CCM yajipanga kutumia mitandao kujiimarisha

tatanyengo

JF-Expert Member
Mar 30, 2011
1,134
280
Katika hali inaayoonekana kutaka kukiimarisha chama hasa kwa kutumia vijana, Chama Cha Mapinduzi kinajiandaa kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, twitter na mingineyo kwa ajili ya mawasiliano. Hayo yamesemwa na Nape Nauye katika mahojiano yake na TBC radio mchana huu. Nape amesema kwa kuwa wapiga kura walio wengi ni vijana ili kuwakamata vilivyo inatubidi tubadilishe mbinu za mawasiliano na tutumie mitandao ya kijamii.

Source:TBC Radio
 
Kama nilivyosema hapo nyuma, Bado hawajui tatizo lao.
Hiyo twitter na fbook, wanafahamu lengo la vijana kujiunga huko ni nini?

Nape anadhani Twist iliachwa kwa sababu iligeuka kuwa mtindo mbaya wa ku-dance! Simply there came a convenient alternative. Sasa tuna Vyama mbadala viiingi kwa nini vijana wabaki CCM. Kuna nafasi? Au anawaita wajiunge kumpa support yeye na nduguze?
 
nawatumie hila zote maadamu nimuozo, hakibadiliki. Wahenga wanasema, "Cha kuvunda hakina ubani"" na "Cha kuvunja hakina rubani".
 
Mbona bosi wake alizikandia midia jamii? CCM imeamua kufanya U-turn? If so, ni watu watu wangapi Tanzania wanatumia midia jamii? Have CCM heard about "Twitter revolutions" or "Facebook revolutions" across the continent? Kama midia jamii inasaidia ku-maitain status quo, mbona akina Gaddafi, etc hawatumii midia jamii kuwasiliana na wananchi? Kama CCM itawasiliana na wananchi kama inavyofanya kwenye gazeti la Uhuru, then there is a big mountain wa kupanda. Kwenye midia jamii hakifichwi kitu. Every thing is discussed naked! Kama wako tayari kwa hilo then, sina tatizo.
 
Wakileta maendeleo ya kweli na kupunguza umasikini wa watanzania badala ya full ufisadi hawahitaji facebook wala mitandao ya jamii.
 
Katika hali inaayoonekana kutaka kukiimarisha chama hasa kwa kutumia vijana, Chama Cha Mapinduzi kinajiandaa kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, twitter na mingineyo kwa ajili ya mawasiliano. Hayo yamesemwa na Nape Nauye katika mahojiano yake na TBC radio mchana huu. Nape amesema kwa kuwa wapiga kura walio wengi ni vijana ili kuwakamata vilivyo inatubidi tubadilishe mbinu za mawasiliano na tutumie mitandao ya kijamii.

Source:TBC Radio

waitumie JF, maana hapa ndio sehemu pekee ambapo mapungufu yao yanaongelewa ki unagaubaga
 
Buahahaha ccm wapuuzi sana, walikuwa wanaoponda watu wanaotumia jamiiforum and whatnot na kusema ooh watumiaji mtandao wengi wako nje ya Tanzania blah blah. Hiyo twitter account ya ccm iko active muda sasa.
 
Teh teh haha haaa Nape Nnauye na CCM yako mnachekesha.

Njoooni huko facebook na Twitter.

Huko tutawauliza Maisha bora yako wapi. Mbona National cake wanagawana Vigogo na mafisadi wakati watanzania wanaangamia kwa umasikini?

CCM achaneni na facebook au Twitter - Serikali ya ccm iache kukumbatia mafisadi ili watanzania waonje matunda ya rasilimali za Tanzania.

Vijana kwenye facebook hawataki longo longo za maneno matamu, vijana watanzania wanataka good life.
 
Waambieni wakimaliza twitter na Facebook wake hapa jamiiforum basi...!
 
Lowassa JF

Mchungaji siku chache sijazo una kazi. Ukicheki tuu emails zako utakuta hizi:

Edward Lowassa wants to be friends. Click here to add him as a friend.
Rostam Azizi has poked you. Follow this link to poke him back!
Andrew Chenge has tagged you in a photo. Click here to view the photo
Jakaya Kikwete has sent you a message. Click here to read and reply the message.
Yusuf makamba is following you on Twitter!
 
Katika hali inaayoonekana kutaka kukiimarisha chama hasa kwa kutumia vijana, Chama Cha Mapinduzi kinajiandaa kutumia mitandao ya kijamii kama vile Facebook, twitter na mingineyo kwa ajili ya mawasiliano. Hayo yamesemwa na Nape Nauye katika mahojiano yake na TBC radio mchana huu. Nape amesema kwa kuwa wapiga kura walio wengi ni vijana ili kuwakamata vilivyo inatubidi tubadilishe mbinu za mawasiliano na tutumie mitandao ya kijamii.

Source:TBC Radio

Tunaye Kiongozi wa ajabu sana, Kikwete! Anafikiri tatizo la CCM ni kutoonekana kwenye midia jamii? Kama angekuwa smart enough angekuwa anatekeleza ahadi zake badala ya kupoteza muda kupambana na CHADEMA! Midahalo yenyewe waliikimbia, sembuse midia jamii?
 
Mchungaji siku chache sijazo una kazi. Ukicheki tuu emails zako utakuta hizi:

Edward Lowassa wants to be friends. Click here to add him as a friend.
Rostam Azizi has poked you. Follow this link to poke him back!
Andrew Chenge has tagged you in a photo. Click here to view the photo
Jakaya Kikwete has sent you a message. Click here to read and reply the message.
Yusuf makamba is following you on Twitter!

Hahahahahahah sina mwanachama cha magamba kwenye Account zangu lol!
 
  • Thanks
Reactions: EMT
Nape ajue umaarufu wa JF unaletwa na majadiliano ya uwazi na ukweli humu hafagiliwi mtu kwa cheo chake wala jina lake awe rais au kiongozi wa dini, sijui huko FB watakuwa wanapongezana na kuonyeshana picha za kina Dokii kama kwa Michuzi wait n see.
 
Back
Top Bottom