CCM yamwangukia Bashe!

CCM yamwangukia Bashe!

Rev Masanilo,
Be specific on what you want to say or to present. Kinana kagombea nafasi gani ya uongozi leo hii hata tufike sehemu tuhoji uraia wake?
 
Ukizoea kutumwa basi unadhani wote hutumwa hivyo hivyo, hii ni tabia ya ajabu sana. Mimi sijatumwa na mtu au kikundi cha watu. Nikiwa Mtanzania na mwanachama wa JF ninatumia haki yangu kutoa mchango wa mawazo yangu kama raia mwingine yeyote. Hapa tunaangalia maslahi ya nchi, hivyo basi hoja zetu ziwe na mtizamo huo. Unaweza kufafanua kidogo ni kwa namna gani, kiasi gani na akina nani wamevuliwa nguo?
 
Rev Masanilo,
Be specific on what you want to say or to present. Kinana kagombea nafasi gani ya uongozi leo hii hata tufike sehemu tuhoji uraia wake?

Unachotaka kusema tuhoji uraia wale tu wanaogombea uongozi! Hujui dhamana aliyonayo Kinana kwenye nchi hii?
 
Nimeharibu wapi?
umeletea facts zanu kwamba huwa idara ya uhamiaji haifuati taratibu za uraia bali hutumwa na walio "juu" kutoa uraia

Eniwei, tulikua tunalijua hilo lakini hatukutegemea utakuja kuliweka wazi hivyo

i am afraid maagizo kwenye uraia badala ya due diligence ni kuharibu system
 
Ninachoona hapa ni kutofautiana ktk kiwango cha ufahamu. Kabla hatujaenda ndani zaidi naomba kujua kama unajua sheria za Uraia wa Tanzania, na tunafuata utekelezaji wa sheria za Jumuiya ipi?
 
Ninachoona hapa ni kutofautiana ktk kiwango cha ufahamu. Kabla hatujaenda ndani zaidi naomba kujua kama unajua sheria za Uraia wa Tanzania, na tunafuata utekelezaji wa sheria za Jumuiya ipi?

I can sniff where you're heading to!
 
Ninachoona hapa ni kutofautiana ktk kiwango cha ufahamu. Kabla hatujaenda ndani zaidi naomba kujua kama unajua sheria za Uraia wa Tanzania, na tunafuata utekelezaji wa sheria za Jumuiya ipi?
saa hizi ndio unakumbuka sheria wakati umeshasema huko "juu" wanatoaga maagizo watu wapewe uraia??? do you think we are fools to believe kwamba hiyo approach ni kwa bashe pekee???

Shakt... hiyo ndio common practice
 
Acid,

Hapa hatumtetei mtu, ila tunatetea nchi inayoitwa Tanzania, hata kama baba yangu angekuwa amekiuka taratibu na kutoa maagizo hayo ningemsema wazi wazi, maana mimi ninavyoelewa kwa uwezo wangu mdogo nilionao ni kuwa, kuna Tanzania moja tu hapa Duniani, tukiiharibu hautakuwa na Tanzania nyingine ya kwenda.

Kwa mnafiki yeyote atataka kufanya kama ulivyokuwa unadhania, yaani kutokuweka wazi jambo hili. Kwa mtizamo wangu finyu, bado naona sijaliweka wazi jambo hili, bado tunacheza na maneno tu hapa.

Ili mgonjwa apone, anahitaji kunywa dawa. Desturi ya dawa nyingi huwa ni chungu sana. Maamuzi hubaki kwa mgonjwa, kunywa dawa chungu apone au kutokunywa na mwishowe afe. Katika hili napenda kusema ukweli kuwa kuna baadhi ya viongozi wameshiriki kuishinikiza Uhamiaji itoe uraia kwa Hussein Bashe.
 
Jibu swali la msingi ili tueleweshane hapa. Usikurupuke na maneno tu
 
Anyway, ngoja nikatinge mzingo, nisije rudishwa home bure. Majibu ya maswali yangu sijayapata. Next time musipende kuzungumza jambo kama hamlijui au hamna uhakika nalo, mutaumbuka. Hussein Bashe sio Raia wa Tanzania. Kwa herini.
 
Hayo ni matokeo ya mfumo mbovu wa utendaji kazi, na hii ni tip of the iceberg tu CCM na serikali yake inaonekana hakuna mawasiliano kabisa kila mtu anafanya lake matokeo yake wanaishia kupiana lawama tu. What else doTanzanians need kujua kwamba they need CHANGE. it is a pity...it is pathetic!
 
Masha Assitiza Bashe ni Raia: Waziri wa mambo ya Ndani Lawrence Masha ,amesema hana jambo la kuongeza katika Uraia wa aliyekuwa Mgombea ubunge wa jimbo la Nzega Hussein Bashe
Amesema alishatoa tamko kuwa haoni utata wowote kuhusu uraia wake uliosadikiwa kuwa na kasoro hivyo kusababisha chama hicho kumuengua katika kuwania ubunge
Waziri Masha Aliyasema hayo jana akizungumza na Nipashe ,''kuhusu suala hilo nilishajibu siku nyingi kuwa mimi sioni utata wowote wa uraia wa Comrade Hussein Bashe na sina jipya zaidi ya majibu ambayo nilishatoa,''alisema Masha,
 
huyu makamba nae anyamaze tu amedanganywa kiaje so anatuambia raisi wetu ni mbumbumbu kiasi cha kutojua kuchanganua mambo?kama bashe ni raia wa kulaumiwa ni ccm si ndo waliochunguza na wenye dola aache ujinga kwanza mi nashangaa kwanini mpaka leo hajajiuzulu huo ukatibu mkuu haumfai,ila ni kawaida ya ccm mana hata wengine walishawahi kuambiwa sio raia ila walishakuaga hadi wakuu wa wilaya,ndo mtindo wao hao wakiona mtu anashyne wanatafuta jinsi ya kumzima na mwaka huu wanakazi si ajabu pia kuja kusikia dokta slaa sio raia mwashangaa nini sasa
 
Katibu mkuu wa chama cha Mapinduzi (CCM) Yusuph Makamba ,amesema kama aliyeenguliwa kugombea ubunge jimbo la Nzega na chama hicho Hussein Bashe,ni raia halali wa Tanzania basi anayestahili kubebeshwa lawama ni wasaidizi wa JK na si chama hicho

Akizungumza na Nipashe jijini dar es salaam jana,Makamba alisema chama chake kilipata Vielelezo kwamba Bashe si raia kutoka kwa wasaidizi wa Rais hivyo CCM haistahili lawama

'' Wasaidizi wa Rais ndiyo walituambia sisi kuwa Bashe si Raia sasa kama wizara ya mambo inasema ni raia basi ituambie ,lakini leo tunaendelea kuamini tulichoambiwa na wasaidizi wa rais''


Source Nipashe

Makamba usidanganye umma wa watanzania kwa kuwasingizia wasaidizi wa JK, nyie CCM chini ya uongozi wako mlitaka kumwekea fitina dogo kwa sababu zenu kwa kutumia hoja ya uraia ili asigombee ubunge kupitia chama chenu, sasa dogo kalipangua mnaanza kuona aibu. Makamba huu mzigo ni wako huukwepi - Yaani mwaka huu unayo mengi tu mzee wangu bado sakata la ualimu wa shule ya msingi nalo linakukuruka linakufuata. Hatushangai CCM nyie siyo wageni kwetu hili la Bashe si la Kwanza kufanyika yapo mengi tu ya namna hiyo, bahati mbaya hamsoni alama za nyakati.

Na baada ya Bashe kuenguliwa kwa nini hamkumshagua Serelii kugombea ubunge mkamchangue mtu aliyekuwa wa tatu kwenye kura za maoni? Serelii kaamua kufa kiume na tai shingoni ila na yeye angeamua kuita waandishi wa habari na kutoa dukuduku zake hapo CCM Lumumba pangekuwa hapatoshi.
 
Hata huyu Masha nae ni mnafiki tu, kwenye kile kikao kilicho muengua Bashe na yeye si alikuwapo! So kama haoni utata kwenye uraia wa Bashe na anaamini hivyo kwa nini asingesema mule mule ndani? Sasa hivi ndio anakuja na utetezi huu mbele ya waandishi ili aonekane mwema! je amelizungumziaje suala la yeye kutumia uwaziri wake kufake document ili aweke pingamizi kwa mgombea wa Chadema Mwanza?
 
• Yamuomba akaokoe jahazi Nzega

na Kulwa Karedia

CHAMA chama Mapinduzi (CCM), kimegeuka kuwa kigeugeu baada ya kumwangukia aliyekuwa Mjumbe wa Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) na Mjumbe wa Halmashauri Kuu (NEC), Hussein Bashe, kikimtaka akasaidie kukipigia kampeni katika jimbo la Nzega mkoani Tabora. Habari za kuaminika zilizopatikana kutoka Nzega na Dar es Salaam jana, zinasema CCM imeteua zaidi ya makada 20 katika jimbo hilo, kwa ajili ya kukinadi chama hicho ambacho kinaonekana kupata wakati mgumu.

Bashe ambaye alitangazwa na CCM hivi karibuni na kuvuliwa nyadhifa zote na Halmashauri Kuu ya CCM (NEC), kisha kutangazwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi Taifa wa chama hicho, Kapteni John Chiligati, kuwa si raia, kunaibua maswali mengi kama uamuzi huo, ulikuwa sahihi.

Bashe ambaye alishinda kura za maoni kwenye jimbo la Nzega, lililokuwa likishikiliwa na Lucas Selelii, (CCM) na ushindi wake kupewa Dk. Hamisi Kigwangala ambaye amepitishwa rasmi kupeperusha bendera ya chama katika uchaguzi mkuu wa mwaka huu.

Akitangaza uamuzi huo, baada ya kumalizika kwa kikao cha NEC cha mchujo wa wagombea ubunge na Baraza la Wawakilishi, Chiligati, alisema CCM imeamua kumtimua Bashe uanachama na kumuengua kuwania ubunge katika jimbo la Nzega, baada ya kubaini kuwa ni raia wa Somalia.

Alisema uchunguzi uliofanywa na chama hicho kwa kushirikiana na Idara ya Uhamiaji, umebaini kuwa Bashe licha ya kuzaliwa nchini, ni raia wa Somalia na hajaukana uraia wake.

"Bashe sio raia wa Tanzania, alikuwa akiishi kwa mazoea tu. Tulipojaribu kutafuta uraia wake kwa kuwashirikisha watu wa Uhamiaji, walituthibitishia kuwa sio raia, licha ya kuzaliwa nchini na alikuwa akiishi kwa mazoea tu. Hii ni kama iliyowahi kumtokea Jenerali Ulimwengu na ndivyo ilivyo kwa Bashe," alisema Chiligati.

Kwa mujibu wa barua ya Agosti 30, mwaka huu iliyosainiwa na Bagaile B. Lumola na nakala kupelekwa kwa Katibu wa CCM Mkoa wa Tabora, inasoma hivi "Nachukua fursa hii kukupongeza kwa dhati kuwa Kamati ya Siasa ya Halmashauri Kuu CCM Wilaya imekuteua kuwa mpiga kampeni za ubunge kama ulivyopangiwa.

Kwa barua hii nakuomba uwe tayari kupokea maagizo yatakayokuwa yakitolewa kutoka ngazi mbalimbali, pia uzingatie ratiba ya jimbo ulilopangiwa. Pia nakuomba ufike ofisi ya CCM Wilaya Septemba mosi, mwaka huu kwa ajili ya uzinduzi wa kampeni jimbo la Nzega, aidha jimbo la Bukene itakuwa Septemba 4, mwkaa huu.

Nakutakia afya njema na familia yako kwa ujumla ili tukijenge chama chetu na "ushindi ni lazima".

Habari zaidi zinasema mbali ya Bashe, kujumuishwa kwenye kampeni hizo, wamo pia makada 19 pamoja na aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, aliyebwagwa kwenye kura za maoni, Lucas Selelii.

Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba, alipotakiwa kutoa ufafanuzi na gazeti hili, alisema yeye anatambua wazi Bashe bado ni mwanachama wao halali, hivyo viongozi wa mkoa wa Tabora wana haki ya kumtumia pale panapohitajika.

"Kama Katibu wa Mkoa wa Tabora amemteua, ana haki ya kufanya hivyo, anatambua mchango wake ndani ya chama… hata kama kuna makada 20, kumbuka ndugu yangu hata kanisani utasikia kuna askofu, padri, mchungaji, shemasi, katekista na wazee wa kanisa… hivyo hata CCM tunao wa aina hii,

… kama hilo suala limefikiwa basi ni jema, nadhani wamegundua namna mchango wake unavyotambulika ndani ya chama," alisema Makamba.

Kwa upande wake, Bashe alipotafutwa kwa njia ya simu na gazeti, alikiri kusikia tetesi hizo ingawa barua rasmi haijamfikia mkononi mwake.

"Duh kaka hamniachi? Hiyo ndiyo nasikia kwako sijapata barua, lakini ufahamu huu ni wajibu wangu kukisaidia chama nikiwa mwanachama kimeniomba lazima nikisaidie kwa kuwa hilo ni jukumu langu, kwa hiyo tunasuburi barua ikinifikia nitaenda kukisaidia, kuhusu kauli ya mzee Makamba nashukuru alichokisema ndiyo ukweli siku zote nimekuwa mwanachama na nitaendelea kuwa mwanachama mwaminifu na mkweli wa CCM," alisema Bashe.
 
Nitamshangaa sana Bashe akikubali hili na hilo litajidhihirisha wazi kwamba either Bashe huna nia dhati ya kuwatumikia wananzega au ni una agenda nyengine isiyokuwa ya utumishi kwa wananzega inakuyokusukuma ugombanie ubunge. Mie naamini mtu lazima uwe na misimamo katika maamuzi yako.

Watu kama wamekutenga na kukuengua katika ubunge ni wazi hawakutaki na wanajua either ni njaa na tamaa ya kuwa matarajio ya kurejea mjengoni ndio zinazokufanya uwakubalie. Nilifurahishwa sana na mbunge anayeondoka wa bumbuli (William Shelukindo) alipogundua hatakiwi aliwaachia nyama watafune akina makamba na familia yake yeye akaendelea na shughuli zake.

Kwasababu ukiwa nje ya system bwana lolote utakalosema la kutowafurahisha wazee litaeleweka venginevyo na hili linaweza kukuathiri zaidi ya kukujenga. Sasa kama unataka unaamini katika unafiki then kubaliana nao but kwa expense ya kuyasahau matakwa ya wananzega!!!
 
Back
Top Bottom