JanguKamaJangu
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,177
- 7,472
Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi Tanzania, Jenerali Venance Mabeyo amesema anatamani Jeshi letu liwe la kisasa zaidi na liweze kuchangia uchumi wa nchi na liwe la kujitegemea ‘sustainable military’.
“Kwa nini wenzetu wanatengeneza zana kutuuzia sisi, na kwa nini na sisi tusitengeneze zana za kututosheleza sisi wenyewe, wenzetu wana nyumba nzuri, hoteli, wanachangia uchumi wa nchi.
“Napenda Wanajeshi wote wawe na afya ya akili na wawe wanafikiria maendeleo muda wote,” anasema Mabeyo alipokuwa akihojiwa na ITV.
Kuhusu Jeshi kuaminiwa
"Wosia wangu kwa Watanzania ni kulisaidia Jeshi...tukifanya mambo mazuri wananchi wanatusifia, tukifanya mambo mabaya kwa bahati mbaya hata kama ni mtu mmoja kafanya...tunajumuishwa Wanajeshi wote, tunashutumiwa vibaya sana, nawaomba msiwashutumu," - Jenerali Mabeyo.
Kuhusu ugaidi Tanzania
"Baada ya kutoka Kibiti waliteremka Kusini mikoa ya Mtwara, Ruvuma...kuna wananchi wetu waliathirika...kuna baadhi ya vijiji ukienda kule Tandahimba...Nanyamba...Mtwara Vijini wameathirika... mpaka Newala baadhi ya maeneo...
"Wengine wamevamiwa, wamechomewa nyumba zao, wameharibiwa mali zao, baadhi ya Watanzania wametekwa na vile vikundi na kulazimishwa kuvuka upande wa pili," Jenerali Mabeyo.
Chanzo: ITV