CCM inajijenga wakati CHADEMA inaendelea kulalamika!

voicer

JF-Expert Member
Jul 13, 2020
5,553
11,885
Huu mchezo wa siasa ni mtamu sana!

Miaka zaidi ya 30 ndani ya siasa za upinzani nchini. Ni wazi kwamba CHADEMA bado haijajua jinsi ya kupanga karata zake.

Badala yake tunaiona CHADEMA ikibaki kuwa mcheza ngoma wa CCM.

Mfano hai ni jinsi Paul Makonda wa CCM anavyozunguka nchini kuiamsha CCM, ambayo imelala kwenye Ubadhirifu na Ufisadi lukuki, na huku CHADEMA wakimfuatilia na kupambana nae kwa maneno yaleyale ya miaka yote.

Tunamuona Lissu akiwa ughaibuni akiendelea kulalamika kushambuliwa kwake.

Pia tudisahau Mbowe alikataza wafuasi wake kumuunga mkono Mwabukusi na "Sauti ya Watanzania" kutumia platform ya Chadema kwenye mikutano yao Dsm na akawazimia simu ilhali walikwisha wekeana "MoU"

Sasa Mbowe yeye yuko kimya anapambana kutafuna Ruzuku ya asali aliyolambishwa kupitia kwa Kinana!

Wafuasi wa CHADEMA wanaandamana na Makonda mitandaoni kwenye ziara yake ya Uhamasishaji wa Pro-Magufuli.
 
Hakuna chama chenye uwezo wa kuitikisa wala kuisumbua CCM Katika sanduku la kura.hii ni kutokana na uimara wake, mfumo wake imara pamoja na mtandao mpana wa uongozi mpaka ngazi za Mashina huko ndani vijijini kabisa. CCM imekuwa na utamaduni wa kubadilika kulingana na wakati ili kukidhi mahitaji ya mabadiliko, na hili imelifanya na inafanya kupitia ilani yake katika kila uchaguzi.

CCM Inabeba sera na ajenda zinazogusa maisha ya watanzania wanyonge nakuhakikishia kuwa zinatekelezwa kikamilifu pasipo kusuasua lakini pia CCM kimekuwa ni chama chenye kuwatetea wanyonge na kuhakikisha kuwa wanapata haki zao. Usikivu wa CCM na Serikali yake vimekuwa ni vitu vinavyoendelea kuvuta maelfu kwa mamilioni ya wanachama kila mwaka.

Ukija vyama vya upinzani kama CHADEMA havina hata uwezo wa kuandaa tu ilani yake wala kuandaa mgombea urais ,hapa unaweza kurejea kilichotokea 2015. Ni vyama visivyo na muelekeo wala dira.havieleweki vinasimamia nini na vinapigaia nini.

Vimebeba taswira ya mkusanyiko wa watu waliokwaajili ya kusaka madaraka na kuneemesha matumbo yao ,ndio mama hakuna sera wala hoja ya kugusa maisha ya watu zaidi ya kupigania vitu wanavyoona vitawasaidia kupata madaraka ya ubunge na udiwani ili wakatafune kodi za mtanzania. upinzani haijawahi kuwa na maslahi na wananchi na wala hawana uchungu na maisha ya watanzania kama ilivyo kwa CCM ambacho kimekuwa na uchungu na maisha ya Watanzania.
 
Ndugu yetu...

Lucas mwashambwa !
Bila kumumunya Maneno..
Kuna ukweli ndani ya andiko lako pale ambapo CCM inapojua jinsi ya kucheza na akili ya watanzania!
CCM imetumia uzoefu wake kwenye siasa za nchi hii, kujua ni wapi na lini waweke nini, na pia nani wamuweke kwa wakati husika kuendana na mahitaji ya wakati!

Mfano!
Kuna kundi Remote!

Wamemtumia "Makamba" akatufunga "Kamba"wakapiga vya kuwatosha kufanyia kampeni zao binafsi hadi na kusaza!

Na kisha sasa wanatuletea "Makonda" na sasa anawapiga "Makonde" ya Ulaghai wananchi ili kujenga Daraja la kuvukia Uchaguzi wa serikali za Mitaa na pia Uchaguzi mkuu wa 2025.

CCM wamegundua kwamba bila kulitafuta kundi la wafuasi wa Magufuli hususan huko kanda ya Ziwa!
Mambo hayatakuwa Shwari kabisaa!

Makonda ametumika kama Mbeleko ya kanda ya ziwa baada ya ile ya Biteko kukwama!
Hiyo imeenda ndugu yangu.

Lucas mwashambwa !
 
Ndugu yetu...
Lucas mwashambwa !
Bila kumumunya Maneno..
Kuna ukweli ndani ya andiko lako pale ambapo CCM inapojua jinsi ya kucheza na akili ya watanzania!
CCM imetumia uzoefu wake kwenye siasa za nchi hii, kujua ni wapi na lini waweke nini, na pia nani wamuweke kwa wakati husika kuendana na mahitaji ya wakati!

Mfano!
Kuna kundi Remote!
Wamemtumia "Makamba" akatufunga "Kamba"wakapiga vya kuwatosha kufanyia kampeni zao binafsi hadi na kusaza!
Na kisha sasa wanatuletea
"Makonda" na sasa anawapiga "Makonde" ya Ulaghai wananchi ili kujenga Daraja la kuvukia Uchaguzi wa serikali za Mitaa na pia Uchaguzi mkuu wa 2025.

CCM wamegundua kwamba bila kulitafuta kundi la wafuasi wa Magufuli hususan huko kanda ya Ziwa!
Mambo hayatakuwa Shwari kabisaa!

Makonda ametumika kama Mbeleko ya kanda ya ziwa baada ya ile ya Biteko kukwama!
Hiyo imeenda ndugu yangu..
Lucas mwashambwa !
😄😄😄
 
Back
Top Bottom