CCM yamwangukia Bashe!

CCM yamwangukia Bashe!

Kwa barua hii nakuomba uwe tayari kupokea maagizo yatakayokuwa yakitolewa kutoka ngazi mbalimbali, pia uzingatie ratiba ya jimbo ulilopangiwa. Pia nakuomba ufike ofisi ya CCM Wilaya Septemba mosi, mwaka huu kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni jimbo la Nzega, aidha jimbo la Bukene itakuwa Septemba 4, mwkaa huu.

Viongozi wengi wa kitanzania hawajui matumizi ya diplomasia katika kuwasiliana na wenzao. Barua hii inamuamuru Bashe akubali kuamriwa na ngazi mbalimbali ilihali kimsingi inatakiwa imuombe ushirikiano wake katika kampeini.
 
Maji yamewafika shingoni sasa wanahaha huku na kule. Siku chache tu walitaka kumtema huyu nje ya Tanzania leo wanampigia magoti! Bila hata ya Kikwete kumuomba samahani hadharani.
 
Katibu mkuu wa ccm, yusuf makamba, alipotakiwa kutoa ufafanuzi na gazeti hili, alisema yeye anatambua wazi bashe bado ni mwanachama wao halali, hivyo viongozi wa mkoa wa tabora wana haki ya kumtumia pale panapohitajika.

"kama katibu wa mkoa wa tabora amemteua, ana haki ya kufanya hivyo, anatambua mchango wake ndani ya chama… hata kama kuna makada 20, kumbuka ndugu yangu hata kanisani utasikia kuna askofu, padri, mchungaji, shemasi, katekista na wazee wa kanisa… hivyo hata ccm tunao wa aina hii,

… kama hilo suala limefikiwa basi ni jema, nadhani wamegundua namna mchango wake unavyotambulika ndani ya chama," alisema makamba..

leo wanasema haya..........na jana walisema hivi

ogwalumapesa said:
katibu mkuu wa chama cha mapinduzi (ccm) yusuph makamba ,amesema kama aliyeenguliwa kugombea ubunge jimbo la nzega na chama hicho hussein bashe,ni raia halali wa tanzania basi anayestahili kubebeshwa lawama ni wasaidizi wa jk na si chama hicho

akizungumza na nipashe jijini dar es salaam jana,makamba alisema chama chake kilipata vielelezo kwamba bashe si raia kutoka kwa wasaidizi wa rais hivyo ccm haistahili lawama

'' wasaidizi wa rais ndiyo walituambia sisi kuwa bashe si raia sasa kama wizara ya mambo inasema ni raia basi ituambie ,lakini leo tunaendelea kuamini tulichoambiwa na wasaidizi wa rais''


source nipashe
HYPOCRITES!!!!!
 
Nitamshangaa sana Bashe akikubali hili na hilo litajidhihirisha wazi kwamba either Bashe huna nia dhati ya kuwatumikia wananzega au ni una agenda nyengine isiyokuwa ya utumishi kwa wananzega inakuyokusukuma ugombanie ubunge. ...Sasa kama unataka unaamini katika unafiki then kubaliana nao but kwa expense ya kuyasahau matakwa ya wananzega!!!

Kwa kweli Bashe atakuwa anawtukana wanaNZEGA...maanake wao ndio walimchagua sasa akirudi kumpigia kampeni Mr WAMA basi atakuwa anawadharau Nzegas.......
 
Hao ndiyo CCM wanakufanya kama kondomu wanakutafuta kwa udi na uvumba wakimaliza haja zao wanakuona kinyaa.
 
Maji yamewafika shingoni sasa wanahaha huku na kule. Siku chache tu walitaka kumtema huyu nje ya Tanzania leo wanampigia magoti! Bila hata ya Kikwete kumuomba samahani hadharani.

Pamoja na kujikoroga kwa CCM, na hila za kumweka Mr WAMA bungeni, nina hoja moja inayomhusu Bashe. Huyu bwana amezaliwa hapa na wazazi wahamiaji ambao si watanzania. Amekulia na kusomea hapa Tanzania hadi eimu ya chuo kikuu. Amekuwa kiongozi wa vijana na CCM kwa muda mrefu. Mwaka 2008 kwakujua kuwa anataka kugombea ubunge akaenda mahakamani kuukana uraia wa somalia, uraia ambao ameutumia kinyume cha sheria kwa kusoma kama Mtanzania na kupata nyadhifa kama mtanzania.

