John Nchimbi na Haider Gulamali washinda kura za maoni Songea Mjini na Singida Kaskazini

Boniphace Kichonge

JF-Expert Member
Jul 31, 2017
1,607
2,000
Wadau
John Nchimbi na Haider Gulamali wamefanikiwa kushinda kura za maoni katika mchakato wa kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ys CCM kwenye uchaguzi wa Ubunge katika maajimbo ya Songea Mjini na Singida Kaskazini.

1.Songea Mjini
Wagombea. 20
Wapiga kura 605
Ndg John Nchimbi kura 219
Dk Theresia Huvisa kura 181.
Ndg Damas Ndumbaro kura 83

2.Singida Kaskazini
Wagombea 20
Wapiga kura 1,010
Ndg Haider Gulamali kura 606
Ndg Justine Monko kura 133
Ndg Juma Mgoo aliyekuwa Mkurugenzi wa huduma za misitu kura 46.

Mchakato wa uteuzi bado utaendelea kupitia vikao vya juu vya CCM.
 

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
26,565
2,000
Siku hizi radha ya uchaguzi imekwisha uchaguzi umegeuka vita, kwanini CCM wasichague jina moja wakalipeleka NEC kuthibitishwa ili akaapishwe bungeni ili kuepuka gharama na usumbufu.
Swadaktaaaa,
Tunapoteza Muda na Hela bure wakati NEC wanae tayari mshindi wao mfukoni,
Bora tu wafanye mambo yao mengine
 

johnthebaptist

JF-Expert Member
May 27, 2014
38,808
2,000
Wadau
John Nchimbi Na Haider Gulamali wamefanikiwa kushinda kura za maoni katika mchakato wa kuomba ridhaa ya kupeperusha bendera ys CCM kwenye uchaguzi wa Ubunge katika maajimbo ya Songea Mjini na Singida Kaskazini.
1.Songea Mjini
Wagombea. 20
Wapiga kura 605
Ndg John Nchimbi kura 219
Dk Theresia Huvisa kura 181.
Ndg Damas Ndumbaro kura 83
2.Singida Kaskazini
Wagombea 20
Wapiga kura 1,010
Ndg.Haider Gulamali kura 606
Ndg Justine Monko kura 133
Ndg. Juma Mgoo kura 46
(Ndg Juma Mgoo aliwahi kuwa Mkurugenzi wa huduma za misitu)
Huyu Ndumbaro mi yule wa Wekundu wa Msimbazi?!!
 

Namalenga

Senior Member
Dec 7, 2017
146
225
Siku hizi radha ya uchaguzi imekwisha uchaguzi umegeuka vita, kwanini CCM wasichague jina moja wakalipeleka new kuthibitishwa ili akaapishwe bungeni kuepuka gharama na usumbufu.
Acha kulialia wakati wewe ni dawa, kama wewe unalia unadhani mgonjwa afanye nini?
 

Lutifya

JF-Expert Member
Jan 6, 2011
1,374
2,000
Duuh huyu Justine Monko mate wangu wa Arusha Tech.college hilo jimbo amelitafuta muda mrefu bila mafanikio pamoja na Baba yake alikuwa mbunge wa jimbo husika. Ingawa ni DED kwa sasa
 

The Palm Tree

JF-Expert Member
Apr 13, 2013
6,562
2,000
Kwahiyo Prof Kitila wamempotezea?!!!!

Vijana wa UVCCM kwanza muwe na ufahamu wa ishu mnayoijadili...

Prof Kitila Mkumbo si mkazi wa Singida Kaskazini. Yeye ni mkaazi wa Iramba Magharibi (Jimbo la Mwigulu Madelu Nchemba) kwa sasa....

Kitila kwa kabila ni Mnyiramba na wazazi na karibu ukoo wake wote makaazi yao ni huko Iramba magharibi....

Singida Kaskazini asilimia karibu 90 wakaazi wake ni kabila la wanyaturu. Kumlazimisha Kitila Mkumbo kutoka Iramba akagombee ubunge eneo ambalo hana hata kibanda cha makaazi, ugenini ni kwenda kulazimisha ushindi wa damu tu kwa sbb by any means angeenda kukataliwa na wapiga kura....

Hapa hata kama CCM wanaweza kushinda pasipo hata kutumia nguvu iwapo tu watakuwa wise enough kuweka mtu anayekubalika ktk eneo husika na wenyeji...

Lakini kumpeleka huyu jamaa mgeni kule ingekuwa ni indicator number one ya kugaragazwa asubuhi tu na baadaye mtumie bunduki kuua watu kulazimisha ushindi.....

Chukueni watu wenye hata nusu ya uenyeji huko wenye sifa na wako kibao tu wagombee ili at least kupunguza ulazima wa kutumia bunduki za SMG kulazimisha ushindi....

Kwa sbb mimi naamini, Lazaro Nyalandu akirudi kugombea kwa tiketi ya chama kingine chochote lazima atawapelekesha na kwa 100% ataweza kabisa ku - retain Jimbo lake unless mtumie undavaundava wa umwagaji damu na uhuni mwingine kupora ushindi wake...!!

Lakini kama uchaguzi utakuwa free and fair, CCM saa 3asb tu watakuwa wamegaragazwa na maCHADEMA, trust me!!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom