nngu007
JF-Expert Member
- Aug 2, 2010
- 15,862
- 5,797
KITAIFA
[h=1][/h]
Bendera ya Chama Cha Mapinduzi(CCM) Picha na Maktaba
Na Mwinyi Sadallah, Mwananchi
Posted Januari18 2014 saa 10:17 AM
KWA UFUPI
- Ni katika mkakati wa pamoja katika kikao cha pamoja kilichofanyika mapema wiki hii.
Zanzibar. Wabunge na Wawakilishi wa CCM Zanzibar tayari wamekutana na kupanga mkakati wa pamoja kwa nia ya kupinga Mfumo wa Muungano wa Serikali tatu uliopendekezwa katika Rasimu ya Tume ya Mabadiliko ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imefahamika juzi visiwani Zanzibar.
Uchunguzi wa Mwananchi umebaini kuwa kikao hicho kilifanyika Ofisi Kuu ya CCM Kisiwanduwi kuanzia saa 9.00 Alasiri hadi saa 1:00 ya usiku chini ya Uenyekiti wa Makamo wa Pili wa Rais, Balozi Seif Ali Iddi na Naibu Katibu Mkuu wa chama hicho Zanzibar, Vuai Ali Vua.
Vyanzo mbalimbali vya habari kutoka ndani ya kikao hicho vinaeleza kwamba, wabunge hao wa Bunge la Katiba walipokea msimamo wa chama chao na kutakiwa kuutetea kwa umoja wao watakapojadili rasimu hiyo.
Baada ya kuwasilishwa ajenda hiyo kikaoni, wajumbe mmoja baada ya mwingine walitoa maoni yatakayofanikisha kufuzu kwa mkakati huo huku wengine wakishauri wajumbe wapewe nafasi ya kuijadili rasimu kupitia semina ili kujua ni maeneo gani yana manufaa na hasara.
Imeelezwa Mwakilishi Hamza alisema kutokana na umuhimu wa rasimu hiyo,waandaliwe semina maalumu ili kukijadili kwa kina kifungu baada ya kifungu kabla ya kufikia uamuzi wa kupitisha na kutopitisha mambo yasiyokuwa na manufaa kwa Zanzibar na Usalama wa Muungano wenyewe.
Alisema suala la Katiba halipaswi kujadiliwa haraka,linahitajika umakini kwa manufaa ya Zanzibar na wananchi wake na kukiomba chama hicho kitayarishe semina hiyo ya uchambuzi, kujenga uwezo na ufahamu kabla ya Bunge la Katiba halijakutana na kujadili rasimu hiyo.
Hata hivyo kwa upande wake, Asha Bakari aliweka wasiwasi wake kwa wajumbe kuhusu kukosa msimamo wa pamoja na kutaka kila mjumbe aulizwe kama anataka Serikali tatu au mbili badala ya kuja kupanga na baadaye kusalitiana mbele ya safari na kuhatarisha misingi ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
Hata hivyo, mfanyabiashara maarufu na Mbunge wa Mpendae ,Salum Turkey alisema kutokana na uzito wa suala la mfumo wa Muungano ni vizuri kukafanyika kisomo maalumu (halbadiri) na mjumbe yoyote atakayekwenda kinyume na msimamo wa chama apate laana duniani na akhera.
Wazo hilo licha ya kuwashtuwa baadhi ya wajumbe, wengi walionekana kukubaliana naye ili mkakati wa chama hicho uweze kufikiwa huku Waziri wa zamani,Hamza Hassan akisisitiza rasimu yote ya katiba ichambuliwe yanayokubalika na yasiyokubalika kabla ya Bunge la Katiba kukutana mwaka huu.
Hata hivyo Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Vuai Ali Vuai hakuweza kupatikana kuelezea kikao hicho na maazimio yaliyofikiwa baada ya kuulizwa kwa njia ya simu na kueleza yupo katika kikao na atafutwe muda mwengine mara baada ya kikao hicho.
Vuia aliwahi kutoa msimamo wake wakati akifungua mkutano wiki mbili zilizopita akisema atakuwa wa mwisho kuafiki.