Ninadhani wapo watu walimshauri kuhusu jambo hili na hatari inayomkabili. Kwavyovyote vila Hussein Bashe si Mwadilifu kwasababu amevunja sheria za nchi kwa miaka zaidi ya 25 na sasa anataka aende kwenye jengo akatunge sheria zile zile asizoziheshimu. Kwamamtiki hii sidhani kuwa bashe ana mapenzi na nchi hii, vinginevyo angeukana usomali pale tu alipokuwa na fahamu za uraia wake pengine hata kabla ya kujiunga na chuo kikuu na sio miezi 24 kabla ya uchaguzi.

Tutawezaje kujua kuwa kabla ya september 2008 huyu bwana alikuwa ni mwananchama wa Alshaabab, kwa maana kuwa hakuwa Mtanzania bali Msomali aliyeishi kwa mazoea tu. Narejea tena pamoja na mizengwe aliyowekewa lakini UADILIFU wa Bashe unatia mashaka sana na mbio zake mjengoni pengine si za kuwakilisha wana nzega bali kundi jingine kwa mgongo wa Nzega
 
Yaani hata chembe ya aibu HAWANA! Kweli ukisikia ya hayawani, haya yamezidi!

Oneni aibu kidogo jamani! Mlisema si raia, sasa asiye raia ataweza kweli kwenda kuwapigieni debe jimboni?

Bashe, huu ni uhuni, achana nao. Njoo CHADEMA, ndiko waliko Watanzania wenzako wenye uchungu na nchi yao!

-> Mwana wa Haki
 
Pamoja na kujikoroga kwa CCM, na hila za kumweka Mr WAMA bungeni, nina hoja moja inayomhusu Bashe. Huyu bwana amezaliwa hapa na wazazi wahamiaji ambao si watanzania. Amekulia na kusomea hapa Tanzania hadi eimu ya chuo kikuu. Amekuwa kiongozi wa vijana na CCM kwa muda mrefu. Mwaka 2008 kwakujua kuwa anataka kugombea ubunge akaenda mahakamani kuukana uraia wa somalia, uraia ambao ameutumia kinyume cha sheria kwa kusoma kama Mtanzania na kupata nyadhifa kama mtanzania.

Ninadhani wapo watu walimshauri kuhusu jambo hili na hatari inayomkabili. Kwavyovyote vila Hussein Bashe si Mwadilifu kwasababu amevunja sheria za nchi kwa miaka zaidi ya 25 na sasa anataka aende kwenye jengo akatunge sheria zile zile asizoziheshimu. Kwamamtiki hii sidhani kuwa bashe ana mapenzi na nchi hii, vinginevyo angeukana usomali pale tu alipokuwa na fahamu za uraia wake pengine hata kabla ya kujiunga na chuo kikuu na sio miezi 24 kabla ya uchaguzi.

Tutawezaje kujua kuwa kabla ya september 2008 huyu bwana alikuwa ni mwananchama wa Alshaabab, kwa maana kuwa hakuwa Mtanzania bali Msomali aliyeishi kwa mazoea tu. Narejea tena pamoja na mizengwe aliyowekewa lakini UADILIFU wa Bashe unatia mashaka sana na mbio zake mjengoni pengine si za kuwakilisha wana nzega bali kundi jingine kwa mgongo wa Nzega

"UPO SAWA KABISA" jamani huyu BASHE lazima muelewe kuwa ni mwanamtandaoUFISADI maana siku zote anafadhiliwa na ROSTAM AZIZ (RA) na hiv sasa ni muajiriwa wa NEW HABARI COP. mali ya RA je mnategemea nini kutoka kwake? Huyu bwana ndani ya UVCCM ndiye aliye kuwa anatakiwa na RA na EL kuwa mwenyekiti wa UVCCM. Hawezi kujivua KASHFA ya kumuangamiza NAPE NAUYE hadia akavuliwa uanachama wa UVCCM. Baada ya kummaliza NAPE akaanza kutimiza ndoto za kuutaka uenyekiti hapo ndipo alipokosana na RIDHIWAN (RIZ 1) maana RIZ 1 alikuwa anaitaji swahiba wake BENNO MALISA ndie awe mwenyekiti. Baada ya timbwilitimbwili lao kuwa kubwa wakati wao wote ni vijana wenye nasaba na UTATU wa SHETANI {JK ,EL na RA (huu ndio utatu wa SATAN ndani ya CCM)} Ndipo JK kumaliza varangati hilo akaamua vijana wa ZENJ ndio wagombee uenyekiti hao ni HASSAN NASSORO MOYO na MASAUNI MASAUNI wakati BASHE na MALISA wakatakiwa kugombea umakamu mwenyekiti. Baada ya uchaguzi MASAUNI na BENNO MALISA wakashinda hapo vita ya ki ALSHABAB ikaanza upya BASHE akaunganisha nguvu na MASAUNI wakati NENNO na RIZ 1 wakaunganisha nguvu na HASSAN MOYO. Kwa kuwa vita aichagui silaha MASAUNI yakamkuta ya kuchakachua umri maana wakina RIZ 1 waliona hiyo ni silaha muafaka ya kumaliza vita. Baada ya dafrao la MASAUNI kinara wa Kambi yao akawa Bw. BASHE.

Ukizingatia rangi yake na muonekano wake haikumuwia vigumu RIZ 1 kujua BASHE atammaliza kwa silaha hipi, kwa kuwa BASHE anaasili ya kipiganaji (AL SHBABA) wakati vita inaanza tu ndani ya UVCCM aliwahi Uhamiaji kuweka mambo level tena kwa kutumia mgongo wa MASHA ndio maana mwanzoni MASHA alipata kigugumizi kuzungumzia uraia wa BASHE maana anajua kuna mkono wake na AJUI NINI KIMETOKEA HADI URAIA WA JAMAA unatiliwa shaka na (mzee wa MSOGA) baba RIZ 1. Maana baba RIZ 1 ktk kikao alisema taarifa alizonazo ni kutoka usalama wa Taifa kwakuwa MASHA sio member wa CC ya CCM ilibidi asitolee maelezo suala hilo hadi alipogundua kuwa hakuna cha usalama wa Taifa wala usalama wa mkoa kumbe ni Usalama wa BAGAMOYO chini ya RIZ 1 ndio chanzo cha taarifa hizo,ndipo akatoa kauli.

Hivyo huyu BASHE ameshikwa pabaya na JK hata na kundi la wakina RIZ 1 ndani ya UVCCM hivyo hana ujanja lazima akale matapishi yake kwa kumpigia kampeni KIGWANGALA tena ikibidi kampeni si tu za nyumba kwa nyumba au za mama JK za kitanda kwa kitanda na shuka kwa shuka zake zitakuwa za chupi kwa chupi maana kesha kuwa mtumwa wa CCM JK na mkumbuke "MTAKA CHA UVUNGUNI LAZIMA AINAME" vile vile BASHE hana fedha, badala yake anategemea ufadhili wa RA na ndiye alimbeba kwa kumpa pikipiki na fedha za kuchakachua wakati wa kula za maoni CCM (source SELELI) na kama mtakumbuka kuna pikipiki ziliibiwa pale SINZA KIJIWENI ofisi za New Habari ambazo zilikuwa maalum kwa kampeni za NZEGA na IGUNGA. Hivyo watanzania tuelewe BASHE ni remote control ya RA, na RA ndiye atampa likizo ili aende kupiga kampeni ili wasimuudhi JK ili waweze kuwa Watanzania maana utanzania wao upo mikononi mwake.

Ni vyema wananchi msiangalie BASHE aliongoza kura za maono NZEGA jiulizeni alishinda bila mkono wa shetani kutumika, je kweli mtu anayefadhiliwa na RA anaweza kuwa mkombozi wa watanzania na wananzega? TAFAKARI KISHA ................................
 
Bashe alitangazwa kuwa sio RAIA sasa hivi ni mwenyekiti wa kamati ya kuangalia muundo mpya wa UVCCM.? Nan arirudi kumtangaza kuwa ni RAIA ? ..nan ana matatizo Bashe au CCM.
 
Suala la uraia wa Bashe lilishamalizwa na idara ya Uhamiaji ambayo ina mamlaka juu ya hilo.
 
Nape kama kweli unataka mabadiliko njoo upinzani tukufundishe kazi,japo itakuwa ngumu kuikamua na kuimaliza damu ya ccm manake inaonekana umekuzwa nayo,kwangu mimi naona kama bahati mbaya yaliyokukuta,lakini jaribu tukusaidie!aghhhhhhhhhh
 
Kingine nillichozungumza ni swala zima la kufungwa kwa vyuo vikuu nchini....nilisema naamini kinachopigiwa kelele sio SERA YA UCHANGIAJI YENYEWE bali ni UTEKELEZAJI WA SERA, hivyo sioni sababu ya serikali kutumia ubabe kufunga vyuo badala yake wakae chini na wadau kujadili namna bora ya kutekeleza sera hii. Najua kuwa iko katikati ya mwaka wa fedha wa serikali lakini muhimu kukubali kuwa yapo matatizo katika utekelezaji wa sera hii, ili njia bora itafutwe kisha tuwe na utekelezaji bora zaidi mwaka ujao wa fedha. Maghembe aache ubabe si jambo la buisara kila mara kufunga vyuo hivi maana tunaanzisha utamaduni mbovu wa kutojadiliana kumaliza matatizo yetu hili sio jema.....
icon14.png


Nimeamini ndugu yangu Nnauye tuko pamoja,shida kubwa ni kuwa katika chama cha Magamba.Wewe hustahili kuwa huko ila kwa kuwa macho na akili ya kuona mambo unayo chukua hatua sasa.Tatizo si MTU bali SYSTEM.
wenzio tuliwahi kuwa huko tukajifunza,tukaelewa na kisha tukaamua.Nguvu ya umma ni slogan nzuri na ni dini ya kutufikisha peponi.TAFAKARI.
 
Kingine nillichozungumza ni swala zima la kufungwa kwa vyuo vikuu nchini....nilisema naamini kinachopigiwa kelele sio SERA YA UCHANGIAJI YENYEWE bali ni UTEKELEZAJI WA SERA, hivyo sioni sababu ya serikali kutumia ubabe kufunga vyuo badala yake wakae chini na wadau kujadili namna bora ya kutekeleza sera hii. Najua kuwa iko katikati ya mwaka wa fedha wa serikali lakini muhimu kukubali kuwa yapo matatizo katika utekelezaji wa sera hii, ili njia bora itafutwe kisha tuwe na utekelezaji bora zaidi mwaka ujao wa fedha. Maghembe aache ubabe si jambo la buisara kila mara kufunga vyuo hivi maana tunaanzisha utamaduni mbovu wa kutojadiliana kumaliza matatizo yetu hili sio jema.....
Kaka naona umefafanua vyema, kwanza nikupongeze kwa kuingia jamvini na kuchangia hoja hii, ninakuomba ujibu na thread nyingine zinazokuhusu humu jamvini, nimepata huzuni sana kuona thread kuwa wachagga waliopo CCM wanajipendekeza, hawa kaka zetu Cyril Chami, Aggrey Mwanri, Beno Malisa na wengine wengi akiwemo dada yangu wa Kilimanjaro mama Nsilo Swai wanaotumikia CCM ina maana wanajipendekeza?? naomba ujibu hoja zinazokuhusu humu jamvini... Ahsante ni hayo tu mkuu
 
Naiheshimu sana forum hii kwani inasaidia kutoa mambo ambyo wakati mwingine hayasemwi na vyombo vingine.Nawashukuru kwa kunikaribisha, napokea kwa heshima kubwa karibu yenu wakubwa, naahidi ushirikiano mkubwa kwa kadri ya uwezo wangu wote.
SASA MAMBO MUHIMU TULIYOONGEA KATIKA KIPINDI CHA MLANGO WA DHARURA NI;

1). Niliunga mkono uteuzi wa wagombea kutoka Zanzibar kugombea Uenyekiti UVCCM. Baadhi ya sababu ni kuwa haya ni maamuzi ya kikao halali cha chama NEC, kwa kuzingatia kuwa hakuna uteuzi ambao usingekuwa na mapungufu, hata huu ninaouunga mkono una mapungufu yake mengi tu, lakini ukilinganisha na uteuzi mwingine kwa MTAZAMO WANGU huu ulikuwa nafuu kuliko mingine. Lakini nilikumbusha kuwa mwaka 2003 niligombea mimi uenyekiti uvccm na kulikuwa na wagombea toka znz ambao hawakurudishwa hivyo sioni sababu ya bara kulalamika leo.
2).Utendaji wa Makamba, nilichosema ni kuwa si dhambi kujadili utendaji wa Makamba kama katibu mkuu wa CCM, tena hata wanachama wa kawaida wana nwajibu wa kujadili hali ya chama chao, KWANI NAAMINI HICHI NI CHAMA CHA WANA CHAMA NA SI VIONGOZI. N a nikaongeza kuwa kikao chenye mamlaka ya kumwajibisha Katibu mkuu wa ccm ni NEC huu ndio utaratibu, hivyo hata baada ya kujadili mwisho lazima malalamiko yaletwe NEC ndo wanaweza kumwajibisha Katibu Mkuu.

3). Nikasema KUGOMBEA URAIS 2010 SI DHAMBI ni huru kwa mwana chama yeyote kwa mujibu wa katiba ya CCM ambayo ndio sheria mama, kwani hata ilani ya uchaguzi inatengenezwa mpya, hivyo sitashangaa kuona watu wanachukua fomu kuomba uteuzi, ndio demokrasia.

4). Nikasema pia si kweli kwamba wanaokosa wanakumbatiwa, inawezekana kwa upande mmoja lakini sio katioka kesi zote, nikatoa mfano wa waliowajibishwa kwa makosa ya Richmond, nikasema hawa walisaliti chama kwani tuliwatuma kutekeleza ilani ya chama wao wakaenda kutekeleza yao.

5.) Nikajibu swala la kufukuzwa uana chama uvccm, nikasema MWENYE AKILI NAJUA NANI MKWELI NANI MWONGO kwani UJENZI MPAKA SASA UNAENDELEA BILA MKATABA, MAPUNGUFU NILIYOYAELEZA NDIYO YALIYOUNDIWA TUME KUREKEBISHWA, SASA MWONGO NA MKWELI IKO WAZI, lakini najua mtu mzima kukiri kosa ni ngumu...maji marefu hapa kwa mzee wangu....

HAKIKA HATUKUMTAJA KABISA HUSSEIN BASHE KATIKA MAZUNGUMZO YOTE, SI MIMI, WALA OMARY KIMBAO AU JERRY SILAA NA HATA MTANGAZAJI KIBONDE, NIMESIKITISHWA NA TAARIFA HIZI KUZIKUTA HUKU, GAZETI LA TANZANIA DAIMA WALICHAPA PIA LAKINI KIMAKOSA, SIKUKANUSHA KULE COZ INGEATHIRI UCHAGUZI KWA UPANDE MMOJA NA HASA MGOMBEA MMOJA.

Namwomba ndugu yangu asituharibie heshima ya forum hii, naamini nimeeleza kwa kifupi yaliyotokea.
Nnauye Jr
Nape tunashukuru kwa kutua jamvini na kutoa ufafanunuzi kuhusiano na jambo hilo na tungelifurahi zaidi kama ungelikua unajitokeza mara kwa mara kutokana na nafasi yako katika chama kuzitolea maelezo baadhi ya hoja.Hii itatusaidia kuepuka majungu,kuna maswala mengi na kero nyingi hivi sasa ambazo ni kubwa kwa wananchi ukimya wa CCM unazaa habari nyingi amabazo ni vigumu kuelewa upi uzushi na upi ukweli.Ombi langu kwako habari namba moja na ambayo kila Mtanzania anaisubiri kwa hamu ni hatima ya kujivua "magamba"Ili kuepuka majungu tufahamishe kwa kifupi swala hili limefika wapi?Maana kuna minon'gono barua zimeandikwa hazikuandikwa,wamekabidhiwa hawakukabidhiwa nk.Ebu tupe kwa ufupi
 
Ajitoe, halafu aende wapi?? nani anataka makapi??
 
Back
Top Bottom