CCM yazoa wanachama wapya wilayani Temeke

hao watu ni wakuangalia IQ zao kama ziko sawa. ccm tena?
Watu 250 wamejiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) kupitia Tawi la Kigunga B, Kilakala wilayani Temeke jijini Dar es salaam.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi kadi kwa wanachama wapya, Katibu wa Vijana wa CCM, wilayani Temeke Onesha Haruna amesema viongozi wa chama hicho wana jukumu kubwa la kuhakikisha idadi ya wanachama inaongezeka kila kukicha.

Hili litafanikiwa ikiwa kila mmoja wao atatekeleza ilani ya chama chao kwa vitendo, ikiwa ni pamoja na kufanya uhamasishaji kwa watu mbalimbali.

“Ilani ya CCM haina mapungufu hata chembe. Ikiwa itafuatwa na kutekelezwa kila kilichoandikwa ndani yake, ni wazi kuwa chama chetu kitakuwa chama cha mfano na chenye kuongoza kwa idadi ya wanachama kuliko hata ilivyo sasa” alisema.

Licha ya kuwepo kwa changamoto ndogo ndogo za ndani kama vile kuwepo kwa makundi ndani ya chama, bado kimeonyesha kuimarika zaidi kutokana na kuwa na viongozi wenye moyo madhubuti wa kukiongoza.

Katika hotuba yake, Haruna alitoa wito kwa wenyeviti wa vijana katika matawi ya wilaya hiyo kuhamasisha makundi ya vijana kujiunga na CCM.

“Vijana ni taifa la leo, hivyo kuwa na ushiriki mkubwa ndani ya chama, kuwezesha kupatikana kwa maendeleo kwani siku zote chama ni watu,” alisema Haruna.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom