CCM yahalalisha rushwa Igunga - Yaibana TAKUKURU | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

CCM yahalalisha rushwa Igunga - Yaibana TAKUKURU

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Candid Scope, Aug 30, 2011.

 1. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #1
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  WAITUMIA TAKUKURU SALAMU

  CCM kimesema kuwa fedha zilizogawanywa miongoni mwa wajumbe wake katika kura za maoni Jimbo la Igunga hazikuwa za rushwa, bali zilitolewa na chama.

  Maelezo hayo yametolewa na chama hicho kufuatia taarifa za wanachama wake watatu kushikiliwa na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru) katika eneo la ukumbi wa mkutano wa kura za maoni na baadaye kuachiwa.


  Mwigulu aliwataka maofisa wa Takukuru kuwa makini katika kutekeleza majukumu yake kwa kufuata kanuni na taratibu zao za kazi.


  Mwigulu alisema Takukuru inapaswa kutambua kuwa CCM inapowaita wajumbe kutoka sehemu mbalimbali kwa ajili ya mikutano na vikao, gharama za uendeshaji ni juu ya chama na ndicho kilichofanyika katika mkutano huo. "Sisi kama Chama Cha Mapinduzi tunapoita wajumbe kutoka sehemu mbalimbali hatutarajii wajumbe wetu wajitegemee, ni CCM inayoingia gharama zote kuanzia kusafiri, kula na kulala hadi mkutano utakapokwisha," alisema Mwigulu.


  Alisisitiza kuwa hicho ndicho kilichofanyika Igunga kwa kuwapa wajumbe fedha baada ya kufika mkutanoni. "Ninasikia ni kuwa TAKUKURU waliwakuta mkutanoni hapo na si kwinginepo," alisisitiza. Mwigulu alisema Takukuru na vyombo vingine watambue kuwa fedha hizo hazikuwa za wagombea bali ni mfuko wa chama.

  Alisema: "Taasisi itambue kuwa vipo vikundi vya uhamasishaji ambavyo vinakusanywa kwa ajili ya maandalizi, ni wajibu wa CCM kuandaa na kugharimia safari zao na malazi hivyo ni wajibu wa taasisi (Takukuru) kupata maelezo kuhusiana na hilo isijekutokea wakadhani kuwa wanapewa rushwa."


  Aidha, akizungumzia uchaguzi huo, Mwigulu alisema wakati vyama vya siasa vikikimbilia kuchukua fomu, CCM inajipanga kwa ajili ya ushindi mkubwa na wa kishindo.

  "Ninachotaka kuwaambia kuhusiana na uchaguzi ujao ni kwamba, ushindi uko wazi kwa CCM kwa kuona mtaji mkubwa uliopo na hasa vijijini," alisema. Alisema kuwa vyama vinapaswa kujipima na bora kujitoa mapema kuliko kuanza malalamiko na kukimbilia Takukuru.


  IPPMedia
   
 2. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #2
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Thana ya kutoa rushwa inamhusu mtu binafsi tu au kikundi, kampuni au chama wanaweza kutoa rushwa kwa malengo ya kufanikisha jambo fulani kwa manufaa yao?
   
 3. Mpaka Kieleweke

  Mpaka Kieleweke JF-Expert Member

  #3
  Aug 30, 2011
  Joined: Feb 27, 2007
  Messages: 4,137
  Likes Received: 67
  Trophy Points: 145
  Takukuru wanapaswa kutumia ile sheria ya gharama za uchaguzi kwani kama wakikutwa wanagawa fedha kwa watu na ambao majina ya watu hao sio miongoni mwa timu ya kampeini basi wakamatwe maana na wapokea rushwa.
   
 4. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #4
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Nawashauri wanaigunga msikubali virushwa havitawasaidia na mtateseka kwa miaka minne ya jasho na damu kuweni makini jamani
   
 5. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #5
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  <br />
  <br />
   
 6. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #6
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,822
  Likes Received: 10,120
  Trophy Points: 280
  yale yale yaleeeeeeeeeeeee
   
 7. M

  Mthuya JF-Expert Member

  #7
  Aug 30, 2011
  Joined: Jun 9, 2011
  Messages: 1,415
  Likes Received: 65
  Trophy Points: 145
  Hapo iangaliwe sheria ya uchaguzi , aiwezekani ugawe pesa wakati wa uchaguzi useme ni posho mbona awakugawa wakati si wauchaguzi? Jamani ccm hacheni vi2ko mmetuchosha jamani
   
 8. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #8
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa nini vyama vingine vya siasa vinavyoshiriki uchaguzi havilalamikiwi na mambo haya ya kugawana posho kutoka vyama vyao vya siasa? Mazingara ya ugawanaji pesa kama ni kwa utaratibu wa kawaida isingetiliwa shaka kama kwenye vyama vingine mambo yanaenda kwa mfumo na utaratibu usiolalamikiwa. Mazingira haya ya CCM kwa vyo vyote yanatia shaka na kuanza kuwazipa kipao TAKUKURU kwa vitisho kitu ambacho kinaashiria hali isyo ya kawaida kwamba na dhana ya rushwa ya uchaguzi kwa wapiga kura.
   
 9. Sikonge

  Sikonge JF-Expert Member

  #9
  Aug 30, 2011
  Joined: Jan 19, 2008
  Messages: 11,503
  Likes Received: 539
  Trophy Points: 280
  Helmut Kohl CDU-party finance scandal.

  A party financing scandal became public in 1999, when it was discovered that the CDU had received and kept illegal donations during his leadership.

  Investigations by the Bundestag into the sources of illegal CDU funds, mainly stored in Geneva bank accounts, revealed two sources. One was the sale of German tanks to Saudi Arabia (kickback question), while the other was the privatization fraud in collusion with the late French President François Mitterrand who wanted 2,550 unused allotments in the former East Germany for the then French owned Elf Aquitaine. In December 1994 the CDU majority in the Bundestag enacted a law that nullified all rights of the current owners. Over 300 million DM in illegal funds were discovered in accounts in the canton of Geneva.

  The fraudulently acquired allotments were then privatized as part of Elf Aquitaine and ended up with TotalFinaElf, now Total S.A.

  Mwisho lazima tuseme wazi kuwa hata EPA ilikuwa ni pesa kwa ajili ya chama na WABUNGE WOOTE wa CCM, ukianzia akina Sitta, Mwakyembe, Mwandosya, Magufuli nk hadi kwa Mafisadi woote walivuta Milioni tano za EPA. Ndiyo maana hutasikia wakisema kitu.

  Huyo Mkapa, ni wa kuzomea huko Igunga kwani Ufisadi uliokubuhu ni yeye aliuleta.
   
 10. H

  Hofstede JF-Expert Member

  #10
  Aug 30, 2011
  Joined: Jul 15, 2007
  Messages: 3,584
  Likes Received: 32
  Trophy Points: 0
  Kama CCM huwa inagawa hela kama njugu kwenye mikutano yao, swali linakuja je: Ni wapi utakapopatikana uthibitisho wa malipo kama hakuna kusign kwa mpokeaji wa malipo? Je auditing ikifanyika source documents zinakuwa confirmed vipi?, maana kuandika tu kiasi kadhaa kimetumika kwa malipo haitoshi kama hakuna evidence hiyo from mlipwaji?

  Je CCM ndiyo inavyofanya hivi kuwalipa watendaji wake?, kama ndiyo basi watakuwa ni wakwepa kodi wakubwa sana. Huyu Mwigulu ninaamini atakuwa amepitia pale mlimani BCOM, atueleze wale wataalam wa uhasibu na fedha ndiyo walimfundisha awe analipa pesa kama njugu bila ya kurecord?. Tukisema kuwa Mwigulu ni Fisadi aliyewalipa watu kumi na kuandika kalipa mia tutakuwa tumekosea>

  My take

  Malipo yote halali ni lazima yawe na utaratibu ufuatao
  1. unakuwa na list ya majina ya walipwaji au unayaandika

  2. Wakati wa kumlipa mtu anasaini kuwa kapokea kiasi kadhaa kwa ajili ya kadhaa

  3. Kama unamlipia mtu usafiri, malazi na chakula wakati akiwa kishafika eneo la tukio basi kwenye usafiri utatakiwa kukusanya risiti za usafiri ili kuwa-refund pesa waliyotumia, otherwise uwalipe kabla ya kusafiri. Je Mwigulu alilifanya hilo?

  Kama hayo ya juu yamefanyika Mwigulu yupo sahihi ila kama jayakufanyika mwigulu alikuwa anagawa RUSHWA. Maana kumpatia mtu monetary assets without accounting for, at a time when you need a favoirable return (Assisting CCM to win an election) from him/her is CORRUPTION and nothing else.
   
 11. Buchanan

  Buchanan JF Diamond Member

  #11
  Aug 30, 2011
  Joined: May 19, 2009
  Messages: 13,203
  Likes Received: 371
  Trophy Points: 180
  Hata CUF walidai kwamba wanawalipa posho mawakala waliosimamia uhesabu kura uchaguzi mkuu wa mwaka 2010!
   
 12. jogi

  jogi JF-Expert Member

  #12
  Aug 30, 2011
  Joined: Sep 25, 2010
  Messages: 19,335
  Likes Received: 12,801
  Trophy Points: 280
  mwigulu, tafadhali mwigulu, mwigulu torati yasema(usimtokose mwana mbuzi pamoja na maziwa ya mama yake) kama hujui tafsiri ya maneno hayo nakushauri ufunge kisha umlilie mungu akutendee muujiza wa sauli kwani hakika unamuudhi mungu, na umeshupaza shingo kama farao, hivi ni kweli unapenda kaka zako waendelee kuwa watumwa. damu za watu wangu na ziwe juu ya kichwa chako na familia yako, hakika mungu awanyesheaye mvua sisimizi, mijusi na vipepeo atayachunguza mapito yako sawa sawa na mapenzi yake.
   
 13. MtamaMchungu

  MtamaMchungu JF-Expert Member

  #13
  Aug 30, 2011
  Joined: Apr 10, 2011
  Messages: 3,695
  Likes Received: 507
  Trophy Points: 280
  Kweli kazi ya TAKUKURU ngumu, watu wanatumia mbinu zote kuhalalisha rushwa. Sheria ya gharama za uchaguzi ipo wapi?
   
 14. mshikachuma

  mshikachuma JF-Expert Member

  #14
  Aug 30, 2011
  Joined: Dec 2, 2010
  Messages: 2,853
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Mkuu nakubariana na wewe kabisa! yaani umeongea point za kushiba. CCM ni sawa na jini linyonyalo damu
   
 15. p

  politiki JF-Expert Member

  #15
  Aug 30, 2011
  Joined: Sep 2, 2010
  Messages: 2,356
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  TRA JE MNAKATA KODI MALIPO HAYA.
  Kama kawaida yakifanyika malipo ya aina yeyote lazima kodi ikatwe kama ambavyo unapokwenda kununua kitu dukani au unapolipwa posho, mshahara au bonus lazima ikatwe kodi. je wahusika hawa wanalipa kodi kwenye pesa wanazogawiwa kama njugu ?? hii ni rushwa ya wazi na ni
  lazima takukuru wachukue hatua na chadema kwanini msitafute kamera ndogo ili kuwarekodi wakati wanagawana pesa hizi.??
   
 16. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #16
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Bwana Mkubwa

  Kwa expirience niliyo ipata kwa last campaign huku Dodoma mkuu ni kuwa CCM wanapenda pesa esp wale wapiga kura wao hupewa posho ambazo wao huziiita takrima na unakuta katika makundi yao kabisa wana weza kupishana kwa ajiri ya hivyo vijisenti hilo liko wazi CCM humwaga pesa na Tsht kofia na kadharika.

  Takukuru ndio kabisaaa usisema ndio Corrupt wa kuwanza kwenye hizi kampeni na hapo ndipo muda wao wa mavuno wana twist stories Dodoma nilishuhudia yule Gulam anapewa story ya kimbisa kafanya nini na hao Takukuru na wakawa wana sema lazima wamwangushe tuu hapo takukuru hajashili kupokea rushwaa mkuuu hebu niambiene.

  Hii hali ya kupeana pesa hutengeza uhasma baina ya ndugu, jamaa, koo hapa na pale kisa tu ni uchaguzi namtaka fulani kwanini tusimchague tu mtu kwa sera zake za kutushawishi tu kuliko kutanguliza pesa???
   
 17. W

  We know next JF-Expert Member

  #17
  Aug 30, 2011
  Joined: Sep 9, 2010
  Messages: 664
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 35
  Watakao chagua chama kwa kupokea rushwa kwa nyakati hizi, kwa kweli historia itakuja wahukumu.
   
 18. mashikolomageni

  mashikolomageni JF-Expert Member

  #18
  Aug 30, 2011
  Joined: Jan 5, 2010
  Messages: 1,565
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  hiyo ni kauli ya mwigulu na serikali yao ya mafisadi hakuna ukweli zaidi ya kuwa walikuwa wanagawa rushwa maana taratibu za posho zinajulikana rate/day na fare hulipwa kulingana na umbali wa mjumbe baada ya kuonesha tikiti ya usafiri unaokubalika. Hawezi kukiri kuwa naye ni GAMBA anayetakiwa kujivua/kuvuliwa
   
 19. Jethro

  Jethro JF-Expert Member

  #19
  Aug 30, 2011
  Joined: Mar 23, 2009
  Messages: 2,223
  Likes Received: 98
  Trophy Points: 145
  Na hao ndugu zangu wa Igugnga watafanya hivyo ujue kwani watatishiwa kuwa anagalieni CCM ilicho wafanyieni kipindi cha Rostam yote hayo yalipitia kwa CCM kutatokea maneno ya ajabu lakini ukija baini undani wa maendeleo ya ndugu zangu hapo ingunga utachoka maana upendeleo wa kuleta maendeleo ulitizamwa kweli katika kila wilaya?????
   
 20. Candid Scope

  Candid Scope JF-Expert Member

  #20
  Aug 30, 2011
  Joined: Nov 8, 2010
  Messages: 11,896
  Likes Received: 119
  Trophy Points: 160
  Kwa hoja TAKUKURU kuwahoji wahusika kisha kuwaachia bila kuchukua hatua ni dalili ya kuwa ni washiriki wa kubwa wa rushwa. Maana katika uchaguzi wa mwakajana walichachamaa kipindi cha wanamagamba walipokuwa wanateuliwa, lakini kwenye kampeni za vyama vyote na kuchaguzi baada ya wanamagamba kuwa na wagombea wao rasmi licha ya urshwa kushamiri lakini nichoshuhudia TAKUKURU kuwa likizoni.
   
Loading...