CCM yapangua hoja za Chadema | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yapangua hoja za Chadema

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Wa Ndima, Sep 3, 2010.

 1. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #1
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimemuomba Msajili wa Vyama vya Siasa kuiagiza Chadema kuisoma na kuielewa vizuri Sheria ya Gharama za Uchaguzi na sheria nyingine za uchaguzi ili kuepuka usumbufu.

  Ombi hilo ni miongoni mwa maombi matatu yaliyotolewa na CCM wakati wa kujibu malalamiko yaliyotolewa na Chadema, dhidi ya Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia CCM,
  Jakaya Kikwete.

  Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa jana na Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba kwa vyombo vya habari, Chadema haijaelewa Sheria ya Gharama za Uchaguzi na kama
  inaelewa, imeamua kufanya usumbufu usiokuwa wa lazima kumwekea pingamizi Kikwete.

  Taarifa hiyo imenukuu kifungu 21 (1), “wakati wa uteuzi, kampeni
  za uchaguzi au uchaguzi, kitendo kinachokatazwa ni…” Kwa tafsiri ya asili kwa mujibu
  wa taarifa hiyo, maneno ya kifungu hicho hayahusu ahadi zitakazotekelezwa
  baada ya uchaguzi kwa kutumia fedha za Serikali, bali kinahusu ahadi zinazotekelezwa wakati wa mchakato wa uteuzi wa wagombea, kampeni au wakati wa uchaguzi.

  Pia kinakataza wagombea kutumia fedha binafsi kutekeleza ahadi zake. “Kama sheria hiyo ingekataza kutoa ahadi zitakazotekelezwa baada ya uchaguzi, ingeua dhana nzima
  ya kampeni inayovitaka vyama vya siasa na wagombea kuelezea mambo gani wanayoahidi iwapo watachaguliwa,” alisema Makamba.

  Makamba amesisitiza kuwa malalamiko ya Chadema hayahusu sheria hiyo kwa sababu haipingani na dhana nzima ya kampeni kama ilivyoainishwa ndani ya Sheria ya
  Uchaguzi, pamoja na maadili ya uchaguzi kwa ajili ya uchaguzi wa rais, wabunge na madiwani.

  CCM inasema inashangazwa na hatua iliyochukuliwa na Chadema kwa kuwa jambo lililofanywa na mgombea wa CCM, linafanywa pia na wagombea wa vyama vingine
  akiwamo Dk. Willibrod Slaa. CCM inamshangaa Kaimu Katibu Mkuu wa Chadema, John Mnyika anayejiita raia mwema kwa kutomuwekea Dk. Slaa pingamizi kwa kutoa ahadi kemkem katika kampeni zake kama kweli anaamini kuwa kutoa ni ukiukwaji wa sheria.
   
 2. M

  Mutu JF-Expert Member

  #2
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 30, 2008
  Messages: 1,333
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  swala si liko kwa Tendwa .
  MAKAMBA HAKUNA ANACHOJUA KWA KWELI Aibu,hawana waongeaji wengine huyu kichwa maji anaboa
   
 3. Zak Malang

  Zak Malang JF-Expert Member

  #3
  Sep 3, 2010
  Joined: Dec 30, 2008
  Messages: 5,410
  Likes Received: 18
  Trophy Points: 0
  Na ndo maana Tendwa aliomba aende ITV ili atoe huo "ufafanuzi" wake wa sheria hiyo katika kipindi cha Kipima Joto leo saa 3 usiku. Hii nadhani Tendwa anafanya kinyume cha utaratibu katika azma yake ya kuizima pingamizi la Chadema. Inakuwa kama vile kabla ya hakimu kutoa hukumu yake katika kesi anayoisikiliza, kwanza anakwenda kwenye TV kufanya mjadala na watu wengine kuhusu sheria ambayo chini yake ndiyo mshtakiwa anashitakiwa. Is this right? Nadhani hii ichukuliwe kama hoja moja ya kukata rufaa huko mbele iwapo pingamizi la Chadema litatupwa.
   
 4. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #4
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Wa Ndima
  Member

  Join Date
  Fri Aug 2010
  Posts
  44
  Thanks : 0
  Thanked 10 Times in 5 Posts
   
 5. Mpambalyoto

  Mpambalyoto JF-Expert Member

  #5
  Sep 3, 2010
  Joined: Mar 26, 2010
  Messages: 752
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Augusteez siyo?
   
 6. The Son of Man

  The Son of Man JF-Expert Member

  #6
  Sep 3, 2010
  Joined: Feb 9, 2010
  Messages: 12,124
  Likes Received: 1,709
  Trophy Points: 280
  Ndo manake mkubwa yaani utawaelewa tu, wako wengi dunia nzima!
   
 7. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #7
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145

  Una maana gani kuNOTE kujiunga kwangu. Sio wote unaowaona wamejiunga hapa ni wapya!!! Wengine tumefungua ID mpya. Soma hoja sio unaorodheka nimejiunga lini, unataka kumaanisha nini? Kwamba sijui kitu au? Acha hizo
   
 8. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #8
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  Ufinyu wa kufikiri huu. Hii ni stori halisi si ya kubuni tazama kesho HabariLEO fronpage
   
 9. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #9
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145

  Umeona enh??
   
 10. m

  mwita ke mwita JF-Expert Member

  #10
  Sep 3, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 5,501
  Likes Received: 1,226
  Trophy Points: 280
  makamba simuamini allisema bashe si raia mara akasema raisi kikwete alidanganywa, anasema mtu akimtukana baba yako inabidi usinyamaze wakati kikwete alimtukana baba yangu mfanyakazi kuwa ni mzandiki,mfitini,muongo na mnafiki.nitampinga kikwete kurejesha thamani ya mzazi wangu so makambba usijichanganye
   

  Attached Files:

 11. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #11
  Sep 3, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Huyu Mkuu ndo maana Alibaka akafukuzwa Kazi ya Ualimu Hana analojua kwani ukiangalia kwa Nyekundu utaona tu kwani Rais Kikwete anatumia madaraka yake vibaya sasa hawezi akampandisha waziri kuahidi kitu hii ni kutumia madaraka yake KIBABE, Sasa huyu Mzee kweli amezeeka maana anajibu vingine. Angalizo Tendwa Ofisi imekushinda au wewe si msomi au umechanguliwa tuu Fuatasheria usifuate watu wansema nini? Utajiaibisha sana wakienda mahakamani.:mad2:


   
 12. Original Pastor

  Original Pastor JF-Expert Member

  #12
  Sep 3, 2010
  Joined: Nov 14, 2007
  Messages: 1,256
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  Yap!! Hii Sheria lazima itawakamata tu wana CCM, Wakuu tunawaomba mkaze buti kwani ukibadili kitu mfano Rangi kwa nyumba itakubidi utumie gharama muda mwingi ili ubadilishe sasa CHADEMA mtaweza tu
   
 13. Kiby

  Kiby JF-Expert Member

  #13
  Sep 3, 2010
  Joined: Nov 16, 2009
  Messages: 5,209
  Likes Received: 1,012
  Trophy Points: 280
  Mshahara Jk anaowaahidi wafanyakazi utalipwa na serikali yake ikiwa watamrudisha madarakani au unaanza kulipwa katika miezi ya kipindi cha campaign? Na kama ni katika kipindi hicho ni kwa nini isiwe rushwa? Maana mwenye dhamana ya kutangaza mishahara mipya ni waziri baada ya pesa hizo kuidhinishwa na bunge. Tumuulize makamba mpayukaji, ni wapi na lini mshahara mpya ulitangazwa kwa mujibu wa sheria na kanuni za nchi? Kuahidi ni jambo moja na utekelezaji wa ahadi ni jambo jingine linalopaswa kutumia taratibu na sheria za nchi. Kweli chama tawala kimekosa umakini na kupoteza mwelekeo. Hapa Chadema wanachotakiwa ni kujiandaa kukiburuza ccm mahakamani ikiwa Tendwa hatatenda haki, ili wakamuumbue makamba kule kama ilivyotokea kwa kihiyo wa Temeke.
   
 14. Wa Ndima

  Wa Ndima JF-Expert Member

  #14
  Sep 4, 2010
  Joined: Aug 13, 2010
  Messages: 1,512
  Likes Received: 39
  Trophy Points: 145
  kaaaazi kwelikweli
   
 15. B

  Baija Bolobi JF-Expert Member

  #15
  Sep 4, 2010
  Joined: Feb 25, 2009
  Messages: 931
  Likes Received: 697
  Trophy Points: 180
  =====

  Mbona unaripuka kana kwamba hujui kitu kabisa!?
   
 16. Mimibaba

  Mimibaba JF-Expert Member

  #16
  Sep 4, 2010
  Joined: Jul 1, 2009
  Messages: 4,566
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0

  Unataka tuchangie nini? Makamba ni kichefu chefu kama amekutuma, hatuna matarajio ya jema toka kwake ni mpinzani wa haki za wengine isipokuwa zenu
   
 17. Ilumine

  Ilumine Senior Member

  #17
  Sep 5, 2010
  Joined: Dec 27, 2008
  Messages: 196
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  wametumwa hawa waje humu JF!
   
 18. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #18
  Sep 5, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,427
  Likes Received: 370
  Trophy Points: 180
  ID mpya august?
  wewe ni Augusteez kwishney.
  Kwani ukileta hoja yako kwa id yako ya awali itakosa mashiko?

  uzuri ni kwamba huwezi kushindana na saikolojia yako mwenyewe.
  mtajiumbua sana hapa kipindi hiki
   
Loading...