CCM yajificha,CHADEMA yajifichua

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,135
17,800
Wakati CCM ikiendesha vikao vyake sirini huko Mtwara kwa Kinana kuhutubia wanachama wavaa sare tu,CHADEMA inafanya mikutano ya hadhara. Taarifa rasmi nilizozipata toka Mtwara zinasema kuwa Kinana tangu afike Mtwara amekuwa akifanya mikutano yake kwenye kumbi za starehe,nyumba za mikutano na baa. Vikao vya ndani kwa ndani tu.Halafu waandishi wanaripoti kana kwamba Kinana ameunguruma mbele ya halaiki ya wananchi wenye sare na wasio na sare.

Je, kweli mikutano iliyoamriwa na Mwenyekiti wetu ndio hii? Ni kweli 'spidi' ya M4C itapunguzika kweli na kuirudisha CCM mioyoni mwa watanzania?
 
peoples power. unafikiri kinana atakuwa na ajenda yoyote mpya. obvious mvinyo ni uleule tofauti ni chupa tu
 
Kuhutubia mikutano ya hadhara inahitaji mipango mathubuti na si kukurupuka!
 
Kinana ana uwezo sana wakusafirisha pembe za ndovu kisirisiri, wanafikiri pia ataweza kuifaulisha CCM hivyohivyo kisirisiri, yaani logic yao ni kwamba kama mtu aliweza kupitisha mzigo wa pembe za ndovu kimyakimya basi ataweza pia kukufaulisha CCM kimyakimya hivyo
 
Hata mimi nilidhani wataunguruma kwenye mikutano ya hadhara kumbe baani!! ccm kushnei.SOMA ALAMA ZA NYAKATI.
 
Sasa Kinana atawaambia nini ndugu,jamaa na marafiki wa vijangili vidogo vilivyoko gerezani, vilivyokuwa vinawinda swala kwa ajili ya kitoweo huku yeye Kinana anasafisha nyara za gharama kisha anapewa Ukatibu ccm?
 
Kumpa Kinana ukatibu mkuu ni dalili kuwa CCM imeishiwa watu wasafi. Huyu bwana amekuwa na kashfa za chinichini nyingi na hata hajamaliza wiki kwenye cheo kipya tayari kampuni yake inatajwa kwenye issue ya pembe za ndovu
 
Kuungurum hadharani usifanye mchezo!!! bora CDM watu hujitokeza wenyewe ktk mkutano! ila wenzetu nyinyiem huingia gharama kubwa sana kulipa watu na kuwasafirisha ili kujaza uwanja waonekane wapendwa na wengi kumbe wa kukodi! sasa kulianzisha kujibu nchi nzima gharama yake hawana sasaivi! ni kama kampen za Urais gharama karibia!!

Hivyo ni bora kufanyia vikao BAR ili ku-save gharama za mkutano!! ndicho anachofanya kinana huko Mwara!!!
 

Similar Discussions

1 Reactions
Reply
Back
Top Bottom