CCM yasikitishwa, yaomba radhi kwa Bango lenye ujumbe wa Uchochezi Zanzibar

W
No way.....kuweni specific.Bango halikubebwa na Mwanachi mmoja bali lilibebwa na Mwanachama wa CCM akiwa mbele akiongoza wengine huku akiwa amevaa sare za ccm.Kwani kabla ya kuanza maandamano hawakukaguwa mabango au kila mtu alikuwa anaandika atakavyo...????hapo inaonesha wako dis organized....SHAME.....SHAME....SHAME...hii ni dhambi mbaya saana na itawatafuna milele.Mzee Karume muasisi wa mapinduzi aliowa Muarabu wakajaaliwa watoto machotara sasa leo anatukanwa.NO.....NO....NO.
Wapuuzi sana eti bango lilibebwa na mwananchi wakati ni mwanachama wao,waliliandaa wao wenyewe kwa utashi wao wa kiubaguzi waache kujitetea hapa
 
Nilidhani wangesema tumekosea kama binadamu kwa vile hatujakamilika na tunaomba msamaha kwa wote.baada ya hapo wahusika waachie ngazi kistaarabu tu.Sasa hivi kampeni zikifanywa ccm hawatapata kura kutokana na bango lao.Ni vizuri CUF wakubali kurudia na wapige kampeni kwa kutumia hilo bango.Matokeo yatangazwe baada ya wagombea wote kukubali kura zilizopigwa.
 
h
Huyo ni mwananchi wa kawaida au ni vijana wa CCM ambao wako kwenye maandamano kabisa na askari wapo.

Acheni kufanya watu wote wana akili kama zenu.
apa kwa wenye akili timamu wanapata jibu kuwa hata hayo mazungunzo yanayoendelea ccm wanamchukulia maalim seif kwa mtazamo wa hilo bango.
 
TAARIFA KWA UMMA

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimesikitishwa sana na ujumbe wenye maudhui ya ubaguzi ulioandikwa kwenye moja ya Bango lililobebwa na mmoja wa wananchi waliojitokeza katika maadhimisho ya Sherehe za Miaka 52 ya Mapinduzi ya Zanzibar.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinaomba radhi kwa ujumbe huo, kinapinga na kinakemea kabisa fikra, hisia na mitazamo yoyote yenye maudhui ya kibaguzi.

Ujumbe huo sio tu kuwa una maudhui ya kibaguzi bali pia unaenda kinyume kabisa na falsafa na Shabaha ya waasisi wa Mapinduzi hayo Matukufu ya mwaka 1964 na unapingana na misingi na itikadi ya CCM inayohimiza Umoja na Mshikamano wa Kitaifa.

Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
12/01/2016

View attachment 316495

Daniel Chongolo
Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM.
Wewe unajiita Mkuu wa Mawasiliano na Umma CCM ndio wakushtakiwa kwasababu ndie uliowatuma wafanye hivyo baada ya kuwajua kwamba hawakusoma ni wajinga ndio ukatumia fursa ya kuwatumilia ili ulete mfarakano dhidi ya Wazanzibari ili wapate kuzidi kuchukiana wenyewe kwa wenyewe na hata pengine kufikia kuuwana kama yaliyotokea Burundi, Wazanzibari 95% ni watu waliochanganya damu lakini kwa kupotosha kwa siasa mbovu mlizokuwa nazo ndio wengine wameshindwa kujijua kama wazee wao wazamani babu wa babu wa babu au bibi wa bibi wabibi aidha ametokea Yemen/ Oman / Syshells / Commoro au Iran na kwa vile wakijitizama rangi ya ngozi zao wanajiona wao ni waafrika safi hawana mchanganyiko wa damu yakigeni na kutokana na jina lako wewe Daniel Chongolo wazanzibari wengi tunakutilia shaka kwamba huna asili ya Zanzibar na wala huijui historia ya Zanzibar.
 
Kama walisikitishwa na ujumbe ule wa kibaguzi, ambao kwa hakika ni wa kibaguzi na kuhatarisha amani ya Zanzibar na Tanzania kwa ujumla, je CCM walichukua hatua gani za kinidhamu kwa Mwanachama wao huyo, au viongozi wa kwenye Tawi lake? Je serikali ya mapinduzi imefanya juhudi gani kwa kumfikisha kwenye vyombo vya sheria mtu huyo anayehatarisha usalama wa nchi?

Je, sheria za nchi zinasemaje kwa mtu kutoa ujumbe wa kuhatarisha usalama wa nchi?

Maswali ni mengi kuliko majibu mepesi yaliyotolewa na CCM!
 
Chongolo huna lolote bango mmeliandaa Kwa makusudi Na mmeamua kulipitisha mchana kweupe mbona viongozi wenu hawakulikemea palepale uwanjani Na walikuwepo? Malipo ya dhambi hiyo in hapahapa duniani Mungu anaona dhuluma mnayoifanya Bara na Visiwani ya Uchaguzi
 
Ubaguzi ni utamaduni wao hata sasa wamembagua MaalimSeif baada ya kushinda urais wanaendelea wao kutawala bila ridhaa ya Wazanzibari na wanatumia majeshi kuwatisha watu wasidai haki ya kiongozi wao waliomchagua.
 
Tz baada ya uhuru na hata muungano pamekuwa na Mawaziri na wabunge: wazungu, wahindi, waarabu etc kwa vile ni watanzania. Kigezo/Sifa ni uraia na sio rangi ya bendera. Pole sana kwani taifa letu lapoteza mwelekeo.
nini wabunge na mawaziri wahindi, hata Marekani ina Rais mweusi lakini ubaguzi dhidi ya mweusi upo.

Kwani kwenye bendera yetu rangi nyeusi ina maana gani?
 
Hii sera ya ubaguzi ipo na ilianza kuota mizizi hadi sasa .kama mnakumbuka dk. SALIM AHMED SALIM alipotaka kugombea uraisi wa tanzania ,wajumbe kutoka zanzibar walimpinga walisema ni muarabu na akatoswa .na wala hawakuulizwa kama huo ulikua ni ubaguzi .lakini marekani wazungu walimchagua obama muafrica .hii kuomba radhi ni unafiki uliotukuka .
Ubaguzi huwa ni jambo baya sana
 
W

Wapuuzi sana eti bango lilibebwa na mwananchi wakati ni mwanachama wao,waliliandaa wao wenyewe kwa utashi wao wa kiubaguzi waache kujitetea hapa
hii reply ya huyu mwamba naipa hadhi ya nyota tano kabisa! Kumbe sio mimi tu nnaewaona wanaccm kama wadudu flan nzi wa kijani
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom