CDF Mstaafu Mabeyo ametaka kufikisha ujumbe. Je, wananchi tumeuelewa ujumbe?

Aibu ikamtengua kabla ya kutenguliwa saivi kimyaa asee dharau na kiburi mafikio yake mabaya
Ndugai alikuwa na dharau sana, alishawahi kumpiga mtu bakora mpaka akaanguka, kwenye mkutano wa kampeni.

Halafu, kama ile haikuwa aibu ya kutosha, akaja kukumbushia huku anajisifu.
 
ningekuwa Mabeyo ningebadili gia angani, ningeitisha uchaguzi mkuu tu ..kwamba sina imani na waliobaki...nataka mrudi kwenye uchaguzi mkuu tu:cool:. Ningeweka rekodi na msingenisahau milele, ningekuwa kwenye vitabu vyenu vya kumbukumbu..........bahati nzuri sikuwa CDF :p
 
ningekuwa Mabeyo ningebadili gia angani, ningeitisha uchaguzi mkuu tu ..kwamba sina imani na waliobaki...nataka mrudi kwenye uchaguzi mkuu tu:cool:. Ningeweka rekodi na msingenisahau milele, ningekuwa kwenye vitabu vyenu vya kumbukumbu..........bahati nzuri sikuwa CDF :p
Hiyo mara nyingi ni rahisi sana mdomoni, ila kivitendo ni ngoma nzito.

Usikute opsheni zote zilizingatiwa, hitimisho likawa, Not a chance!

Je, unajua zile timu mbili kubwa zilizokuwa zikihasimiana na kuchezeana rafu za waziwazi?

Halafu hapo hujajua wale wavaa-suti nyeusi wataangukia mrengo gani.
 
Katiba Ina mapungufu ila kwa hili la Uraisi iko wazi kabisa kuwa endapo itatokea Raisi kushindwa kumiliki ofisi kwa ugonjwa kifo au Sababu yeyote Makamu ndiye anachukua
 
Ni miaka 3 imepita tangu Rais Magufuli afariki. Ni jambo la kawaida, hasa siku ya maziko au wakati wa kutangaza kifo, kutolewa taarifa za kina za mazingira ya kifo cha marehemu, na kama pengine marehemu alitoa kauli yoyote. Haikuwa hivyo kwa Hayati Magufuli.

Wengi walipenda na walikuwa na shauku, msiba tu ulipotokea, wafahamu kwa kina aliugua lini, alifikishwa hospitali lini, jitihada zilizofanywa katika harakati za kuokoa uhai wa marehemu, mpaka kushindikana, na hatimaye kuyapokea mapenzi ya Mungu. Kukosekana kwa taarifa hizo, kumesababisha maneno mengi, ya kweli na yasiyo ya kweli.

Miaka 3 baadaye, baadhi ya taarifa za kina zimetolewa na CDF. Siamini kama taarifa hizi zimetolewa tu ili kujifurahisha, bali kuna ujumbe umetumwa kwa wananchi.

UJUMBE MUHIMU
Kuna shida kwenye katiba ya nchi. Kuna vitu havijawa sawa na kwa uwazi. Kwa maelezo ya CDF, ni kwamba ni yeye CDF ndiye aliyetoa msisitizo wa kuwa ni Makamu wa Rais ndiye anatakiwa kuwa Rais, na siyo mwingine yeyote. Tena ameeleza kuwa ni yeye CDF ndiye aliyeelekeza kuwa inabidi makamu wa Rais aapishwe kabla ya maziko ya Rais maana bila hivyo jeshi haliwezi kumtambua kama ndiye Amiri Jeshi Mkuu.

Lakini pia Rais mstaafu Kikwete, wakati Ndugai alipoondolewa kwenye nafasi ya uspika, alieleza kuwa Rais alipofatiki, spika alimwendea na kumwambia kuwa kwa mujibu wa katiba, yeye spika ndiye anatakiwa kuwa Rais. Yeye Kikwete alimkatalia.

Lakini pia zipo habari ambazo hazijawekwa wazi, huenda zikawekwa wazi siku za mbeleni, kuwa wale waliokuwa wakipinga Makamu kuchukua nafasi ya Urais baada ya kifo cha Rais, walieleza kuwa katiba inasema kuwa Rais akitoka bara, makamu atatoka visiwani. Na kwa vile aliyefariki alikuwa anatoka bara, urais ulikuwa nafasi ya bara, nafasi ya visiwani ilikuwa ni umakamu, hivyo makamu aendelee kuwa makamu.

HATARI ILIYOPO
Tusistegemee nyakati zote tutakuwa na CDF wa aina ya Mabeyo. **** siku tutakuja kuwa na CDF mwoga wa kutoa maamuzi na wanadiasa wakatii, au tukawa na CDF mwenye tamaa ya madaraka, anaweza kutumia nafasi ya kukosekana maelewano miongoni mwa wanasiasa, akayanyakua madaraka yeye CDF.

HITIMISHO
Tumepewa ujumbe ambao ni angalizo, kuwa tunatakiwa kuiweka sawa katiba ili kila jambo liwe wazi kwenye katiba, na katiba izibe mianya yote ya tafsiri zisizokusudiwa.

