thetallest
JF-Expert Member
- Oct 21, 2017
- 8,256
- 9,085
Nchimbi ni barozi anaiwakilsha nchi, kama sikosei ni BrazilKamati Kuu ya CCM imeteua wagombea ubunge katika majimbo matatu kama ifuatavyo; Monko Joseph (Singida Kaskazini), Damas Ndumbaro (Songea Mjini) na Stephen Kiruswa (Longido).
View attachment 651911
My Take;
Rais alisema sasa ni muda wa kazi tu. Nchimbi, Kimbisa na Sophia Simba mlisema mumewasamehe.
Kama tunavyojua Nchimbi ndo alishinda Kura za Maoni. Kwanini mumekata jina lake. CCM acheni kulipiza visasi.
Uchaguzi ushaisha na sote tunajenga nchi moja.
Hili swala limenisikitisha sababu si la kozalendo. CCM ubaguzi wenu hautawaacha salama.
Pale Dodoma Mlitangaza kwamba mumewasamehe wote waliomuunga mkono Lowassa, na Nchimbi alitubu hadi akakaribishwa Ikulu.
Kama ndivyo Nape Nnauye, Hussein Bashe wajiandae Kisaikolojoa 2020. Hawatapita sababu ya kuongea ukweli na kwenda kinyume na CCM.
Bashe alilalamika bungeni kwamba watu wasiojulikana wanamfuatilia.
Nakumbuka Bashe na Msukuma waliwekwa Korokoroni kisa wanahoji pale CCM inapokosea.
Hii mbaya sana kuongoza kwa visasi.