VUTA-NKUVUTE
JF-Expert Member
- Nov 25, 2010
- 6,135
- 17,802
Wakati CCM ikiendesha vikao vyake sirini huko Mtwara kwa Kinana kuhutubia wanachama wavaa sare tu,CHADEMA inafanya mikutano ya hadhara. Taarifa rasmi nilizozipata toka Mtwara zinasema kuwa Kinana tangu afike Mtwara amekuwa akifanya mikutano yake kwenye kumbi za starehe,nyumba za mikutano na baa. Vikao vya ndani kwa ndani tu.Halafu waandishi wanaripoti kana kwamba Kinana ameunguruma mbele ya halaiki ya wananchi wenye sare na wasio na sare.
Je, kweli mikutano iliyoamriwa na Mwenyekiti wetu ndio hii? Ni kweli 'spidi' ya M4C itapunguzika kweli na kuirudisha CCM mioyoni mwa watanzania?
Je, kweli mikutano iliyoamriwa na Mwenyekiti wetu ndio hii? Ni kweli 'spidi' ya M4C itapunguzika kweli na kuirudisha CCM mioyoni mwa watanzania?