Mapungufu yetu ya katiba hayapo tu pale ambapo Rais atafariki akiwa madarakani, yapo maeneo mengi. Tangu enzi za Tume ya Jaji Nyalali, mapungufu ya katiba yamekuwa yakiainishwa, lakini wafanya maamuzi wamekuwa magumegume, wanafanya mabadiliko madogo madogo kwenye maeneo yale tu wanayoona yanawahakikishia kubakia madarakani hata bila ya matakwa ya umma.

Hata Samia ambaye nusura asiwe Rais kwa sababu ya sintofahamu za katiba, baada ya kuipata Urais, hataki katiba mpya kwa vile anaona iliyopo inamhakikisha mamlaka ya kuwa hata dikteta akitaka, bila ya kubughudhiwa. Amesahau kuwa bila ya hekima ya CDF huenda asingekuwa Rais. Manufaa yake binafsi yamefifisha hekima yake katika kuyaangalia maslahi ya Taifa.

Ni lini tutampata Rais mzalendo anayelitazama zaidi Taifa kuliko madaraka yake binafsi na manufaa ya chama chake? Kuwa na hawa viongozi wanaojali zaidi madaraka kuliko madlahi ya Taifa, kuna siku nchi itakwenda kwa namna isiyotarajiwa. Pongezi kwa CDF kwa kujali maslahi ya Taifa.
Magufuli alikuwa ni mwanasayansi...
Hivyo akamfafanulia CDF hiki kilichofanyika hapa ni maksudi...wameshani....hivyo nipeleke tu nyumbani....
Aah washkaji nilikuwa naota tu
 
Gen Venance Mabeyo akiwa na viongozi waandamizi wa Ulinzi na Usalama

Nimesikiliza clip ya mahojiano ya Mstaafu CDF Gen Venance Mabeyo na mwandishi wa habari wa gazeti la serikali, Daily News.

Udhubutu wa kuyaweka mambo wazi ni kipaji na ujasiri ambapo nampongeza kwa dhati Gen Mabeyo kwa hilo.

Mambo mengi imekuwa utamaduni kuyafutika futika na hivyo ukweli kutojulikana.

Kwa dhamira njema kabisa, Gen Mabeyo amethibitisha kuliweka mbele Taifa kama kiapo chake kinavyomtaka, kulinda Katiba.
Huu ni ujasiri usio kawaida, maana kwa watu walafi wangeweka maslahi yao mbele kuliko matakwa ya Taifa na Katiba.

Tunaona umuhimu wa viongozi waadilifu, ambao siku hizi ni wachache.

Mungu akulinde Gen. Venance Mabeyo.
Apewe another SILVER STAR 🌟
 
Naam,

Watu wangeweza kuhakiki vizuri nyendo za Paroko na Kardinali siku gani zilikuwaje.

Ile haikuwa interview, ile ilikuwa kama lecture.

In fact, it was a sermon, not even a lecture. Kwenye lecture huwezi kuuliza swali tu kwanza lazima unyooshe mkono.

Muandishi wa Daily News hata hakunyoosha mkono, alikuwa kama kakaa kanisani anasikiliza mahubiri, akinong'ona ni kama anasema "Preach" "Halleluyah".

Ukiangalia na kusikiliza unaona na kusikia kabisa muandishi kasahau kazi yake ya kuuliza maswali, kakaa pale anamuogopa, anamtukuza, anamuhusudu, anamshangaa Mabeyo.

Waandishi wa Daily News walishapewa maagizo kwamba wasimuulize swali wala kumuingilia Mabeyo, wamuache aseme alichotaka kusema tu.

Daily News ni chombo cha serikali, hapa kuna propaganda za serikali zinaendelezwa.

Ndiyo maana Mabeyo hajatoa hizi habari kwenye mkutano na waandishi wa habari au kwenye chombo binafsi cha habari ambako angeweza kubanwa vizuri kwa maswali.
Preeach.😀😀
 
ningekuwa Mabeyo ningebadili gia angani, ningeitisha uchaguzi mkuu tu ..kwamba sina imani na waliobaki...nataka mrudi kwenye uchaguzi mkuu tu:cool:. Ningeweka rekodi na msingenisahau milele, ningekuwa kwenye vitabu vyenu vya kumbukumbu..........bahati nzuri sikuwa CDF :p
Sasa hata mkirudi kwenye uchaguzi ingewasaidia nini? Wagombea wenyewe Mwigulu Nchemba na January Makamba si mkosi mtupu huo?
 
Ndugai alikuwa na dharau sana, alishawahi kumpiga mtu bakora mpaka akaanguka, kwenye mkutano wa kampeni.

Halafu, kama ile haikuwa aibu ya kutosha, akaja kukumbushia huku anajisifu.
Kitu ambacho sitokuja nimsamehe Ndugai NI kumfuta ubunge Lisu huku akiwa kitandani anajiuguza.

Hii laana itamuandama mpaka kaburini.
 
Kitu ambacho sitokuja nimsamehe Ndugai NI kumfuta ubunge Lisu huku akiwa kitandani anajiuguza.

Hii laana itamuandama mpaka kaburini.
Hawa watu walitakiwa kupigwa tit for tat tu.

Wewe mwenzako anakula pensheni kwa sheria ya mafao ya viongozi mpaka anakufa halafu wewe unajifariji kwa kusema laana itamuandama mpaka kaburini mkuu?

Kama laana ndiyo kuishi kwa mafao hayo, hata mimi naitaka mkuu.
 
Back
Top Bottom