CCM yazoa wanachama wapya wilayani Temeke

Kibo10

JF-Expert Member
Aug 20, 2013
11,280
2,000
Watu 250 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Tawi la Kigunga B, Kilakala wilayani Temeke jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya, Katibu wa Vijana wa CCM, wilayani Temeke Onesha Haruna amesema viongozi wa chama hicho wana jukumu kubwa la kuhakikisha idadi ya wanachama inaongezeka kila kukicha.

Hili litafanikiwa ikiwa kila mmoja wao atatekeleza ilani ya chama chao kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kufanya uhamasishaji kwa watu mbalimbali.

“Ilani ya CCM haina mapungufu hata chembe. Ikiwa itafuatwa na kutekelezwa kila kilichoandikwa ndani yake, ni wazi kuwa chama chetu kitakuwa chama cha mfano na chenye kuongoza kwa idadi ya wanachama kuliko hata ilivyo sasa” alisema.

Licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo za ndani kama vile kuwepo kwa makundi ndani ya chama, bado kimeonyesha kuimarika zaidi kutokana na kuwa na viongozi wenye moyo madhubuti wa kukiongoza.

Katika hotuba yake, Haruna alitoa wito kwa wenyeviti wa vijana katika matawi ya wilaya hiyo kuhamasisha makundi ya vijana kujiunga na CCM.

“Vijana ni taifa la leo, hivyo kuwa na ushiriki mkubwa ndani ya chama, kuwezesha kupatikana kwa maendeleo kwani siku zote chama ni watu,” alisema Haruna.
 
kababu

JF-Expert Member
Mar 14, 2013
1,593
2,000
heri waamie ccm km watu tuliokuwa tunawategemea ndio hao wanakusanya mia tano tano zetu, bila kutuonea huruma anaenda kula na hawara yake dubai,
 
m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,374
2,000
heri waamie ccm km watu tuliokuwa tunawategemea ndio hao wanakusanya mia tano tano zetu, bila kutuonea huruma anaenda kula na hawara yake dubai,

We kweli msukule! nenda kachukue buk 7 yako.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
79,193
2,000
heri waamie ccm km watu tuliokuwa tunawategemea ndio hao wanakusanya mia tano tano zetu, bila kutuonea huruma anaenda kula na hawara yake dubai,

Hongera ! Kufumba na kufumbua post yako imeingia kwenye ile TOP TEN ya post mbovu ya mwaka ! Endelea kutuma zaidi ujiongezee nafasi ya kushinda .
 
kibogo

JF-Expert Member
Apr 1, 2012
9,728
2,000
Watu 250 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Tawi la Kigunga B, Kilakala wilayani Temeke jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya, Katibu wa Vijana wa CCM, wilayani Temeke Onesha Haruna amesema viongozi wa chama hicho wana jukumu kubwa la kuhakikisha idadi ya wanachama inaongezeka kila kukicha.

Hili litafanikiwa ikiwa kila mmoja wao atatekeleza ilani ya chama chao kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kufanya uhamasishaji kwa watu mbalimbali.

"Ilani ya CCM haina mapungufu hata chembe. Ikiwa itafuatwa na kutekelezwa kila kilichoandikwa ndani yake, ni wazi kuwa chama chetu kitakuwa chama cha mfano na chenye kuongoza kwa idadi ya wanachama kuliko hata ilivyo sasa" alisema.

Licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo za ndani kama vile kuwepo kwa makundi ndani ya chama, bado kimeonyesha kuimarika zaidi kutokana na kuwa na viongozi wenye moyo madhubuti wa kukiongoza.

Katika hotuba yake, Haruna alitoa wito kwa wenyeviti wa vijana katika matawi ya wilaya hiyo kuhamasisha makundi ya vijana kujiunga na CCM.

"Vijana ni taifa la leo, hivyo kuwa na ushiriki mkubwa ndani ya chama, kuwezesha kupatikana kwa maendeleo kwani siku zote chama ni watu," alisema Haruna.

Wale wataalam wa Takwimu wanasema unapotaja idadi na namba ikaishia na zero basi hiyo takwimu ni feki na ndio maana hata katika takwimu za Sensa yetu waliamua kuweka Namba 4 mwisho ili kuondoa ufeki ingawa ilikuwa feki kwa hiyo hata Hii taarifa yako ni FEKI kwa sababu ya hiyo zero
 
kajirita

JF-Expert Member
Jul 27, 2013
1,575
1,225
Magamba yaliyovaa Magwanda yanayowaaminisha watu kuwa yamekuwa ni magwanda yaliyoota magamba!
 
Kibanga Ampiga Mkoloni

JF-Expert Member
Aug 9, 2007
18,452
2,000
Hakika JIONI ya leo, nitakuwa hapo kuthibitisha ukweli huu wa watu 250 kujiunga na CCM maana kama ni kweli basi hili nipigo kwa CUF na harakati za Ukombozi kiujumla.
 
Toothpick

JF-Expert Member
Nov 14, 2013
348
250
Vitu kama hivi ukiwasimulia watoto wanaweza kukuelewa kuliko hapa jf.Unapaswa kuangalia cha kuleta hapa jf sio lazima uonekane unatoa mada,ukiwa mchangiaji inatosha kuliko kujizalilisha namna hii.
 
Rugaijamu

JF-Expert Member
Jul 10, 2010
2,938
2,000
Ni haki yao kujiunga na chama chochote cha siasa,lakini kwa mtu makini mwenye akili timamu,anayetambua namna Nchi ye2 ilivyoharibiwa na wananchi wake kufanywa mafukara wa kutupwa,HAWEZI KUJIUNGA NA CCM....!
 
Comi

JF-Expert Member
Oct 2, 2011
3,329
1,500
Yaani watu wengine ovyo kweli. Kati ya ccm na nccr nani anatakiwa kusema amepata wanachama wapya?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom