Ojuolegbha
JF-Expert Member
- Sep 6, 2020
- 1,770
- 1,173
YAH: KULAANI SHAMBULIO DHIDI YA PADRE DKT. CHARLES KITIMA
Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimepokea kwa mshtuko na masikitiko makubwa taarifa za kushambuliwa kwa Katibu Mkuu wa Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Padre Dkt. Charles Kitima, tukio lililotokea usiku wa Aprili 30, 2025, katika eneo la Kurasini, Dar es Salaam.
Kwa mujibu wa taarifa zilizoripotiwa, Padre Kitima alivamiwa na watu wawili wasiojulikana na kushambuliwa kwa kitu butu kichwani na mwilini na kusababisha majeraha mbalimbali.
Tunaungana na taarifa iliyotolewa awali na Makamu Mwenyekiti wa CCM Bara, Stephen Wasira kulaani vikali kitendo hiki cha kikatili na kisicho na utu dhidi ya kiongozi wa dini ambaye amejitolea maisha yake kuhudumia jamii kwa upendo na uadilifu.
Soma Pia: Padri Kitima ashambuliwa na watu wasiojulikana. Inadaiwa hali yake ni mbaya
Chama kinatoa wito kwa vyombo vya usalama kufanya uchunguzi wa kina na wa haraka ili kuwabaini na kuwachukulia hatua kali wahusika wa tukio hili. Aidha, CCM inatoa pole kwa Padre Dkt. Charles Kitima, familia yake, Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania, na waumini wote wa Kanisa Katoliki kwa mshtuko na maumivu yaliyosababishwa na tukio hili.
Tunamuombea Padre Kitima uponaji wa haraka na kurejea katika majukumu yake ya kiroho na kijamii.
CCM itaendelea kushirikiana na taasisi zote za dini katika kujenga taifa lenye kulinda na kuendeleza misingi ya amani, umoja wa kitaifa, mshikamano, heshima na linaloheshimu haki za binadamu.
KIDUMU CHAMA CHA MAPINDUZI
Balozi Dkt. Emmanuel John Nchimbi
KATIBU MKUU
1/05/2025