Christiano Ronaldo
JF-Expert Member
- Feb 14, 2012
- 258
- 41
TENA 10 SI 5:-Mkuu acha Porojo.
Nitajie mambo matano tu yaliyopiganiwa na mbunge Eugene Mwaiposa kuhusu Ukonga.
Pili nielezee kuhusu barabara za Ukonga kipindi cha mvua.
TENA 10 SI 5:-
1. Barabara ya mombasa - kivule pale Mombasa mwanzoni ukonga palikuwa si barabara bali korongo lakini pamejengwa kwa lami na mradi unaendelea kila mwaka.
2. Barabara ya banana kitunda ilifikishwa na Mahanga mbele kidogo ya reli ya tazara lakini mwaiposa ameendeleza kidogo na bado kidogo itafika kitunda stendi
3. Barabara kivule na kipunguni b imeboreshwa hata kama si kwa lami
4. Barabara ya mvuti Msongola inaendelea kujengwa kwa lami na sasa karibu inaungana na mpaka wa Msongola na chamazi
5. Barabara ya kiltex kuelekea Pugu mnadani imeboreshwa sana.
6. Barabara ya nzasa imeboreshwa
7. Hili ndilo jimbo lililojenga shule nyingi za wananchi za sekondari kuliko jimbo lolote Dar miaka ya hivi karibuni - shule 22
8. Mwaiposa amehamasisha sana akina mama na kuwasaidia kuanzisha vicoba na saccos ili kuondokana na umasikini wao na akina mama wengi wanampenda kwa hilo.
9. Juzi ameahidiwa visima virefu vitano vya maji kwenye jimbo lake baada ya kumbana waziri wa maji ili kuongezea visima vilivyopo.
10. Kwa ufuatiliaji wake zahanati za jimbo la ukonga zimeboreshwa sana - nenda kazitembelee
Kuhusu barabara wakati wa mvua, lazima tujue kwamba miaka michache iliyopita maeneo mengi yalikuwa mapori yenye mabonde na mito kadhaa hivyo itachukua muda kidogo kuboresha jimbo hilo lifikie majimbo mengine ya wilaya ya Ilala yaani segerea na Ilala. Hivyo haishangazi hali ya barabara wakati wa mvua kuwa mbaya, lakini zinaendelea kuboreshwa na mwaiposa na serikali ya CCM. Aidha kwa sasa ndipo watu wengi wanahamia ukonga hivyo na maendeleo yatakwenda kwa kasi zaidi sasa.
CDM imekuwa kama Dini vile hata ujue unaongopewa lakn hupingi,kila kisemwacho unashabikia,,,,,,,,,sie ndo tupo ukonga msiokuwepo endeleen kuongea.
jimbo la ukonga ni kubwa na kuna sehemu zina barabrara nzuri zaidi
CDM imekuwa kama Dini vile hata ujue unaongopewa lakn hupingi,kila kisemwacho unashabikia,,,,,,,,,sie ndo tupo ukonga msiokuwepo endeleen kuongea.
Isijekuwa unamaanisha Barabara ya Pugu( Nyerere). Ile si ya Jimbo nadhani na Mwaiposa hana mkono wake pale. Tuachieni wenyewe wanaukonga ndio tunaojua lakini huyu Mbunge Mwaiposa ni hovyo, tunamuona kwenye mitandao tu kama hivi lakini ukweli hilo Jimbo halina barabara tuache blabla. Wewe unakaa wapi kwa sababu mimi nakaa Kivule mbele kidogo ya Mwembeni, wewe kwako wapi Ukonga hii? Mbona mnatuzingua hali ya kuwa kila siku tukiingia mjini lazima tukoshe magari yetu la sivyo yanakuwa vituko, na kila siku tunabadilisha spea za magari yetu kwa kukosa barabara. Kukiri si udhaifu ni kujitathmini ili kurekebisha kilichoharibika. Ila kwa kifupi niseme kwamba, mleteni tena CCM mtu aitwaye Mwaiposa kama mgombea wenu 2015 halafu utakuja tena hapa jukwaani kutoa majibu ya kitakachojiri.
Jimbo la Ukonga ni kati ya majimbo ambayo CCM ina hali ngumu sana na hii ni kutokana na maendeleo duni katika jimbo hilo. Mbunge wa Jimbo hilo Eugene Mwaiposa ni kati ya wabunge ambao hawaongei chochote cha kupigania Jimbo lake. Ni mbunge ambaye ameshindwa kufanya mkutano wowote wa hadhara Jimboni kwake kwa aibu ya kuzomewa na kushindwa kujibu kero za wananchi.
Jimbo la Ukonga barabara zake asilimia 90% ni mbovu na hazipitiki kabisa kipindi cha mvua.Kutokana na ubovu wa barabara hizo kipindi cha mvua wananchi wanatozwa mpaka shilingi 1000/- kutoka kituo kimoja hadi kingine. Hali hiyo imekuwa ni kicheko na mbeleko kubwa kwa chama cha CHADEMA. Kwa sasa CHADEMA ndio inashikilia siasa za Ukonga na wamekuwa wakifanya mikutano mfululizo kwenye matawi na Kata. Kunawiri kwa CHADEMA Jimboni Ukonga kunachangiwa pia na viongozi wa chama hicho ngazi ya Jimbo kushirikiana kwa pamoja kuimarisha chama kwa kufanya kazi bila kuchoka.
CHADEMA wamekuwa wakiwaeleza wazi wananchi kwamba mateso yao yanatokana na kuichagua CCM kwenye uchaguzi uliopita. CHADEMA imekuwa ikiwapa mfano wa majimbo ya Ubungo na Kawe yanayoshikiliwa na CHADEMA jinsi wabunge wake wanavyopiga kelele na jinsi kulivyo na maendeleo makubwa katika majimbo yao. Ni ukweli ulio wazi kwa hali ya CCM jimboni Ukonga ni ya kusikitisha sana.Matawi mengi yanafungwa na kugeuzwa kuwa ngome za CHADEMA.
Na endapo hali ikiendelea hivi hivi ni wazi CHADEMA itapata ushindi mkubwa kwenye jimbo hili uchaguzi ujao na idadi kubwa ya madiwani. Wanachpaswa CHADEMA tu ni kuteua wanachama wanaokubalika kugombea nafasi za Ubunge na Udiwani.
Hii ni Tathmini yangu binafsi baada ya kuzunguka kata zote za Ukonga kwa ziara binafsi kwa kipindi cha wiki mbili.
kwahiyo mwaiposa ndio anajenga barabara sio??
i think Makongoro alicheza na wenzake kuondoa makapi i.e. sehemu mbaya wakitegemea kupoteza part ya jimbo
Segerea kuna CHADEMA wangapi? Ndiyo maana hata Tundu Lissu aliwaambia pale Liwiti mlipomwandalia mkutano wa hadhara wa watu 30 akasema Segerea CHADEMA hakuna kitu. Niambie mkutano wa CHADEMA Segerea uliovutia wananchi? Mwaka 2010 CHADEMA Segerea ilisaidiwa na wana CCM kutokana na magomvi yao hasa kata za Segerea na Kimanga lakini bado kura hazikutosha kwa upande wa ubunge, sasa mnadhani kila siku ijumaa? Mwaka 2015 hakuna magomvi ndani ya CCM Segerea.Masisiem si ukonga tu ndipo yalipokataliwa segerea hata ukitaja neno masisiem unaweza kupigwa mawe!!!magamba ni laana mbaya sana!!
- Chadema wangeenda kuwaelemisha wananchi wa Wilaya ya Hai kwanza kwamba ni kwa nini bara bara zao ni mbovu na hazina lami pamoja na kuwa na Mbunge mmaja wa Chadema kwa miaka 10 sasa, kweli nyani hajioni mwenyewe hivi hali niliyoiona kwa macho yangu majimbo kama Hai, Rombo, Bukombe, Biahramulo, Kasulu, Kigoma Vijijini, kweli kuna mfuasi au kiongozi wa Chadema anaweza kuwa na ubavu wa kuuliza majimbo ya wengine kuliko huko kwenu kwanza? Please kama kweli Wananchi wanatakiwa kchagua mbunge kwa vigezo vya ahadi na Maendeleo ya jimbo then you guys have a big problems, nenda jimbo la mfano yaani jimbo jipya la Wilaya ya Siha jirani na Hai, yaani vitu viwili tofauti kabisa.
- Mkuu sana Chadema hawana la maendeleo ya kuwabeza wegine, Mheshimiwa Mwaiposa yupo vizuri sana na wala hana tatizo, ndio kwanza majuzi World Bank wameleta hela za bara bara karibu zote za Ukonga na Segerea, kwa sababu Mbunge Mwaiposa angetoa wapi hela za bara bara bara?
Le Mutuz
Isijekuwa unamaanisha Barabara ya Pugu( Nyerere). Ile si ya Jimbo nadhani na Mwaiposa hana mkono wake pale. Tuachieni wenyewe wanaukonga ndio tunaojua lakini huyu Mbunge Mwaiposa ni hovyo, tunamuona kwenye mitandao tu kama hivi lakini ukweli hilo Jimbo halina barabara tuache blabla. Wewe unakaa wapi kwa sababu mimi nakaa Kivule mbele kidogo ya Mwembeni, wewe kwako wapi Ukonga hii? Mbona mnatuzingua hali ya kuwa kila siku tukiingia mjini lazima tukoshe magari yetu la sivyo yanakuwa vituko, na kila siku tunabadilisha spea za magari yetu kwa kukosa barabara. Kukiri si udhaifu ni kujitathmini ili kurekebisha kilichoharibika. Ila kwa kifupi niseme kwamba, mleteni tena CCM mtu aitwaye Mwaiposa kama mgombea wenu 2015 halafu utakuja tena hapa jukwaani kutoa majibu ya kitakachojiri.
Which is which, Mwaiposa hausiki na Barabara za Jimbo la Ukonga au Jimbo la Ukonga lina Barabara nzuri? sikuelewi!
jamani tuacheni ushabiki,mama mwaiposa watu wa huku hawataki hata kumuona,barabara ya mombasa - moshi bar ni mbaya mpaka aibu,kila mara naua busha za gari,ccm wajitafakari
Mkoa wa Dar si jimbo la ukonga tu na Segerea yatakayobaki CCM mwaka 2015 lakini pia Ilala, Temeke, Kigamboni na Kinondoni. Kazi iliyopo ni kurudisha Ubungo na Kawe, siyo ku retain yalioko CCM tayari likiwemo Ukonga. Na kwa CCM tunachoangalia ni jimbo kubaki CCM, hatujadili watu kwa sasa kama mnavyomjadili akina Mwaiposa. CCM ndiyo hatimaye itatekeleza Ilani yake Ukonga kufikia 2015 na itamsimamisha mwana CCM bila kujali majina, na atakayesimamishwa atashinda.
Huwa wewe ni kati ya watu ninaowapuuza sana hapa Jamvini.
Wewe ni Mzee wa miaka 60 lakini unaandikaga ujinga usioendana na umri wako.
Nakuonea huruma sana.
Hapa wana Ukonga tunajadili matatizo ya Ukonga wewe unaleta porojo za kilevi.Mtu unashinda kwenye madisko na mabar usiku kucha utatambuaje matatizo ya watu wa Ukonga?
Acha longolongo wewe. Mama mwaiposa ana strategy gani zaidi ya kuwaandalia mabonanza wanaccm ili baadae mkale mitori na supu za makongoro!? Anaogopa nini kuitisha mikutano ya hadhara ili awasikilize wananchi?
Mwaka jana daraja la mongolandege lilivunjika lakini ni sisi tuliosimamia na kuwasiliana na mhandisi wa manispaa ya Ilala hadi likajengwa. Mbunge hakuonekana hata mara moja kuja kusaidiana na wapiga kura wake kujinasua na kukosa kivuko.