CDM Geita nao watoa Tamko mauaji Arusha

Mongoiwe

JF-Expert Member
Feb 26, 2008
524
263
TAMKO LA CHADEMA - GEITA KULAANI UTUMIAJI WA NGUVU ZA ZIADA KUDHIBITI MAANDAMANO YA TEREHE 05.01.2011 MJINI ARUSHA

Ndugu watanzania na wapenda Amani wote. Uongozi wa Chadema na jumuiya zake, wapenzi wote wa chadema ndani ya mkoa wetu mpya wa Geita tunapenda kuungana na wadau wote ambao wanalaani kitendo cha jeshi la polisi cha kutumia nguvu kupita kiasi kudhibiti maandamano yaliyofanyika tarehe 5 January 2011 mjini Arusha na kusababisha mauaji ya watu, majeraha kwa ndugu zetu wa Arusha na uharibifu wa mali za raia wasio na hatia
Itambulike kwamba kitendo cha polisi kutumia nguvu kilikuwa si cha msingi ili hali nguvu hiyo ingetumika katika kudhibiti wale ambao wangetaka kuleta fujo kwenye maandamano hayo.
Jeshi la polisi kupitia kwa mkuu wake (Inspector General wa Police – IGP) lilitoa tamko la kusitisha maandamano siku moja kabla ya maandamano ya amani kupitia television kwa madai kwamba limepata taarifa za kiintelijensia kwamba kutakuwepo na uvunjifu wa amani. Bila kukokotoa zaidi, jeshi hilo likaona ni vyema kuzuia maandamano. Tulitarajia nguvu itumike kudhibiti viashiria ambavyo vingesababisha amani kuvunjika na badala ya kudhibiti maandamano hayo kwa kufyatua risasi za moto hovyo kuelekea kwa waandamaji kulikosababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi wengine wengi,kupiga watu virungu na kuwasababishia maumivu makali kuharibu mali za watu kwa kupasua vioo vya magari
Jeshi la polisi limekuwa likilalamika kwamba kuna upungufu wa vifaa vya kutendea kazi. Majambazi yamekuwa yakiendelea kuvamia maeneo mbalimbali na kupora mali na kukatisha roho za raia wasio na hatia kwa kisingizio kwamba kuna uhaba wa vitendea kazi. lakini cha kushangaza, hivi majuzi tu tarehe 5, 2011 mji mzima wa Arusha ulikuwa umetanda maaskari wakiwa wako tayari na magari yakipita huku na kule na wengine wakiwa wameshikilia bunduki kwa nia ya kuzuia maandamano.
Wengi mtakuwa mashahidi kwamba jeshi letu linajidhihirisha kuwa makini na hodari katika matukio ambayo wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao wanapokuwa katika harakati za kidemokrasia, kwa mfano siku ya kutangaza matokeo ya ubunge majimbo ya Nyamagana na Ilemela wa tarehe 31 Oktoba,2010 jeshi la police lilitanda katika kona mbali mbali za jiji la Mwanza wakiwa katika magwanda na vifaa vya kivita kama bunduki,mabomu na magari ya maji ya pilipili kwa lengo la kuingilia mchakato wa kutangaza matokeo ya uchaguzi.
Baada ya harakati za wananchi wenye mapenzi mema na nchi yao kupitia harakati za demokrasia kuisha jeshi la polisi huhifadhi dhana/vifaa hivyo mithili ya nguo za kuendea kwenye sherehe na kusubiri tukio jingine ili kusambaratisha jitihada zao kwa kisingizio cha kulinda Amani.
Jumuiya ya wanachadema inalaani kitendo hicho cha police na lawama zinaelekezwa kwao kwa kusababisha watu wengine kupoteza maisha, wengine kupata vilema vya maisha, wengine kupoteza mali zao. Tunawasihi mawaziri wenye mamlaka husika idara ya ulinzi, Tamisemi wayafanyie kazi matatizo ambayo yamesababisha tafurani hiyo kwa kurudia uchaguzi upya wa umeya wa jiji la Arusha.
Tunapenda pia kutoa ushauri kwa baadhi ya viongozi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ambao inaonekana busara inataka kuwatoka waache kukejeli kauli za wadau/ jumuiya mbalimbali ambazo zinalaani kitendo hicho,kwani kwa kufanya hivyo ni kuingilia uhuru wa watu kuikosoa na kuirekebisha serikali yao pale inapokosea pasipo kusababisha uvunjifu wa amani.
Tunawapongeza pia viongozi wa Chadema taifa kwa kuonyesha mshikamano wao na nia yao ya kuendelea kuwatetea wananchi na kauli ya Mwenyekiti wa taifa chadema kugharamia gharama za mazishi ya wale ambao wamepoteza maisha yao, na matibabu kwa wale waliojeruhiwa katika harakati za kudai haki zao.Tunaomba moyo huu uigwe na viongozi wengine.

Mungu ibariki Tanzania, mungu ibariki afrika
Imetolewa leo tarehe 12.01.2011
Uongozi wa CHADEMA
Wilaya ya Geita
Mkoa mpya wa Geita
C. 1.jpg
 
Mwaka JK matamko yatamtoa roho hadi ayasome yote miaka mitano itakuwa imepita na ahadi zake zitakuwa bado kutekelezwa!
 
Good, naamini mtaandamana pale uongozi wa CHADEMA Taifa utakapotoa taarifa.
 
Matamko yaendelee!..kuna jamaa pale anauliza"so what"...nia ni kutaka wananchi wote tokea Ngara had Tandahimba wamjue dhulmat-ccm anayetumia vyombo vya walipa kodi wote, kujinufaisha yeye binafsi, na kuwaacha wao wakifa+kwa umasikini, na huku wakitandikwa risasi kama swala wa kitoweo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom