi huo na kuanza kutembeza kichapo kwa wajumbe wa Kamati ya Utendaji, hali iliyosababisha vurugu kubwa.

  Makundi hayo ya vijana ni miongoni mwa wafuasi wa chama hicho wanaopinga kitendo cha diwani huyo na mwenzake wa Kata ya Igoma kuvuliwa uanachama.

  Katika vurugu hizo, Mbunge wa Ilemela, Highness Kiwia (Chadema), aliyekuwa miongoni mwa wajumbe hao, aliamua kujificha chini ya meza kama njia ya kujinusuru.

  Wakati Kiwia akiingia uvunguni mwa meza kujinusuru, baadhi ya wajumbe walikimbia huku na kule na wengine waliamua kujificha chooni, ili kujinusuru.

  Kutokana na vurugu hizo, uongozi wa hoteli hiyo uliamua kupiga simu polisi ambapo kikosi cha polisi wenye silaha na zana nyingine walifika na kuwatawanya vijana hao.

  Akizungumza na Mtanzania baada ya vurugu hiyo, Chilongozi alizidi kusisitiza msimamo wa kamati yake kwamba, hapakuwa na sababu za kuahirisha kikao hicho.

  Chilongozi alifafanua zaidi na kusema kuwa kamati yake iliamua kumzuia Matata kutokana na maelekezo yaliyotolewa na viongozi wa juu kutoka makao makuu ya chama.

  Akizungumza na waandishi wa habari Matata alisema kuwa, kamati hiyo imeonyesha dharau kubwa kwa mahakama na kusema kuwa, wajumbe hao wanapaswa kuchukuliwa hatua ili iwe fundisho.

  "Amri ya mahakama haiwezi kuvunjwa na wahuni wachache kwa manufaa yao, nitapigania haki yangu hadi pale kitakapoeleweka, siwezi kukaa kimya," alisema Matata.

  chsnzo ni gazeti la mtanzania
   
 19. WOWOWO

  WOWOWO JF-Expert Member

  #19
  Sep 24, 2012
  Joined: Aug 3, 2011
  Messages: 582
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Mkuu Makene heshima kwako. Nadhani ungepata nakala ya gazeti la Mtanzania ndiyo uje jamvini. Habari hiyo si nzuri kwa image na credibility ya CDM. Inahitaji ufafanuzi wenu mkuu. I trust you much. Umepikika vema na kuiva
   
 20. t

  thatha JF-Expert Member

  #20
  Sep 24, 2012
  Joined: Apr 29, 2011
  Messages: 15,234
  Likes Received: 179
  Trophy Points: 160
  Wavuti
  CHADEMA Mwanza wakung'utana makonde ya 'chap chap'
  MTANZANIA -- KIKAO cha Kamati ya Utendaji ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) Wilaya ya Ilemela jana kilivunjika, baada ya kutokea vurugu kubwa, zilizosababisha wajumbe kutwangana makonde. Kikao hicho kilikuwa kikifanyika katika Hoteli ya Ladson iliyopo Bwiru, kwa ajili ya kupitisha maj
  source: wavuti.com
  link: Full Article...
   
Loading...